Malaya jela kwa kuuza miili yao lakini mafisadi wanauza mali zetu wanaachwa

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Malaya jela kwa kuuza miil yao

WAKAZI wawili wa Dar es Salaam, wamehukumiwa kifungo cha wiki mbili jela baada ya kukiri shtaka la kufanya biashara ya kuuza miili yao kinyume cha sheria. Washtakiwa hao ni Aisha Nassoro (20) na Upendo Julius (39), wote wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive,kujibu shtaka lililokuwa likiwakabili. Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi, alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Aprili 23, mwaka huu eneo la Buguruni.

Magodi alidai siku ya tukio majira ya usiku eneo hilo, washtakiwa walikamatwa na polisi waliokuwa katika doria wakifanya biashara ya kuuza miili yao, huku wakijua ni kinyume cha sheria. Washtakiwa walikiri shtaka linalowakabili na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, William Mutaki, aliwahukumu kutumikia adhabu ya kifungo cha wiki mbili jela kama fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.

Katika hatua nyingine, wakazi watatu wa Dar es Salaam wamefikishwa katika mahakama hiyo kujibu shtaka la kupiga debe na kubughudhi abiria katikati ya jiji. Watuhumiwa hao ni Said Salum (19), Rajae Ismail (28) na Damian George (25).

Magodi alidai siku ya tukio Aprili 23, mwaka huu katikati ya jiji washtakiwa walikamatwa na polisi wakiwafanya vurugu na kubughudhi abiria waliokuwapo kituo cha daladala, huku wakijua ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa walikana shtaka na Hakimu Mutaki aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 7, mwaka huu itakapotajwa tena na washtakiwa walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini bondi ya Sh100,000 kila mmoja

MWANANCHI
 
Tena haya mambo yananikera sana,mtu aliyefanya makosa anajulikana kabisa alafu anaachwa,wanaacha kumkamata aliye7bisha mpaka hao wadada wakawa macd,tazama mtu ameiuza Bandari ya Mtwara bila hata kutupatia taarifa hajashikwa.Hiv Mlima KILIMANJARO unaweza kuuzwa pasipo Wachaga kujua?,Wanakusini wenzangu hizi ni dharau za dhahiri.
 
Back
Top Bottom