Ni majungu kama iivyo kwa majungu mengineJuzi nikiwa Dodoma nilimtembelea rafiki yangu ambaye ni afisa mwandamizi serikalini. Akanionesha muswada uitwao FINEST VALOR.
Kwanza nikataka kumjua mwandishi. Nikaona ni Novatus Igosha. Japo hatujawahi kuonana lakini nafahamu umahiri wake katika masuala ya diplomasia na siasa za kimataifa. Ni moja ya vijana waliobarikiwa ubongo wenye uwezo mkubwa.
Nikapitia Dibaji nikakuta imeandikwa na mzee Pius Msekwa. Nikapitia sura kadhaa kujua maudhui, nikaona amefanya narrative analysis ya utawala wa Magufuli kwa miaka mitano iliyopita na dira yake kwa miaka mitano ijayo. Amechambua strength, challenges na opportunities na kushauri mambo kitaalamu na kwa weledi.
Amemtafsiri Rais Magufuli kama VALOR yani mtu jasiri asiyeogopa vitisho hata katikati ya hatari. Amejaribu kuonesha Magufuli alivyochukua hatua katika mambo ambayo alitarajiwa angesita kuchukua hatua.
Amechambua kuhusu diplomasia ya kimataifa akifanya historical reflection tangu enzi za Mwalimu. Ametoa ushauri wa kitaalamu wa mambo ya kufanya kuimarisha diplomasia yetu.
Kwa kifupi ni moja ya reflective analysis bora kabisa. Akifanikiwa kuchapa muswada huu kuwa kitabu basi atakua ameipa serikali "road map" ya kule wanakotaka kwenda.
Lakini nikasikia wapo watu ndani ya serikali wamezuia muswada huu kuchapwa. Nikauliza hofu inatoka wapi mbona hakuna baya? Mbona haujaandikwa na mpinzani? Mbona kachanbua kwa kuonesha changamoto na suluhisho?
Nikaambiwa kuna watu wanahofia muswada huu ukiwa kitabu kitasomwa sana kwa sababu kimetoa majawabu ya mambo mengi. Hivyo watakua wamevuliwa nguo, maana wataulizwa kwanini mambo hayo hawakuyaona wao hadi yaonekane na kijana mdogo asiye na wadhifa wowote serikalini? Hiyo ndio vita?
Nikaambiwa aliwahi kuwekwa "mahabusu" na Naibu Katibu wa wizara kwa sababu ya muswada huu. Yapo madai kuwa wanataka kumuibia muswada huu wauchapishe kwa jina la wizara. Hivyo kufanikiwa kuzika juhudi zake. Nilimhoji @novatusigosha nikasikitika sana.
Kwa nchi zilizoendelea angepaswa kutumika vizuri kwa maslahi ya taifa. Thadei Ole Mushi huwa anasema akili kubwa zote ni mali ya Rais. Lakini huku kwetu ni vice versa. Yericko Y. Nyerere aliwahi kusema ukiwa akili kubwa Afrika sio sehemu salama kwako. It's either uipumzishe ili uishi vizuri, au uitumie uishi kwa mashaka.!