DOKEZO Mamlaka ya udhibiti wa ubora wa vyakula inatumia utaratibu upi? Kuna bidhaa nyingi zilizopita muda madukani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Wakuu heshima mbele, niende moja kwa moja kwenye mada.

Pengine inaweza kuonekana kama jambo la ajabu kwangu mimi naweza kuchukua hatua je wangapi wasiojua hili?

Ipo hivi majuzi nilitinga katika supermarket moja hivi , nina utamaduni wa kila bidhaa nitakayonunua lazima nitizame expiry date.

Bidhaa ya kwanza kushika imexpire March 2023

Bidhaa ya pili imexpire July 2023 .

Kiukweli niliishia palepale nikawafuata wahusika nikawaeleza na nikawauliza je ni bahati mbaya au hawakua wakifahamu ,je mtu mwingine kama alichukua au angechukua bidhaa hizo bila mimi kuona ingekuwaje kama zingeleta madhara baada ya matumizi?

Niliwapa somo fupi juu ya ukaguzi bora wa bidhaa kisha nikanunua bidhaa ambazo bado ni hai nikaondoka.

Nitoe rai kwa wafanyabiashara japo pesa ni muhimu tutangulizw utu kwanza.

Mamlaka husika mtoe mafunzo ya mara kwa mara kaguzi za mara kwa mara msisubiri mpaka tatizo litokee ndio tuone barua mitandaoni na kauli za tunaendelea na uchunguzi.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom