SoC04 Mambo ya kuboresha katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na halmashauri ili kufikia mapinduzi ya kiuchumi kwaka 10 ijayo nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

tinyyn

New Member
Apr 29, 2024
1
0
Nchini Tanzania mikopo hii hutolewa na halmashauri kwa makundi maalum yanayostahili kupata mikopo hiyo makundi hivyo ni vijana, wanawake na wenye ulemavu ambapo vijana ni asilimia 4%, wanawake ni asilimia 4% na walemavu ni asilimia 2%. Mikopo hii ina umuhimu mkubwa katika jamii hasa katika kuinua uchumi kwa makundi stahiki ya mikopo hii.

Hivi karibuni serikali imeweka misingi mizuri itakayowezesha utolewaji wa mikopo hiyo na urejeshwaji wa marejesho ya mikopo hiyo kwa wakati kupitia benki. Ili ukongeza ufanisi zaidi katika kufanikisha utolewaji wa mikopo hii kwa walengwa na urejeshwaji wa marejesho kwa wakati serikali inapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Makundi/ vikundi stahiki visikopeshwe fedha taslimu bali wakopeshwe vifaa kulingana na mradi walioandika katika andiko lao.
Jambo hili litasaidia kikundi husika kinachoomba mkopo kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mradi wao na kupelekea urejeshwaji wa marejesho ya mikopo hii kwa wakati. Kwa mfano kikundi ambacho kinaomba mkopo kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufyatuaji matofali, kikundi hiki kikopeshwe vifaa stahiki vya mradi wa ufyatuaji wa matofali kama vile mashine maalum za kufyatulia matofali, cement pamoja na kuonyeshwa eneo ambalo wataanzisha mradi huo.

2. Vikundi vinavyokopeshwa lazima viweke dhamana ya mali isiyohamishika.
Jambo hili litasaidia kuvibana vikundi vilivyokopeshwa kurejesha marejesho ya mikopo yao kwa wakati, vilevile kama wasiporejesha kwa wakati halmashauri husika iwe na haki ya kuuza mali hiyo ili kufidia mkopo ambao haujarejeshwa kwa wakati uliowekwa.

3. Kila mwanakikundi lazima atambulike.
Jambo hili litasaidia Kuwatambua wanakikundi husika waliokopeshwa mikopo hiyo, na pale inapotokea changamoto yoyote hii itasaidia kuwapata kwa urahisi wahusika wote na kufuatilia kwa ukaribu katika urejeshwaji wa marejesho ya mikopo waliyokopeshwa.

4. Kuwepo na vigezo maalum vya kupima uhitaji kwa makundi husika.
Jambo hili litasaidia mikopo hii walengwa wote kwa usawa ambao ni vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Hivyo halmashauri zetu ziweke utaratibu maalum wa kutambua makundi yenye uhitaji kwa jamii husika, hivyo itasaidia walengwa wote wenye uhitaji kufikiwa na mikopo hii kwa usawa.

5. Kuwepo na ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa vikundi vilivyokopeshwa.
Jambo hili litasaidia walengwa waliokoeshwa kufuatiliwa kwa ukaribu ili kujua maendeleo ya miradi iliyoanzishwa kupitia mikopo iliyotolewa kwao na kujua ni changamoto gani zinawakabili kwenye miradi yao na kuzitatua changamoto hizo ili kuwazezesha kufikia malengo yao. Hivyo maafisa maendeleo katika eneo husika wanatakiwa wafatilie kwa ukaribu vikundi hivi.

Hitimisho
Endapo mambo hayo yatafanyiwa kazi kwa vitendo basi mikopo hiii itazidi kuwa na tija na umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi kwa makundi hayo, pamoja na hayo taifa zima la Tanzania litaweza kuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi kwa miaka 10 ijayo.
 
Back
Top Bottom