UZUSHI Manchester United imewahi kufungwa 39-0 na Arsenal mwaka 1920

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Arsenal inashikilia rekodi ya kuichapa Man U kichapo kikubwa zaidi kwenye ligi ya Uingereza cha Magoli 39-0 mwaka 1920.

Habari hii inasambaa sana mtandaoni, JamiiCheck tunaomba mtusaidie kuifuatilia.

Man u vs Ars (2).jpg

 
Tunachokijua
Ligi Kuu ya Uingereza hujumuisha vilabu 20, na kwa kawaida misimu huanza Agosti hadi Mei, huku kila timu ikicheza mechi 38 dhidi ya timu nyingine zote, nyumbani na ugenini. Michezo mingi huchezwa Jumamosi na Jumapili alasiri, na ratiba ya jioni kwa siku za wiki.

Historia ya ligi kuu ya Uingereza (EPL)
Mapema miaka ya 1990, vilabu vya Ligi ya Daraja la Kwanza viliamini kwamba marekebisho makubwa ya soka yanahitajika ili wao na sekta nzima ya mchezo wa mpira wa miguu kwa ujumla waweze kuku ana kustawi.

Hivyo, Julai 17, 1991, walitia saini Mkataba wa Wanachama Waanzilishi, wakiweka kanuni za msingi za kuanzisha Ligi Kuu ambayo ingekuwa na uhuru wa kibiashara na Kampeni ya kwanza ya Ligi Kuu ilianza Jumamosi Agosti 15, 1992, ikiwa na vilabu 22.

Arsenal na Manchester United ni miongoni mwa timu waanzilishi wa michuano hii.

Wakati Ligi Kuu ilipoanzishwa, kila mara kulikuwa na nia ya kupunguza idadi ya vilabu hadi 20 ili kukuza maendeleo na ubora katika ngazi ya klabu na kimataifa. Hili lilifikiwa mwishoni mwa msimu wa 1994/95 wakati vilabu vinne vilishushwa daraja na mbili pekee kupanda.

Kichapo cha Magoli 39-0
Septemba 9, 2023, Mtumiaji wa Mtandao wa X anayefahamika kwa jina la Tyga aliweka chapisho linalodokeza kuwahi kuwepo kwa mechi kati ya Arsenal na Man U mwaka 1920 ambapo Arsenal alipata ushindi mnono wa kimbunga wa magoli 39-0.

"On this day 1920, Arsenal beat Manchester United 39-0. Pass it on", aliandika Tyga.

Aidha, Novemba 19, 2023, Mtumiaji mwingine wa mtandao wa Facebook kwa majina ya David Raya aliandika ujumbe unaofanana na huo. Pamoja na kutaja kuwa Ufaransa ilikuwa imeshinda 14-0 dhidi ya Gibraltar, bado ushindi huo ulikuw mdogo sana kulinganisha na ule wa Arsenal dhidi ya Manchester United wa magoli 39-0.

"France are on cloud nine after beating minnows Gibraltar 14-0. But nothing will ever come close to Arsenal absolutely slaughtering Manchester United 39-0 back in 1920.

This time Uganda
🇺🇬
was still under colonial rule by Britain.
Me: is this real ?
Just asking"
ulisomeka ujumbe huo.

Hadi kufikia Novemba 21, 2023, ujumbe huo ulikuwa umependwa (like) na zaidi ya watu 3000, watu wengine 743 walikuwa wamshirikisha wengine (Share) na wengine 555 wakichangia maoni yao (Comment)

Ukweli wa madai haya
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa ujumbe huu hauna ukweli, ni uzushi.

Katika mchezo ulioikutanisha Arsenal dhidi ya Man U Agosti 30, 1920 kwenye ligi daraja la kwanza, Arsenal ilipata ushindi wa goli 2-0. Mchezo huu ulipigwa kwenye uwanja wa wao wa Highbury.

Aidha, tovuti nyingine inadai kwenye mchezo wa Februari 20, 1920, Man ilipata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Arsenal.

Utafutaji mwingine wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck haujaleta majibu yoyote yanayodokeza au kutoa taarifa ya ushindi wa goli 39-0 wa Arsenal dhidi ya Man U.

Utata wa majina ya wafungaji
Ufutiliaji mwingine wa JamiiChek unebaini kuwa majina ya wafungaji walioorodheshwa kwenye ujumbe huo wamezaliwa miaka ya hivi karibuni na hawajawahi kuichezea Arsenal.

Orodha ya wachezaji wa mwaka 1920 inathibitisha haya.

Mathalani, mfungaji anayetajwa kuhusika kwenye kupachika nyavuni magoli 4, Luca Langoni amezaliwa Februari 9, 2002 nchini Argentina. Bila shaka asingeweza kucheza mwaka 1920 kabla hata hajazaliwa.

Pia, utafutaji wa JamiiCheck umebiaini kuwa wachezaji wote waliotajwa ni wazaliwa wa Argentina na bado wanacheza mpira wa ushindani hadi sasa.

Hivyo, kutokana na kukosekana kwa ushahidi usiotia shaka, pamoja na uwepo wa utata kwenye majina ya wafungaji waliohusika kwenye ushindi huo, JamiiCheck inatambua suala hili kama uzushi.

Nani mbabe zaidi?
Arsenal na Manchester United zilicheza kwa mara ya kwanza mechi ya kimashindano mnamo Oktoba 13, 1894 na hadi kufikia Septemba 3, 2023, vilabu hivyo viwili vimekutana mara 239 kwa jumla.

Manchester United wameshinda 101 dhidi ya 88 za Arsenal, na mechi 50 zimeisha kwa sare.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom