Shibalanga
Senior Member
- Mar 1, 2011
- 178
- 93
Ndugu zangu, naomba tusaidiane kwa pamoja kutambua mambo ambayo sisi kama watanzania bila kujali itikadi za siasa, dini, Rangi, kabila,kanda na jinsia; mwisho wa siku yanaturudisha pamoja kama wananchi wazalendo wa nchi hii.
Binafsi, nimekuwa nikijiuliza sana swali hili nakosa jibu, na hii ni kutokana kushuhudia minyukano ya kisiasa, kidini, kiuchumi na kitabaka ambayo hali hii imepelekea sasa kila kukicha ni malalamiko,maandamano,tuhuma, mauaji, vitisho, ubabe; Kiasi kwamba inataka kuonekana kana kwamba Tanzania si pahala pazuri pa kuishi.
Ndugu zangu, najua humu kuna watu makini sana waliobobea katika nyanja mbalimbali na kutokana na umuhimu huo mlio nao hebu kwa pamoja tutambue ni mambo gani ambayo mwisho wa siku sitakuwa na haja ya kutambua huyu ni wa CUF, CHADEMA,CCM, MWISLAM, MKRISTO, MPAGANI, KIJANA, MZEE, MTOTO, PROFESA,MKULIMA N.K lakini tunakuwa kitu kimoja?
Nisaidieni tafadhali.