Wewee Yanga hakuna Watindiga wewe,ulishawahi kuona Yanga imesajili kwa kuonyesha picha ya Mwenyekiti amemshika bega mchezaji tajwa msajiliwa halafu wakashangilia,umeshawahi kusikia katika mkutano wa Yanga taarifa ya mapato na matumizi ikasomwa kisanii na wana Yanga wakashangilia,umeshawahi kuona wana Yanga wamechangia rambirambi za mpendwa wao zikaliwa na Viongozi wao na wao wakakaa kimya,umeshawahi kuona Yanga imeuza wachezaji nje wana Yanga wasihoji fedha iliyopatikana imetumikaje badala yake wakazidi kukamuliwa kwa kuchangishwa kwenye mkutano mkuu....hivi unafahamu kuwa kupata taarifa ya mapato na matumizi hata kwa wewe mshabiki njaa wa huko madongo kuporomoka kwako unakoishi ni haki yako? halafu unajisifia kwa kuchangishwa,kama kuchangishwa pasipo kupata maelezo ya kina ya sababu za kuchangishwa au mapato yaliyopatika katika mwaka wa fedha uliotangulia yametumikaje ni ujanja basi mimi binafsi nitakuwa Mtindiga namba 1 kwani siwezi kukubali hata siku 1.
yaani hicho chote ulichoandika ndo kimedhihirisha namna gani ulivyo mtindiga tena aliyekomaa hadi anatoa unga...! Tena we hujui chochote kuhusu hata hiyo yanga yako. Ila kwa kukusaidia tu hebu kumbuka habari za Costa na Amri said ilikuwaje? Yanga haikuingia cha kike? huyo twite mwenyewe mbona mmekubali kurudisha pesa kama sio utindiga ni nini? Eti klabu kubwa ina wasomi lakini inakuja kuburuzwa na mzee Akilimali ambaye hata ukimpa The Guardian hajui kilichoandikwa kama sio utindiga nini? Timu yenye washabiki wa kuridhisha lakini wanaosubiri kulipiwa na kupewa kadi za bure na mwenyekiti kama sio utindiga ni nini..? Mkadanganywa kagere anakuja, mkasubiri u/taifa holaaa...! Kama sio utindiga nini..? Kama uwanja jengeni kwa kuwa ni kitu muhimu na cha maendeleo, na pia kitaleta changamoto kwa simba nao kuacha longolongo. Wasichotaka watu ni hizi kelele na tambo zisizo na maana. Isije ikawa kama msanii underground anayewadanganya rafk zake kila wakati anaenda kutoa single lakini wapi. Anaishia kuwaimbia kijiweni hadi anafulia. Chukueni hatua hatutaki stori.