samurai
JF-Expert Member
- Oct 16, 2010
- 11,495
- 24,174
China wapo zaidi ya bilioni moja na hatuwafikii kiuchumi. Nigeria wapo zaidi ya milioni 170 na hatuwafikii kiuchumi hata kwenye masuala ya kiutamaduni na kijamii. Sisi ambao hatujafika milioni 60 ndio tuwe na hofu eti wingi wa watu ndio ukaribishaji wa umaskini!!.
Ongezeko na mipango.
Kasi ya Ongezeko na Mipango ya hiyo kasi ya Ongezeko.
Kivuko cha MV Nyerere kilizama na watu zaidi ya 250 huku capacity yake ni 101 na tumeambiwa kivuko kile kinahudumia watu zaidi ya 50000, jibu hapa utaona tumeshindwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhudumia watu wale 50000.
Kuzaliana sio kosa kosa ni pale mnapozaliana huku hamuwezi na hamzaweza kuweka mipango kulingana na kasi hiyo na idadi ya watu wenu.. Baada ya miaka X tutakuwa watu X na serikali imeweka utaratibu X kuhudumia na kuitumia idadi X.
China walizaliana wakiwa na Mpango maalumu ambao umefanikiwa ndio maana wakaweka plan ya mtoto mmoja kwa familia moja, sasa wana plan nyingine ambayo hatujui itachukua miaka mingapi, kuhakikisha wachina wanasambaa dunia nzima lengo kuitawala dunia na kuwepo kila sehemu and this is special project ndio maana sasa wameongeza idadi kufikia watu 2 kwa familia moja.
Wahindi waliweka hiyo plan nafikiri sasa unaona wahindi wako kila mahali na bado wanajaribu kupambana na mchina hasa kwenye hardware maana kwenye software mchina alikuwa bado akajaribu kuiba kwa wahindi, utaona namna gani duniani watu wanaishi kwa mipango.
Tujadiliane kwa uhalisia, sisi tunataka kuzaana tuna mipango gani na ya muda gani na lengo letu tuwe wangapi na tumeweka mikakati kwenye hiyo idadi? TUSIJADILI KISHABIKI TAFADHALI.