Maneno ya Wimbo wa Taifa la Tanzania ni Uvumbuzi wa Mtu wa Afrika Kusini

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,338
Ubeti wa kwanza wa wimbo wa taifa la tanzania "Mungu Ibariki Afrika" unatumika pia katika nchi ya Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.
Maneno katika wimbo huo yalitungwa na mtunzi Enoch Sentonga huyu ni Raia wa Afrika Kusini.

Wimbo huo aliutunga mwaka 1987 ukiwa na maneno "Nkosi sikelel i'Afrika wenye tafsiri yake "Mungu Ibariki Afrika katika lugha ya Kiswahili.

Wimbo huo ni wimbo maarufu Afrika ukitumiwa katika harakati za ukombozi kwa baadhi ya nchi za Afrika. Sontonga alizaliwa 1873 na alifari tarehe 18-04-1915 huko nchini Afrika kusini.

Huyo ndiyo mtunzi wa wimbo unao tumiwa katika ubeti wa kwanza wa wimbo wa taifa "Mungu Ibariki Afrika"
===

Hata kabla ya TANU (Tanganyika African National Union) kuanzishwa mwaka wa 1954, wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulikuwa unaimbwa Afrika Kusini.

Chama cha Afrika Kusini, African National Congress (ANC), kilianzishwa miaka mingi kabla ya chama chetu cha TANU. Na kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika Bloemfontein, South Africa, kuanzisha chama hicho mwaka wa 1912, waliimba Nkosi Sikelel' iAfrika. Nyerere alikuwa bado hajazaliwa. Na Hatukuwa na chama cha TANU miaka ile.

Chama cha kule Afrika Kusini kilichoanzishwa mwaka wa 1912 kiliitwa South African Native Congress chini ya uongozi wa John Dube, Mzulu, na Pixley ka I. Seme pia kutoka Natal kama Dube. Kikabadilishwa jina baadaye na kuitwa African National Congress (ANC).

Kuanzia mwaka wa 1925, wana ANC waliuchagua wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, kama wimbo wao wa taifa. Na bado unaimbwa leo.

Katika nyimbo za mataifa yetu ya Kiafrika, hakuna wimbo mwingine unaojulikana kama wimbo huo. Hata katika nchi za Afrika Magharibi, watu wengi wanajua Nkosi Sikelel' iAfrika ni wimbo gani na unamaanisha nini.

Watu wangapi nchi mbali mbali katika bara letu wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Ghana ingawa ilikuwa ni nchi ya kwanza kupata uhuru miongoni mwa nchi zetu kusini ya jangwa la Sahara? Wangapi wanajua jina la wimbo wa taifa wa nchi ya Nigeria, nchi kubwa inayojulikana sana? Lakini ukienda huko, utawakuta wanaosema wanajua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika.

Ndiyo maana hata Kenya wanaimba wimbo huo. Unaimbwa na unafahamika katika nchi nyingi katika bara letu hata kaskazini ya bara hili. Ukienda Egypt, Algeria na nchi zingine huko, utawakuta watu wengi wanaojua kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Wangapi katika nchi zingine za Kiafrika wanajua kuhusu wimbo wa taifa wa Uganda, au Malawi, au Burkina Faso? Lakini waulize kuhusu Nkosi Sikelel' iAfrika. Utawapata wengi waliousikia wimbo huo.

Enoch Sontonga alitoka Eastern Cape Province, jimbo la Wakosa (Xhosa), ambako pia ni nyumbani kwa Mandela. Alitunga wimbo huo katika lugha yake ya Kikosa na alitunga kama wimbo wa kanisa.

Alipotunga wimbo huo mwaka wa 1897, haukuimbwa hadharani mpaka mwaka wa 1899. Uliimbwa kanisani kwa mara ya kwanza mwaka huo. Halafu, baada ya miaka kumi na tatu, uliimbwa kwenye mkutano wa kwanza wa South African Native Congress mwaka wa 1912 uliofanyika Bloemfontein kuanzisha chama hicho kugombea haki za Wafrika.

Hata Watanganyika wengi waliokwenda kufanya kazi migodini Afrika Kusini miaka ya 1940s na 1950s waliujua wimbo huo. Walikuwa wanaimba Nkosi Sikelel' iAfrika pamoja na watu wa Afrika Kusini walipokuwa huko na waliporudi Tanganyika. Ninawafahamu wengi wao.

Na nina hakika kuna Watanganyika wengi, mara tu tulipopata uhuru, waliokuwa au walioziona music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika. Na ikiwa kuna ambao bado wanazo music sheets hizo, wanaweza kukuonyesha jina la Enoch Sontonga kama ndiyo mtungaji wa wimbo huo.

Nakumbuka sana nililiona jina lake kwenye music sheet hiyo kwa sababu hata mimi nilikuwa nayo. Na si mimi tu niliyekuwa nayo au niliyeiona music sheet hiyo ya wimbo huo. Ilikuwa katika lugha mbili, Kiswahili na Kiingereza, na kichwa chake kilikuwa ni Mungu Ibariki Afrika, God Bless Africa, yaani Nkosi Sikelel' iAfrika.

Melody ya Nkosi Sikelel' iAfrika ilitungwa na Enoch Sontonga. Ukiisikiliza melody hiyo, hakuna tofauti hata kidogo na melody ya wimbo wetu wa taifa, Mungi Ibariki Afrika, au melody ya wimbo wa taifa kule Zambia. Sikiliza wimbo huo Youtube ambao mmoja wa waimbaji wake katika video ni Miriam Makeba. Pia lyrics za Nkosi Sikelel' iAfrika ziliandikwa na Enoch Sontonga, ingawa wimbo wetu una lyrics zake sehemu mbali mbali. Lakini chanzo chake ni wimbo uliotungwa na Enoch Sontonga: Nkosi Sikelel' iAfrika.

Kama nilivyosema kabla ya hapa, wimbo huo siyo wa watu wa Afrika Kusini tu. Enoch Sontonga aliandika na alitunga wimbo huo kama ni wimbo wa bara lote. Ndiyo maana alisema Nkosi Sikelel' iAfrika, God Bless Africa, na siyo God Bless South Africa.

Nyimbo zake nyingi zilikuwa ni nyimbo za huzuni kuhusu maisha magumu ya Wafrika chini ya utawala wa Wazungu waliokuwa wanawakandamiza Wafrika katika bara lote. Wimbo wake, Nkosi Sikelel' iAfrika, ulitokana na maumivu hayo ya Wafrika ingawa pia ulikuwa ni wimbo wa kuwapa tumaini kwamba hawako peke yao. Mungu yuko nao, au yuko nasi, ingawa tunaumia na tunateswa na wanao tutawala kutoka nchi za Ulaya.

Wimbo huo, Nkosi Sikelel' iAfrika, uliwekwa kwenye sahani ya santuri kwa mara ya kwanza, London, mwaka wa 1923. Uliimbwa na Solomon Plaatje, mwimbaji maarafu wa Afrika Kusini ambaye pia alikuwa ni mmoja wa Wafrika walioanzisha chama cha South African Native Congress, Bloemfontein, South Africa, mwaka wa 1912.

Ni wimbo wetu pia kwa sababu Afrika ni moja. Ndiyo maana Enoch Sontonga alitunga wimbo unaosema Nkosi Sikelel' iAfrika - God Bless Africa.

Kwahiyo hatukuiba, na hatukuazima, wimbo huo. Ni wetu kama wao kule Afrika Kusini na nchi zingine. Na Enoch Sontonga alipewa full credit kwenye music sheets za wimbo huo nchini Tanganyika, na baadayeTanzania, kama ndiyo mtungaji wa God Bless Africa.

Miaka yote hii, tangu nilipokuwa kijana mdogo miaka ya 1960s, nimejua kwamba wimbo huo ulitungwa na Enoch Sontonga kutoka Afrika Kusini. Kuna Watanzania wengine wanaojua ukweli huo. Si mimi tu.

Utumizi wetu wa wimbo huo, ambao pia ni wimbo wa taifa, Zambia, unaonyesha pia umoja na undugu wetu kama Wafrika. Ndiyo maana kulikuwa hata vyama vilivyopigania uhuru ambavyo majina yao yalifanana au yalikuwa karibu sana. Kwa mfano, African National Congress (ANC) iliyoundwa Tanganyika na kuongozwa na Zuberi Mtemvu na katibu wake mkuu John Chipaka ilikuwa na jina sawa na la chama cha Africa Kusini cha akina Mandela na wenzake. Pia chama cha kwanza kupigania uhuru Northern Rhodesia kilicho ongozwa na Harry Nkumbula kilikuwa kinaitwa African National Congress, na kiliendelea kuitwa hivyo hata baada ya wanachama wengine waliondoka na kuunda chama kingine, United National Independence Party (UNIP), chini ya uongozi wa Kenneth Kaunda.

Kenya kulikuwa na Kenya African Union (KAU) kabla ya Tanganyika African National Union. Baadaye KAU ikabadili jina kidogo na kuitwa KANU. Na ndugu zetu Zimbabwe waliunda chama kinachoitwa ZANU baada ya baadhi yao, pamoja na Robert Mugabe, kuondoka na kuachana na ZAPU.

Majina hayo, katika nchi zetu mbali mbali, yanafanana kwa sababu tunajiona kama ni ndugu, na ni kweli sisi sote ni ndugu. Pia inaonyesha ushirikiano wetu. Hata Uganda, jeshi lao ni Uganda People's Defence Forces (UPDF), jina linalotokana na jina la jeshi letu: Tanzania People's Defence Forces (TPDF).

Ni sawa na wimbo wa Nkosi Sikelel' iAfrika kuwa wimbo wa taifa Tanzania, Zambia, na South Africa.

Africa ni moja. Sisi sote ni ndugu bila kujali ukabila, rangi, dini, au asili.

Mungi Ibariki Afrika. Nkosi Sikelel' iAfrika.
 
Jukwaa la historia ipo thread full.Shida kasomi anaharaka ya kufika.
Ngoja nimpe like ,sie yatima tunajaliana🤣🤣
Hahaha 🤣🤣🤣
Kweli mkuu acha tujaliane🙏🙏🙏
 
Asante kwa andiko lako zuri...subiri tu uzi wako uunganishwe na mwingine ndugu Emma maana kuna nyuzi zaidi ya saba humu zinaongelea hii kitu kwa mara ya kwanza kuona uzi km huu ilikuwa 2015
 
Asante kwa andiko lako zuri...subiri tu uzi wako uunganishwe na mwingine ndugu Emma maana kuna nyuzi zaidi ya saba humu zinaongelea hii kitu kwa mara ya kwanza kuona uzi kama huu ilikuwa 2015
🙏🙏🙏 Ngoja nisubiri wafanye hivyo kama uzi upo
 
Mungu ibariki Afrika" was translated and became the state anthem of Tanganyika. It was essentially assigned to Enoch Sontonga, who died in 1905. Mungu ibariki Afrika used the tune to "Nkosi Sikelel' iAfrika" with a Swahili translation of the words. It is not known who composed the lyrics but it is known that it was Samuel Mqhayi and Enoch Sontonga who created the early versions used by the African National Congress.[2] Although the tune has been assigned to Sontonga it is thought by some that the tune was originally written by Joseph Parry.[3][1]

Swahili translation Edit
It was first performed in Swahili at a ceremony on 8 December 1961 following the independence of Tanganyika from the British Empire. "Mungu ibariki Afrika" was composed to replace the British national anthem, "God Save the Queen" as the national anthem of Tanganyika.[4] This made Tanganyika the first African nation to adopt the tune of "Nkosi Sikelel' iAfrika" as its national anthem.[5] In 1964, Tanganyika formed a union with Zanzibar, which created the United Republic of Tanganyika and Zanzibar (later renamed to Tanzania). The newly united country adopted "Mungu ibariki Afrika" as its national anthem instead of Zanzibar's anthem.[5] Tanzania's use of "Mungu ibariki Afrika" led the way for other African countries such as Zimbabwe, Ciskei and Transkei adopted "Nkosi Sikelel' Afrika", in parts, as their national anthems.

South Africa where the song comes from use only some of the words, Zambia uses only the tune and other countries have now abandoned its use.[2] "Mungu ibariki Afrika" was inspired by the African National Congress's use of "Nkosi Sikelel' iAfrika" ("God Bless Africa") as its party song after its use at Ohlange High School. The ANC party anthem led to "Mungu ibariki Afrika" being selected as the national anthem of Tanzania.[6][7][8] "Mungu ibariki Afrika" is also used as a hymn requesting Tanzania remain united and independent.[9]

Tanganyika and later Tanzania had concerns about religious unrest between Christians and Muslims after independence. This was because of Christian references in government proceedings and official oaths. The wording of "Mungu ibariki Afrika" was intended to help offset this by being inclusive of the different religious views.[10]

"Mungu ibariki Afrika" is sung daily at Tanzanian schools. A circular issued in 1998 by the nation's Commissioner of Education recommended the singing of the national anthem as a way to promote patriotism in Tanzania's youth.[11]

In 2007, a legal issue arose over the anthem after students who were members of the Jehovah's Witnesses refused to sing the song at their primary and secondary schools in Mbozi District, Mbeya Region. Five students were expelled from school and 122 others received other forms of discipline for their refusal.[11] They objected to singing the anthem because they believed it suggested obeisance to the flag of Tanzania before God.[12] On 2 December 2010, the High Court of Tanzania ruled that the schools' disciplinary actions were appropriate.[11][12] The Court of Appeal of Tanzania overturned that ruling on 12 July 2013, indicating that the disciplinary action taken by the school was unlawful and stating that there was no obligation to sing the national anthem in Tanzanian law.[12]
 
Yaani wimbo unahamasisha utumwa alafu ulitumika kwenye harakati za kujikomboa
 
Back
Top Bottom