Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Tumechokaa na hoja zenu zisizokuwa za msingi, kuna mambo mengi sana ya kuzungumzia tofaut na EL, ongeleeni bsii ata hyo japo utendaji wenu ni mdogo, na wanajamii frm mkafika mahali mbadilike tunapelekeshwaa sana na hawa wanasiasa ehhh
 
Lowasa kiboko, akipiga chafya Lumumba yote inatikisika, je akija 4WD si ndiyo mwisho wa CCM? Kusema ukweli CCM wooooooooooooooote wanamgwaya huyu jama yaani hawamuwezi.

Waige toka CDM jamani....tuuone uwezo wao wa kufanya maamuzi magumu.
 
waliogopa kuwafukuza madiwan bukoba ndo,wataweza kumfukuza lowassa? wakifanya hivyo hawatakawia kusema kikao kilichofikia hayo maamuzi kilikuwa batili
 
Maneno mingi vitendo sifuli, hv wakati anaingia madarakani alisema wale wote walopita kwa rushwa watawajibishwa. Kwa hiyo porojo zake hazifai.
 
lowasa songambele usisikilize maneno ya kukatisha tamaa. pigana hadi dakika ya mwisho utashinda tu
 
CCM ni wepesi wa kusahau mambo wameshasahau kilichowapata kwa Mwakalebela. Kisiki cha mpingo aslani hakikatwi kwa panga. Wakimuengua Lowasa kwa staili hiyo mtu mwenye wafuasi wengi kutoka kila kona ya nchi, mtu mwenye wafuasi hadi ndani ya halimashauri kuu na kamati kuu yake watachochea hasira ya wapiga kura. Kama wanataka hayo yatokee na wamuengue Lowasa halafu itakuwa majuto ni mjukuu.
 
mangula makamu mwenyekti wa ccm taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya edward lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na ccm kama mgombea wake wa urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa ccm labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana lumumba ccm sub hqs!

-------------------------



------------------------------

ccm waamua kumtelea uvivu lowassa mbio za urais 2015



unaweza kusema sasa chama cha mapinduzi (ccm) kimeamua kumfungia kazi waziri mkuu wa zamani, edward lowassa baada ya jana makamu mwenyekiti wake (bara), phillip mangula kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015 watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;

“wapo watu wanataka waichanechane ccm kwa sababu ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi kuyafumbia macho.”

akifafanua hilo mangula alisema: “tutawaita wote walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu, tunajua dhamira yao ni nini.”

mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tangu katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, nape nnauye kusema mwanachama yeyote wa ccm anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.

Nape alitoa kauli hiyo baada ya lowassa siku mbili zilizopita, kutangaza nia ‘kimtindo’ akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia ccm katika uchaguzi mkuu wa 2015, alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania (kkkt), usharika wa monduli.

Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho wanaoutaka urais jana katika kikao cha halmashauri kuu ya kamati ya siasa tawi la ofisi ndogo za chama hicho lumumba, wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wote wa ccm nchini.

Ataja kanuni za uongozi

katika mkutano huo mangula alisaidiwa kusoma kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali na katibu tume ya udhibiti wa nidhamu ya viongozi wa ccm na wanachama taifa, masoud mbengula.

Moja ya kanuni hizo inasema “ni mwiko kwa kiongozi wa ccm kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono.”

mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.

mzee wangu mangula lowas kitu gani mbona wezi wa escrow mmewalinda msitufanye watanzania maboya time will tell kama rais ni lowassa hata mkichimba shimo refu kumzika litawazika weneywe tumesha wajuwa nyie ni wanfiki ungali yasema hayo wakati pinda kajiuzulu ningewakubali ila sasa tumejuwa mnamchkia tu huyu mzee kwa sababu nyota yake ina ng'aaaaaaaa
 
Bado atawatesa sana subirini mud a ukifika
Mkamsalimie mjengoni
 
Huyu punda amekulahela ya escrow ujamuonahata anaongea kama nanii was chama
 
Pengine ule utabiri wa Mwalimu utatimia safari hii. (Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM)

Na sasa sijaona tofauti na ule wakati wa kuelekea 2005 wakati huo JK akipambwa na vyombo vya habari. Ngoja tusubiri wapasuane Wenyewe ili iwe nafuu ya wachukuzi.
 
nec mpendwa wetu kiongozi mahili mchapa kazi mpenda maendeleo unafaa kuwa rais

kwa kuwa ripoti ya daktari inasema hutakiwi kufanya kazi ngumu tunatoa fomu ya kimyang'anyiro cha urais

unahitajika tukae meza kuu kupitsha majina ya wagombea mh EL
 
unawaacha akina chenge na tibaijuka unataka lowasa aondoke we mzee umechanganyikiwa
 
Waungwana, kupitia taarifa ya habari ya channel ten makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(ccm) ametoa tamko kali kwa kusema chama hakitasita kumchukulia kiongozi yeyote hatua kama atagundulika anatoa rushwa ,anatoa michango mbalimbali kama harambe kweny maeneo mbalimbali bila idhini ya chama watachukuliwa hatua na pia ameonya makundi yote yanayokigawa chama waataitwa na kuhojiwa. Swali je hawa watoa michango hawajulikani mpaka wafanye uchunguzi, haya makundi hawayajui. Tujadili

He he Mabugando bwana kwa mbwembwe naye anataka asikike kama Kinana eti atakayegundulika,kwa mtindo huu hakuna atakayegundulika,pia awaseme wale wanaokaa na akina Masaburi na kusema watawafukuza kazi wenzao,pia hujinadi eti kisiri siri kwenye BBC kuwa watagombea uraisi hao ndio angeanza nao kwanza.
 
Back
Top Bottom