Malcolm X alishindwa kutuunganisha Wabantu

Nelson Jacob Kagame

JF-Expert Member
Dec 26, 2022
9,472
12,887
Malcom x alikua anatuchanganya sisi wabantu.Haiwezekani unatuambia tuachane na tamaduni za kizungu na tuache dini za kizungu na taratibu za maisha ya kizungu.

Afu wakati huo huo unatushauri tufuate dini na tamaduni na taratibu za maisha za Kiarabu. Hana tofauti na Martin Luther jr ambae alikua anapromote uzungu wa Kimarekani na imani za kiluther kwa wabantu, au Elijah Muhammad na itikadi zake za kiarabu kwa wabantu wa amerika ya kaskazini.

Wewe kama kiongozi wa kibantu basi ulipaswa uwashawishi wabantu warejee kwenye ubantu wao na tamaduni za kibantu na dini za kibantu na mila na desturi zao.

Sasa kiongozi wa kibantu afu una jina la kiarabu na imani ya kiarabu ,sisi tukuelewe vipi.

Kiongozi wa wabantu afu hauna motisha ya kuunadi ubantu wetu dhidi ya jamii nyingine duniani sisi tukueleweje?

Ndio maana kwa watu tunaojielewa tulikua tunaona na kujua Malcom x na Martin luther king walifeli kutuunganisha wabantu, na walikua wanapromote tamaduni nyingine katika ubantu wetu.

UNAPOTAKA KUTUUNGANISHA SISI WABANTU USITUMIE DINI ZA WAKOLONI KUTUUNGANISHA, HAPO LAZIMA UTATUGAWA NA NDIO KILICHOTOKEA KWA WABANTU WA AMERIKA KASKAZINI.

Malcom x alikosea au alipata mafunzo yasiyo sahii kuhusu ubantu na alikua anatupoteza kuhusu utambuzi wetu wa ubantu wa mababu zetu. Wabantu sisi tunaunganishwa na ubantu wetu na mila na desturi za babu zetu wa kibantu,toka kizazi mpaka kizazi kupitia koo zetu za makabila mbalimbali.

Na kutokana na kufeli huko, kulimsababishia kueleweka kwa wale wabantu wa pan Africanism ambao tuna imani zetu katika ubantu wetu.

NB: Wabantu tuna asili ya kujikataa na kukataa asilia zetu na kudharau rangi ya ngozi zetu na kutokana na kukandamizwa zaidi ya karne tano na jamii nyingine hapa duniani, tumejikuta tulikua wanyonge wa kiakili na kiimani na kitamaduni dhidi ya jamii za watu wenye rangi za ngozi tofauti na zetu.
 
Wabantu hatukuwa na Imani yoyote kubwa zaidi ya vodoo iliyojaa uchawi, kwa kiasi kikubwa dini za kigeni zilituunganidha. Malcolm X hakuona mbadala wa ukristo zaidi ya uislamu
 
Kabla ya kuuawa Malcom X alikuwa anafanya kazi kubwa sana ya kuunganisha 'Wabantu' Unachomshutumu alifanya kinyume chake kabisa. Alisafiri nchi huru nyingi za Afrika akihubiri jinsi watu weusi wa duniani kote wanatakiwa kuungana. Mwishoni mwa maisha yake hakuhubiri dini, alihubiri black nationalism. Hakuna mtu aliyewahi kuhamasisha umoja wa watu wesui duniani kote kama Malcom X. Mwishoni mwa maisha yake alisema kubwa moja ya sababu ya taasisi yake kuwa ya kidini ni kuwapa watu weusi msingi wa maadili, lakini watu weusi wa dini zote walikaribishwa.
 
Alikua mkristo safi,akapigwa mafundisho ya Elaijah Mohamed na dhehebu lake la NOI,akaondoa jina la baba yake ndio kujiita Malcolm X,baada ya kuzinguana na Elijah Mohamed akaenda Saudia kuhiji na kuwa muislam wa sunni na kujiita el-Hajj Malik el-Shabazz.
 
Malcom x alikua anatuchanganya sisi wabantu.Haiwezekani unatuambia tuachane na tamaduni za kizungu na tuache dini za kizungu na taratibu za maisha ya kizungu.

Afu wakati huo huo unatushauri tufuate dini na tamaduni na taratibu za maisha za Kiarabu. Hana tofauti na Martin Luther jr ambae alikua anapromote uzungu wa Kimarekani na imani za kiluther kwa wabantu, au Elijah Muhammad na itikadi zake za kiarabu kwa wabantu wa amerika ya kaskazini.

Wewe kama kiongozi wa kibantu basi ulipaswa uwashawishi wabantu warejee kwenye ubantu wao na tamaduni za kibantu na dini za kibantu na mila na desturi zao.

Sasa kiongozi wa kibantu afu una jina la kiarabu na imani ya kiarabu ,sisi tukuelewe vipi.

Kiongozi wa wabantu afu hauna motisha ya kuunadi ubantu wetu dhidi ya jamii nyingine duniani sisi tukueleweje?

Ndio maana kwa watu tunaojielewa tulikua tunaona na kujua Malcom x na Martin luther king walifeli kutuunganisha wabantu, na walikua wanapromote tamaduni nyingine katika ubantu wetu.

UNAPOTAKA KUTUUNGANISHA SISI WABANTU USITUMIE DINI ZA WAKOLONI KUTUUNGANISHA, HAPO LAZIMA UTATUGAWA NA NDIO KILICHOTOKEA KWA WABANTU WA AMERIKA KASKAZINI.

Malcom x alikosea au alipata mafunzo yasiyo sahii kuhusu ubantu na alikua anatupoteza kuhusu utambuzi wetu wa ubantu wa mababu zetu. Wabantu sisi tunaunganishwa na ubantu wetu na mila na desturi za babu zetu wa kibantu,toka kizazi mpaka kizazi kupitia koo zetu za makabila mbalimbali.

Na kutokana na kufeli huko, kulimsababishia kueleweka kwa wale wabantu wa pan Africanism ambao tuna imani zetu katika ubantu wetu.

NB: Wabantu tuna asili ya kujikataa na kukataa asilia zetu na kudharau rangi ya ngozi zetu na kutokana na kukandamizwa zaidi ya karne tano na jamii nyingine hapa duniani, tumejikuta tulikua wanyonge wa kiakili na kiimani na kitamaduni dhidi ya jamii za watu wenye rangi za ngozi tofauti na zetu.
Nelson, ni bahati mbaya watu wengi tunachanganya vitu. Kabla ya yote nikulize: mila na desturi za kibantu ni zipi na dini ya kibantu ni ipi?

Kinachotuunganisha watu wa Africa ukitoa mataifa ya Kiarabu, ni rangi ya ngozi yetu na history ya kutawaliwa. Nje ya hapo, hakuna cha mila, tamaduni, desturi wala dini unayoweza kusema hii ni ya Mubantu kwasababu kila jamii ilikuwa na taratibu zake tofauti na jamii nyingine. Hata hapa kwetu Tanzania kwa mfano, wanaume wa jamii ya Masaai wanatoboa masikio, kusuka nywele na wengine uvaa hadi vipedo. Mtoto wako akifanya hayo utasema ni uhuni na siyo mila za hao unaowaita wabantu.

Malcolm X alizaliwa na kukulia Marekani, usitegemee angekuwa na mila na desturi tofauti na aina ya makuzi aliyoyakuta. Ni bahati mbaya tu alizaliwa kwenye jamii iliyokuwa ikibaguliwa ya watu weusi pamoja na historia ya utumwa ndivyo vilivyomfanya awe na sense of where he belongs. Ukristo au Uislamu siyo dini za Kizungu. Vyote hivi vianzia Mashariki ya kati na kuenea. Kwa hiyo dini kama Imani, Malcolm X au Martin Luther Jr hawakuwa na makosa kueneza kile walichokuwa wakikiamini.
 
Malcolm X aliuawa pale alipotaka kutoa Siri za Elia Muhammad mtu aliyemslimisha.
 
Malcom X ni mtu ambaye—wakati mwingine—alikuwa na mitazamo finyu ambayo nadhani ilitokana elimu ndogo ya historia ya dunia. Ukiielewa sawa sawa historia, huwezi Ulaumu Uislam au Ukristo—as a doctrine—sababu dini zote mbili zimepinga sana ubaguzi na dhulma.

Mfano, wakati anaaminisha kuwa Ukristo ni chombo cha Ubaguzi ndani ya US, na kuhimiza wafuate Uislam; ni kwa sababu hakujua namna waarabu walivyoshiriki kwenye Ukoloni na biashara ya utumwa—ambayo kwa kweli haikuwa sababu ya Uislam. So, Malcolm X alikuwa na uelewa mdogo wa dunia.
 
Back
Top Bottom