Mambo ya msingi yanapoondolewa katika rasimu ya katiba mpya

Mkulia

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
375
95
Binafsi ninasikitishwa sana na jinsi mambo yanavyoendelea katika Bunge Maalumu la Katibu (BMK) huko Dodoma. Kwa wale mnaofuatilia mwenendo wa Bunge hilo mtakubaliana nami kuwa haitapakikana Katiba iliyotokana na mawazo ya wananchi. Huwa ninaumia sana ninaposikia kuwa mawazo ya wananchi yanasiginwa na badala yake wajumbe wanaweka mawazo yao.

Kwa mfano Rasimu ya Katiba mpya imependekeza kuwa mawaziri wote wasitokane na wabunge kwa lengo la kuwaacha wabunge kuwajibika vizuri zaidi kwa wapiga kura wao. Lakini kutokana na ubinafsi wa wajumbe waliopo Bungeni wamekataa wazo hilo na kutaka mawaziri waendelee kuteuliwa miongoni mwa wabunge. Pia Rasimu ilipendekeza kuwa katiba iwape mamlaka wananchi ya kumuondoa mbunge wao kwa kukosa kuwajibika au kushindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo. Nalo hili limekataliwa na wabunge wa BMK waliopo Dodoma kwa sababu ambazo hazina mashiko kabisa.

Si hivyo tu Rasimu ya katiba pia ilipendekeza kuwe na ukomo wa mtu kuwa mbunge tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kuna watu wamo bungeni kama vile katika majimbo hayo hakuna watu wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi zaidi yao. Pendekezo hili pia limepingwa vikali na wajumbe wa BMK waliopo Dodoma. Sasa kama mawazo ya msingi ya wananchi yanaondolewa katika Rasimu ya Katiba mpya kulikuwa na sababu gani ya kupoteza fedha za wananchi kukusanya maoni? Hayo maoni yalikuwa ya nini na kwa faida ya nani?
 
Kule Dodoma hawajadili rasimu hiyo, bali wanatunga Katiba mpya. Kulingana na wao ile rasimu ina makosa kibao na haiwakilishi mawazo ya Watanzania. Mawazo ya Watanzania ni yale ya CCM na ndiyo sahihi. Kwa msingi huo Katiba mpya itapatikana sio kutoka katika rasimu unayoisema. Theluthi mbili lazima zitapatikana hata kama kuna udhia. Si unapenyeza rupia tu pamoja na kuchakachua? Nani atazuia hili? Ukawa hawapo huko. We uaona tu. Subiri.
 
Ni kosa langu mimi, wewe na yule. Tukiamua tunaweza weka mambo sawa, CCM wanatumia udhaifu wetu kufanya wapendavyo.
Kweli Tanzania ni nchi ya amani au ni nchi ya wasiojitamani?
 
Back
Top Bottom