Mambo 11 mazito yanayomponza RC Hapi mkoa wa Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
Hivi karibuni kumekua na mijadala mbalimbali hasa mitandaoni kuhusu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi na namna anavyotekeleza majukumu yake ya kazi.
Mijadala hii inaongozwa na makundi ya wanaharakati mbalimbali wanaokosoa na kupinga ufanyaji kazi wa Mkuu huyo wa Mkoa.
RC Hapi kitaaluma ni Mwanasheria aliyehitimu Chuo cha Udsm. Kiutendaji amewahi kuwa afisa wa chama Makao Makuu CCM Lumumba na baadaye kuteuliwa kuwa DC Kinondoni kabla ya kuwa RC Iringa.Ni kijana aliyelelewa na kukulia ndani ya CCM na hivyo huwezi kumtenganisha na chama hicho.

Ukitaka kujadili utendaji wa RC Hapi Iringa, yako makundi makubwa mawil ya kutazama katika kupima kazi yake.

Kundi la kwanza ni la wananchi wa kawaida wa Iringa na hasa wanyonge ambao Hapi ameshuka kuwafikia na kutatua kero zao mbalimbali na kusimamia haki zao ambazo nyingine wamesota kwa miaka mingi kuzitafuta. Kundi hili ni kubwa sana Iringa, huku wengi wao wakiwa ni wanyonge wanaomuombea Hapi mema kila uchao.

Kundi la pili ni la wanasiasa na wanaharakati wa kisiasa ambao matendo ya Hapi yanahatatisha uhai wao. Hawa wanasikika sana katika mitandao ya kijamii kama magroup ya whatsap, Twitter, Instagram, vijiwe vya kisiasa vya maeneo ya Mjini na hata mikutano ya kisiasa kama ile ya Msigwa Mwembetogwa. Hawa kazi yao ni kusubiri maeneo ambayo wataona makosa ya Hapi au kauli zenye utata ili wazitumie kama sehemu ya kuonyesha kuwa RC Hapi ni mtu asiyefaa kuwa kiongozi kabisa na pengine hatakiwi kuwepo mkoani Iringa. Malengo ya kundi hili ni ya harakati na siasa zaidi. Nitaeleza baadae.

*RC HAPI ANAJIPONZA MWENYEWE!!!*

Unaweza usinielewe, lakini adui wa Hapi ni yeye mwenyewe Yako mambo mengi ambayo RC Hapi tangu aingie Iringa amekua si tu adui wa wanasiasa wa Iringa na hasa upinzani, bali amekua adui wa wanaharakati wa upinzani nchi nzima. Yako mambo nitayataja ambayo ndiyo yanayomfanya Hapi kuwa adui namba moja wa CHADEMA Iringa na pengine kuingia katika orodha ya maadui wa kitaifa wa Chadema na upinzani kwa ujumla na hivyo kupigwa vita na kushambuliwa.

*1. Rekodi ya ukada wa CCM na utendaji ya Hapi. *

Ally Hapi ni kijana aliyekulia na kulelewa ndani ya CCM akiwa hajawahi kufanya kazi mahali popote nje ya CCM. Ukada wake ambao hauna shaka umemfanya kusimamia kidete maslahi ya nchi, serikali na Chama tawala popote pale alipo. Akiwa DC Kinondoni Hapi aliweza kuongoza ushindi katika chaguzi ndogo ngumu za marudio kata ya Mbweni (jimbo la Kawe) na jimbo la Kinondoni ambako ndiko yaliko makao makuu ya Chadema. Uchaguzi huu ulikua ni kufa na kupona kwa upinzani kutetea ngome yao isipotee. Viongozi wote waandamizi wa Chadema waliungana kuishambulia Kinondoni, lakini hawakufua dafu.
CHADEMA wanaamini kuwa Hapi aliwashughulikia na kufuta upinzani Kinondoni, hivyo rekodi hii kwao ni mwiba mkali. Matukio ya Kuwasweka rumande viongozi waandamizi wa upinzani kama Mwenyekiti wa Bawacha Halima James Mdee kulimuweka Hapi katika orodha ya wateule wa Rais wanaochukiwa na upinzani.

*2. Uteuzi wa Hapi kuwa RC Iringa.*

Hakuna shaka kuwa Iringa imekua ngome ya Chadema kwa muda mrefu. Mbunge wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa ndiye Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za juu kusini na mtu muhimu kwa uhai wa Chama hicho. Kuteuliwa kwa mtu mwenye rekodi ya Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kulitafsiriwa n upinzani kuwa Rais Dkt John Magufuli amemleta Hapi kwa kazi maalum ya kuua upinzani Iringa na kurejesha nguvu ya kihistoria ya CCM. Hivyo tangu uteuzi wake siku ya kwanza, Hapi alitangazwa kuwa adui namba moja wa Chadema Iringa. Hili limetamkwa hadharani na viongozi wote wa Chadema wakiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa.

*3. Ziara ya Iringa Mpya.*

Katika ziara hii iliyobezwa sana na Mhe Msigwa, Hapi alitembea kata kwa kata na alionekana akitatua kero na shida za wananchi wa Iringa hadi usiku vijijini. Hii ni mara ya kwanza kushuhudiwa Iringa. Hali hii iliwanyima usingizi maadui zake wa kisiasa ambao waliona kuwa wafuasi wao wanamegwa taratibu na kuwa wafuasi wa serikali ya CCM. Ziara hii pia ilifunua madudu mengi ya upinzani hasa manispaa ya Iringa na kuwafanya wananchi kuuona upande wa pili upinzani, Msigwa na manispaa ambayo inaongozwa Na Chadema. Moja katika halmashauri iliyobainika kuwa na kero na uozo mwingi ni manispaa ya Iringa.

*4. Kukubalika na wananchi wa Iringa.*

Kutokana na hulka yake ya kusimama upande wa wananchi na kusaidia wanyonge, Hapi amekua ni Mkuu wa Mkoa anayependwa na kusikilizwa na wananchi wake mijini na vijijini. Hakuna asiyemfahamu RC Hapi kama ni kimbilio la wanyonge Iringa. Ni mtu anayetajwa kuwa na uwezo mkubwa wa kusikiliza, kushawishi na kutatua matatizo kwa busara na muda mfupi. Hili ni shubiri kwa ngome ya upinzani Iringa ambayo mara zote hutumia matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa.
*
5. Mabadiliko makubwa Iringa ndani ya muda mfupi.*

Chini ya mwaka mmoja, RC Hapi amefanya mambo makubwa Iringa. Kuwezesha bombardier kutua Iringa, matibabu kwa wazee, kuongoza kwa ukisanyaji mapato (mabilioni ya Nguzo), kusimamia ujenzi wa vituo vya afya na hospitali za wilaya, kutatua kero za machinga, bodaboda, migogoro ya ardhi pamoja na kuboresha nidhamu ya watendaji wa serikali ni baadhi ya mambo makubwa aliyoyasimamia Hapi ndani ya muda mfupi. Haya yamewafanya wananchi wa Iringa waone kuwa walichelewa sana kumpata RC wa aina ya Hapi. Wananchi wamepata nafasi ya kuona udhaifu wa viongozi waliokuwepo na hasa wa kisiasa.

*6. Kuvuruga upepo wa kisiasa wa Msigwa.*

Kwa wale wanaofuatilia siasa za Tanzania, watakubaliana nami kuwa hali ya kisiasa ya Mchungaji Peter Msigwa Iringa ni mbaya na hana matumaini ya kushinda 2020. Turufu ya Msigwa imebaki kwenye makosa ya CCM kukosea kuweka mgombea.
Wafuasi wake wanapungua kila uchao na amesikika mara nyingi bungeni na kwenye mikutano yake akimtaja RC Hapi kama mtu anayemyima usingizi.
Watu wa karibu na Msigwa wanasema hana raha, anafanya kila namna kuhakikisha anachafua jina la RC Hapi na pengine kushawishi mamlaka ya uteuzi kumuondoa.

*7. Ushindi wa CCM kiti cha Naibu Meya Iringa.*

Katika uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Iringa Joseph Lyata (CCM), Hapi anatajwa kuongoza mikakati ya ushindi kama alivyofanya kwa Meya Ben Sitta kule Kinondoni akiwa DC. Mara nyingine tena pamoja na Chadema kuwa na wingi wa madiwani kuliko CCM, iliangukia pua. Chadema ina madiwani 15 na CCM 13, lakini CCM ilishinda uchaguzi kwa kura 15. Chuki na lawama za upinzani zilielekezwa kwa RC Hapi.

*8. Kudhibiti watendaji waliokuwa wanatii CHADEMA Iringa.*

Kutokana na nguvu ya upinzani Iringa, baadhi ya watendaji wa serikali manispaa na Mkoa mzima wa Iringa walikua watiifu (loyal) kwa Chadema na Msigwa. Siri za vikao vyote vya serikali na mikakati ngazi mbalimbali zilikua zinamfikia mchungaji Msigwa moja kwa moja.
RC Hapi baada ya kuingia Iringa amefanya kazi kubwa ya kuvuruga mtandao huu wa watendaji. Wako walioshughulikiwa, kuhamishwa, kusimamishwa kazi na hata kuonywa, ili kuwarejesha kwenye utii wa serikali. Leo hii imekua nadra kuona siri za kiutendaji za serikali zinafika kwa Msigwa na kundi lake kama ilivyokua zamani. Barua, memo za serikali n.k hatuvisikii kwenye mikutano ya Msigwa Mwembetogwa. Nidhamu imerejea.

*9. Kupindua agizo la Manispaa kuzuia ukarabati wa nyumba za wananchi masikini.*

Manispaa ya Iringa chini ya Chadema ilipitisha katazo la kukarabati nyumba mitaa ya uswahilini. Mtu yeyote ambaye alitaka kukarabati hata ufa wa nyumba hakuruhusiwa isipokua ajenge gorofa. Mitaa hiyo yenye watu wengi wa hali ya chini na nyumba za kizamani, nyumba zilianza kuanguka. Kila aliyetaka kukarabati hata choo alitakiwa kujenga gorofa. RC Hapi alipofika alitengua amri ya manispaa na kusema ni uonevu na mkakati unaolenga kuwalazimisha masikini wauze nyumba zao kwa matajiri na waondoke mjini. Hivyo Hapi akaruhusu wananchi kukarabati nyumba zao zilizokua zinaanguka na kama kuuza wauze kwa hiyari. Hili liliwafurahisha wananchi wa mjini. Kwa Chadema huu ulikua mwiba mkali. Msigwa alisikika akilalamika bungeni kuwa RC anaingilia MipangoMiji.

*10.Ukimya wa RC Hapi kwa Msigwa*

Tangu Hapi aingie Iringa hajawahi kumjadili Au hata kumtaja jina Mbunge wa Iringa Peter Msigwa hadharani. Hata pale ambapo Msigwa humshambulia RC vikali, Hapi hajawahi kumjibu. Ni kama vile Hapi kampuuza Msigwa na anajua hesabu zake zitaishia wapi. Jambo hilo linamyima sana usingizi Msigwa Na Chadema kwakua wamezoea siasa za malumbano ambazo kwao zinawapa uhai (Kiki). Kwenye hili, hakuna anayejua kwanini Hapi amechagua mbinu hii na nini anapanga. Msigwa ni mtu anayependa malumbano na vita ya maneno.

*11.Mikakati,Msimamo na kujiamini kwa RC Hapi.*

RC Hapi ni mtu jasiri na anayejiamini katika kazi zake. Ni mtu asiyekubali kushindwa na jambo na hayuko tayari kuyumbishwa. Hili linamfanya kutoogopa kuchukua maamuzi na kupambana na wale wanaoonekana kuwa maadui wa serikali na chama chake.
Aidha, Hapi anatajwa kuwa fundi wa mikakati ya kisiasa ambayo Chadema Iringa wanamlaumu kutumia uzoefu wake katika kuivunja ngome yao Iringa. Kila jambo baya la Chadema Iringa lazima lihusishwe na Mkuu huyo wa Mkoa hata kama limefanywa na wengine.

Kwa sababu hizi 11, unaweza kuona kuwa RC Hapi ni msumari wa moto kwa uhai wa upinzani na wanaharakati hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu. Maadui wa RC Hapi hawatalala usingizi hadi wahakikishe RC Hapi ama anarudi nyuma au anatiwa woga. Silaha kubwa ya Chadema ni kuwatikisa watendaji ambao wanaonekana mwiba kwao ili warudi nyuma. Wanafanya hivyo kwa kutumia mitandao, vyama vya harakati, majukwaa ya kisiasa na hata michango bungeni.
*WAANDISHI WA HABARI*
Sakata la waandishi wa habari na hoja ya vitambulisho vya wajasiriamali ni mfano tu wa vita hiyo.
Hakukua na ulazima wowote wa waandishi wa Iringa Au Jukwaa la Wahariri TEF kutoa tamko dhidi ya RC kwa jambo ambalo wangeweza kumpigia simu na kuomba ufafanuzi kutoka kwake kama Kiongozi.

Katika tasnia ya habari kumejaa waandishi wengi wasio na vitambulisho vya wanahabari ( press cards) ambalo ni takwa la kisheria. Leo hii ukiita waandishi huwezi kujua nani mwandishi wa habari rasmi na nani tapeli.

Aidha, waandishi wa habari wengi hawana mikataba rasmi na kampuni wanazofanyia kazi na hawajasajiliwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Ni wachache wenye ajira rasmi na mikataba inayotambulika.

Kauli ya RC Hapi imefungua mjadala wa kulinda na kutetea maslahi ya waandishi hawa ambao hatujawahi kusikia Jukwaa la wahariri TEF likipigania haki zao za kupata mikataba.

Sisi wana Iringa tunasema, RC Hapi usirudi nyuma. Songa mbele na ulipokanyaga usiachie.
Maneno ya mitandaoni yasikurudishe nyuma. Maadui zako wanasubiri uogope, urudi nyuma ili watangaze ushindi.

Swali moja tu; wao walikua wapi Kufanya haya ambayo RC Hapi kafanya ndani ya muda mfupi?
Wamwache RC wetu afanye kazi aliyopewa na Rais Magufuli. Mitandao ya Twitter, whasap n.k sio kipimo cha kazi ya RC Hapi. Maana huko kila aliyeshiba ugali na asiye na kazi ya kufanya anaweza kuandika chochote anachojisikia hata kwa bando la mkopo.

Anayetaka kujua RC
Hapi anafanya nini aje huku tuliko wananchi mitaani na vijijini. Wanyonge tuliokosa pakusemea leo tunapata haki zetu, tunasikilizwa!

*Mti wenye matunda daima hupigwa mawe.*

*Aloyce Siyovela
Iringa.*
 
Aliyekuyuma,mwambie tusipangiane. Kila mmoja anahaki na Uhuru ndani ya nchi yetu. Hakuna aliyejuu ya katiba yetu,mama Tz Ndiyo mkuu wetu. Huyo help abadilike.tunataka mabadiliko kiuchumi,kiutamaduni na kisiasa. Ova
IMG_20190606_075458.jpeg
 
Ungeacha wakuandikie wengine , na nakuhakikishia kwamba una siku chache sana madarakani , Amos Makalla tuliwahi kumpa taarifa kama hizi lakini akatupuuza , kumbuka huyu aliwahi kuwa Mweka hazina wa ccm Taifa , siyo wewe uliyekuwa mesenja
 
Unajisifia kuua upinzani ambao upo kisheria? tunataka maendeleo siyo siasa
 
Hapa nyonyesha Ally Hapi na huyu mtoa hii post ni kama vile sura mbili za za pande ya sarafu moja
 
Mkuu umechambua vizuri sana.

Kila raia mzalendo wa nchi hii anatamani sana mchango wa uongozi wa Hapi.

Hata tulio mikoa ya mbali, tunakunwa na kuguswa sana na uongozi wa huyo Rc nakutamani panapo majaaliwa siku1 ahamishiwe na kwetu.

Huyu kijana ana uwezo mkubwa sana wa kutanzua kero za raia kwa weledi mkubwa na bila upendeleo.

Ingawa kuna msemo usemao 'kizuri hakidumu', lakini kwa uwezo wake Jalali, Rc Hapi atafika mbali.
 
Zezeta linajipigia debe na kujisifia upumbavu. Kumbuka kulikua na kina Kleruu lakini bingwa Mwamwindi aliposema sasa yatosha kilichobaki ni historia.
 
Mkuu, rudi darasani kwanza! Umetumia muda na nguvu nyingi kuandika lakini mantiki hakuna kwa sababu ww unafurahia kiongozi wako kufanya makosa kwa wengine kwakuwa ww hujaguswa ss ipo siku utakuja kusema mengine kinyume cha haya uliyoandika
 
Hii mutu inafikiri sana bila kuwakandamiza wapinzani wako husongi mbele
 
Ukisoma neno kwa neno utajua tu hapa kinanda kinajipiga chenyewe ,,a
Dogo sisi si watoto kihivo ,ungesubiri uandikwe sio kujiandika.
 
Ukisoma neno kwa neno utajua tu hapa kinanda kinajipiga chenyewe ,,
Dogo sisi si watoto kihivo ,ungesubiri uandikwe sio kujiandika.
 
Dah!! Nilianza kusoma nikajua kuna kitu cha maana.

Ni maoni yako mkuu, shukrani for nothing
 
Kwann ujifiche katika Id fake kisha ujisifie hivyo, kama utendaji wako ni mzuri acha watu wakusifie. Watch out Hapi
 
Back
Top Bottom