Mambo 21 ambayo bara la Afrika inajivunia

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
1. Nchi ya Gambia ina chuo kikuu kimoja tu (The University of Gambia).

2. Equatorial Guinea ni nchi pekee Afrika ambayo lugha yake ya Taifa ni Kispaniola (Spanish). Hakuna nchi nyingine Afrika inayozungumza Kispaniola.

3. Afrika kusini ndiyo nchi inayotembelewa na wageni wengi zaidi kuliko nchi zote za Afrika.

4. Nigeria ndio nchi yenye matajiri wengi weusi kuliko nchi nyingine za Afrika (richest Black people).

5. Samuel Eto’o ndiye mchezaji anayelipwa ghali zaidi kuliko wachezaji wengine kutoka Afrika. Analipwa Euro 350,000 kwa wiki (sawa na shilingi milioni 980,000/=). Kwa lugha rahisi ni kwamba mshahara wa Et'oo wa wiki 7 unalingana na pesa zote alizoiba Rugemalira kupitia Escrow na kugawia kina Tibaijuka na Ngeleja.

6. Raia kutoka Nigeria anaitwa Nigerian, Raia wa Niger anaitwa Nigerien na raia wa Burkina Faso anaitwa Burkinabe.

7. Nigeria imeshinda vikombe vingi vya soka kuliko Uingereza (England).

8. Ethiopia na Liberia ni nchi pekee Afrika ambazo hazijawahi kutawaliwa. Italia ilipojaribu kuitawala Ethiopia iliishia kupigwa vibaya na ikassurender.

9. Kabila la Limba huko Zambia, mama wa mvulana ndiye anayemtafutia mwanae binti wa kuoa. Mama ndiye anayemuapproach binti, na kulipa mahari kabla hata binti hajamuona kijana mwenyewe. Kinachotakiwa ni binti kumkubali mama tu.. Ukimkubali mama means umemkubali na mwanae. So mwanae utakutana nae kwenye harusi, mambo mengine kabla ya harusi anafanya mama yake.

10. Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ndiye Rais msomi zaidi duniani. Ana degree 7 alizozisomea ktk vyuo vikuu mbalimbali, mbili kati ya hizo ni Masters.

11. Zinedine Zidane aliwahi kurudi nchi yake ya asili Algeria ili aichezee kwenye mashindano ya kimataifa. Alipofika waziri wa michezo wa Algeria, Abdelmalek Sellal akamwambia "tuna wachezaji wengi wazuri kuliko wewe na hawajapata nafasi kwenye kikosi. Labda tungeruhusiwa kucheza zaidi ya 11 uwanjani ungeweza kubatika kupata namba".

12. Robert Mugabe ndiye Rais mzee zaidi duniani. Anashikilia rekodi kwa kuwa na umri wa miaka 91 akifuatiwa na Shimon Peres, Rais wa Israeli mwenye miaka 90.

13. Shelisheli (Seychellois) ndio nchi ya kwanza duniani ambayo raia wake wameelimika kuliko nchi nyingine. Inakadiriwa kuwa asilimia 91.9% ya watu wake wana elimu ya sekondari na kuendelea. (Tanzania wenye elimu ya sekondari na kuendelea ni asilimia 13.5 kwa mujibu wa HakiElimu.)

14. Mauritius ndiyo nchi pekee Afrika inayoingiza fedha nyingi kupitia utalii wa fukwe (Beach Tourism). Mwaka 2013 iliingiza takribali shilingi trilioni 4.5 kupitia utalii wa fukwe. Tanzania tuliingiza shilingi bilioni 1.7 kupitia Utalii wa fukwe mwaka huohuo.

15. Rwanda ndiyo nchi pekee yenye usawa wa kijinsia kuliko nchi zote duniani (Bunge la Rwanda ni 50% wanaume na 50% wanawake).

16. Ethiopia ndio nchi pekee Afrika yenye viwanja vingi vya ndege vyenye hadhi ya kimataifa (International Airports). Ina viwanja vya ndege 23 vyenye hadhi ya kimataifa. (Tanzania tuna viwanja vya ndege vitatu vyenye hadhi ya kimataifa (JNIA-Dar, KIA-Moshi, na Songwe-Mbeya).

17. Uchumi wa Ethiopia unakua kwa kasi kuliko Uchumi wa China. Uchumi wa Ethiopia (GDP) unakua kwa wastani wa 18.7% kwa mwaka, China GDP inakua kwa wastani wa 11.4% kwa mwaka (according to the World bank fact sheet, 2014).

18. Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ndiye Rais Maskini kuliko wote Afrika. Analipwa mshahara wa Dola 500 za kimarekani ($ 500) sawa na Shilingi 945,000/=. Hiki ni kiwango kidogo cha mshahara kuliko daktari wa mfunzo nchini Tanzania (Intern Doctor).

19. Angola ina watu wengi wanaoongea Kireno kuliko Ureno kwenyewe. Angola ina watu milioni 22 na wote wanaongea Kireno, lakini Ureno ambao ndio wenye lugha wana watu milioni 10.7 tu.
20. Somalia ilipata mashine yake ya kwanza ya ATM tarehe 7, October, 2014. Kabla ya hapo hakukuwa na ATM yoyote nchini Somalia.

21. Zanzibar ndio nchi ya kwanza kuwa na television ya rangi Africa.

Unaweza kuongezea sifa nyingine ambayo bara la Afrika inajivunia.


Mpalestina Mchizi
A Man From Mars
 
Fanya update huu uzi wako wa miaka mitano iliyopita. Halafu huwezi jivunia kuwa na chuo kikuu kimoja ktk nchi.
Ni kweli coz inaonekana kuwa huo uzi ni wa miaka miwili iliyopita
 
Duuh!! namba 11 imenigusa, sio lazima acheze hata kama katoka nchi za kizungu, alitarajia kuwa favoured kisa katoka ulaya
 
Ruge alikwapua bil 75, Eto'o analipwa mil98, kweli bil na mil zinalingana?
Sahihisha namba 6
 
Hapo 21 nina mashaka, INA maana unataka kutuaminisha Zanzibar waliizidi south Africa +misri kuwa na television ya rang?
 
5. Samuel Eto’o ndiye mchezaji anayelipwa ghali zaidi kuliko wachezaji wengine kutoka Afrika. Analipwa Euro 350,000 kwa wiki (sawa na shilingi milioni 980,000/=). Kwa lugha rahisi ni kwamba mshahara wa Et'oo wa wiki 7 unalingana na pesa zote alizoiba Rugemalira kupitia Escrow na kugawia kina Tibaijuka na Ngeleja.
Siyo kweli...
Ruge alipewa mgao wa bils 75 za kitz ambazo ni sawa na kuandika hivi 75,000,000,000.
Samuel Etoo hawezi kuzipata kwa week saba maana ni dolar milion 34 Au approxinately euro milion 27
 
Back
Top Bottom