fangfangjt
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 571
- 139
Tatizo nafikiri hatufati kanuni za uadishi wa paper, ni lazima uli reference mahala fulani ili ku -justfy unachoongelea. Nani alikuambieni Sita, mwakyembe wanapigania masilahi yako. Fuatilia kwa makini mwanzoni mwa sakata la Richmord sita akiwa spika wakati huo wakiwa kundi moja na akina RA. Hoja alijaribu sana kuizima na kusema ulongo ulongo. Sita ameanza kupigana baada ya ku defect kutokana na kuzidiwa ujanja.
Tatizo wewe unaongea kama watoto wa Gadafi kumhasi baba yao na eti nao wamuite dictator baba yao, hasa unapowataja akina Mwinyi. Na vijana wachache waliopo wala sio wakutolea mfano kwa sababu wazee wamewa-abducted.
Tanzania hakuna mzee anayepigania haki ya Tanzania ila ni majambazi wawili wanapigania walichokipora, sasa mmoja anaonekana kulemewa. Na wengine wako pembeni wakitamani kuingia mahali hapo nao waibe.
Kwani dk slaa anapotaka urais ni kwa ajili yako ? Au mtu anapotaka udiwani, ubunge , ukurugenzi wa shirika au cheo chengine chochote ni kwa ajili ya nani? Ndio maana kuna interview, mtu anapewa fursa ya kujinadi ili muone kama mkimpa huo wadhifa wakati yeye anapofaidi matunda ya wadhifa huo atawasaidia vipi nyie mnaomuweka hapo? Ambaye atajinadi vizuri basi mnampa wadhifa. Sasa nimbie Sitta na Mwakyembe walipo sema Dowans wasilpwe walikua wanafaidi nini? Wewe kama mwananchi unapoteza au kufaidika vipi na huo msimamo wake?