kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Mali, Burkina Faso zatuma ndege za kivita nchini Niger kukabiliana na hujuma tarajiwa ya ECOWAS
Mali na Burkina Faso zimeituma ndege za kivita Ijumaa kwenda Niger ili kukabiliana na hujuma tarajiwa ya kijeshi ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
Ripoti iliyorushwa hewani na televisheni ya taifa ya Niger iliangazia juhudi za pamoja za Mali na Burkina Faso za kuunga mkono Niger na kutumwa kwa ndege za kivita ndani ya mipaka ya Niger.
Televisheni ya Niger imeripoti kuwa Mali na Burkina Faso ziligeuza ahadi zao kuwa hatua madhubuti kwa kupeleka ndege za kivita kujibu shambulio lolote dhidi ya Niger na kubainisha kuwa ndege hizo ni za kivita za Super Tucano.
Wakati wa mkutano wa Ijumaa wa wakuu wa kijeshi wa ECOWAS nchini Ghana, tarehe ya uingiliaji kati wa kijeshi unaokuja nchini Niger haikuwekwa wazi lakini umoja huo ulitangaza kuwa vikosi vyake vya kijeshi viko tayari kuingilia kati mara tu amri itakapotolewa.
Burkina Faso na Mali, zote zikiwa chini ya uongozi wa kijeshi, hapo awali zilitoa taarifa ya kuunga mkono Niger dhidi ya operesheni iliyopangwa ya kijeshi ya ECOWAS yenye lengo la kuondoa serikali ya kijeshi madarakani. Nchi hizo mbili zilionya kwamba uingiliaji kati wowote utaonekana kama tangazo la vita dhidi yao.
Jenerali Abdourahamane Tchiani, kamanda wa zamani wa walinzi wa rais wa Niger, alijitangaza kuwa mkuu wa serikali ya mpito mwezi uliopita baada ya Rais Mohamed Bazoum kuondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi.
Hivi karibuni pia Mkuu wa Jeshi la Algeria ameonya kuhusu jaribio la kuivamia kijeshi nchi jirani ya Niger na kusema kuwa uvamizi wowote wa kijeshi wa madola ya kigeni nchini Niger utatishia utulivu na usalama wa eneo zima la Sahel ya Afrika.
Jumatano ya tarehe Julai 26, jeshi la Niger lilifanya mapinduzi na baadaye kumuweka kizuizini rais wa nchi hiyo, Mohammed Bazoum.
Katika upande wa eneo la ardhi, Niger ndiyo nchi kubwa zaidi katika eneo la Afrika Magharibi. Ina ukubwa wa kilomita mraba milioni 1.3.