Makontena 100 ya bidhaa bandia yakamatwa

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
ZAIDI ya makontena 101, yalikamatwa hadi kufikia mwaka jana yakiwa na bidhaa bandia na bidhaa hizo kuharibiwa huku wahusika wakifikishwa mahakamani.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, ameliambia Bunge mjini hapa kuwa kukamatwa kwa bidhaa hizo bandia ni mojawapo ya mikakati inayochukuliwa na
Serikali katika kukabiliana na uingizaji wa bidhaa bandia.

Alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazoathirika na uingizaji wa bidhaa bandia kutokana na utaalamu unaotumika kumpotosha mlaji juu ya uhalisia wa bidhaa kuwa ni wa hali ya juu hivyo ni vigumu kubaini mara moja udanganyifu huo.

Alisema ili kukabiliana na uingizaji wa bidhaa bandia nchini, Wizara ya Viwanda na Biashara
kupitia Tume ya Ushindani imechukua hatua mbalimbali ikiwemo ya kuimarisha idara ya kupambana na bidhaa bandia katika bandari zote nchini na kutoa elimu kwa waagizaji wa bidhaa.

Nyalandu alisema hatua nyingine ni kushirikiana na wamiliki wa nembo na alama za bidhaa (Brand Owners) ili kupata taarifa za uingizaji wa bidhaa kutoka nje.

Alisema mkakati mwingine ni kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma juu ya namna ya kutambua bidhaa bandia na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi ili kudhibiti uingizaji wake.

Naibu Waziri alisema mwenye kumiliki Nembo au Alama ya Bidhaa, ndiye mwenye nafasi kubwa ya kutambua udanganyifu uliofanyika katika bidhaa kuliko mtu mwingine.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Chambani, Salim Hemed Hamis (CUF), aliyeuliza je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza udhibiti wa uingizaji wa bidhaa bandia nchini?



cChanzo: Habarileo
 
Bila shaka nyingi ya mali hizi zitakuwa ni kutoka China.
 
Sasa hawa wanaokamata wanatakiwa wayarudishe yalikotoka sio kuchoma moto. Ni heri wahusika wakayauzie huko walikoyatoa
 
ufisadi umezidi kila mtu anajaribu kuchukua chake mapema.....hii hatari sana kwa kweli na inasikitisha sana!
 
Hii nchi yetu hii tunakoelekea siko kabisa nina kila sababu ya kusema imepoteza mwelekeo, wanaohusika na uingizaji wa hizi bandia sio kuwa ni wafanyabiashara pekee bali hata hawa viongozi wetu wa ngazi za juu wanahusika pia, ninao mfano hai wa pale bandarini kuna mizigo ikifika pale huwa hailipiwi ushuru wala kukaguliwa kwa kisingizio kuwa ni mizigo ya mama( 1st Lady) jamaa wakileta ubishi tu wanamvutia waya kuongea na mama moja kwa moja sasa kwa namna hii tusitegemee kama hizi bidhaa bandia zitaisha ikiwa walioko ngazi za juu ndio wahusika wakubwa wa hili jambo
 
Back
Top Bottom