TANZIA Mama Sabetha John Mwambenja afariki dunia

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,916
2758651_IMG-20210430-WA0088.jpg

Mama SABETHA JOHN MWAMBENJA amefariki katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akioatiwa matibabu.

Mama Mwambenja alipata kuongozana taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki ya Exim, na benki ya Covenant.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi!

=======
WASIFU MFUPI
Sabetha alijiunga na Benki ya National Bank of Commerce (NBC) mnamo 1974.

Kufuatia mfululizo wa majukumu ya kitaalam katika benki hiyo, aliteuliwa kama Meneja Mkuu wa Maendeleo na baadaye kama Mkurugenzi wa kwanza wa Mikopo katika historia ya Benki hiyo.

Mnamo Januari, 1998 aliteuliwa kama Meneja Mkuu wa Benki mpya ya Exim Tanzania Limited. Nafasi hiyo ilimfanya kuwa Meneja Mkuu wa kwanza Mwanamke katika historia ya tasnia ya benki nchini Tanzania.

Baada ya miaka 2 ya utendaji mzuri, mnamo mwaka 2000 alipanda cheo kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa benki ya Exim. Kwa mara nyingine tena, akawa ni CEO wa kwanza Mwanamke na pekee katika sekta ya benki nchini Tanzania, nafasi aliyokuwa nayo kwa miaka 14 hadi 31 Desemba, 2010.

Chini ya uongozi wake, Benki ya Exim Tanzania Limited, imekua kwa kiwango kikubwa na kuwa kati ya benki 10 kubwa nchini Tanzania kwa upande wa mtandao wa mali, faida na matawi.

Mnamo 2010 aliteuliwa kuwa mwanachama wa The World Entrepreneurship Forum (WEF), lililoanzishwa na EMLYON Business School na KPMG.

Mnamo Januari, 2011, Bi. Mwambenja aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki mpya iliyoitwa Covenant Bank for Women Tanzania Limited, benki iliyowalenga kuwasaidia wanawake na wajasiriamali wadogo kupata fedha na mafunzo.

Kwa sababu ya kujitolea kwake kuwawezesha wanawake, Sabetha Mwambenja alikuwa miongoni mwa wachache waliochaguliwa kuiwakilisha Tanzania kama mwanajopo katika Mkutano wa kwanza wa Wake wa Marais wa Afrika (African First Ladies Summit), ulioandaliwa na Taasisi ya George Bush uliofanyika nchini Tanzania.

Mwaka 2012 Rais Jakaya Kikwete alimteua Bi Mwambenja kuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE ambayo iko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
 
Nani anayezipongeza?

Niazime maneno ya beberu kulaani huu mghafiliko:

"Oooooops, ghooosh!"

Mkuu bujibuji ni kiherehere cha Android tu.

Badala kusajili kama nilivyoandika "kuongezeka" yenyewe ikafanya yake na kuwa "kupongezwa."

Nimesikitika sana kwa makosa hayo na nimeparekebisha ipasavyo.


Hiiiiii bagosha!

Nakazia poleni wafiwa, poleni wana Mbeya, na poleni Bujibuji.
 

Mama SABETHA JOHN MWAMBENJA amefariki katika hospitality ya Aga Khan alikokuwa akioatiwa matibabu.

Mama Mwambenja alipata kuongozana taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo benki ya Exim, na benki ya Covenant.
Mipango ya mazishi inaendelea kufanywa.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
Poleni Wanyakyusa wote
 
Back
Top Bottom