Makongoro: CCM imehamishia uchafu UKAWA

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Mwandishi Wetu

HATUA ya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukimbilia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivi karibuni inaelezwa kuwa ni tiba kwa chama hicho kikongwe nchini na sumu kwa mahasimu wao hao wa kisiasa.

Pamoja na kukinusuru chama hicho, hatua hiyo pia inaelezwa kuwa somo la kudumu kwa CCM na kwamba iwapo viongozi wake hawatasikia, basi watakuwa ni sikio la kufa lisilosikia dawa.

Kauli hiyo imetokana na ufafanuzi uliotolewa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM kwa Wilaya ya Kyela uliofanyika mjini Ipinda, Jumapili iliyopita.

Katika hotuba yake ya uzinduzi, Makongoro alijikita zaidi katika utamaduni wa kuleana ulivyovuruga maadili ya uongozi ndani ya chama hicho, kiasi cha kufikia hatua ya mafisadi na wezi kuheshimiwa huku waadilifu wakibezwa na kudhalilishwa.

Mtoto huyo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alikielezea kitendo cha vyombo vya juu kuwaengua baadhi ya makada katika kinyang'anyiro cha urais kupitia CCM, pamoja na kujiandaa kwa miaka zaidi ya ishirini, kwamba kilikuwa cha busara na chenye tija kwa chama na taifa.

"CCM imepata somo la kudumu, isiposikia basi hilo litakuwa sikio la kufa lisilosikia dawa," anasema mmoja wa wagombea ubunge kupitia CCM mkoani Mbeya, akitoa maoni yake kuhusu hotuba ya Makogoro.
Baadhi ya makada wa CCM wamebainisha kwamba mtikisiko uliokikumba chama hicho wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wake wa nafasi ya urais ulisababishwa na utamaduni wake wa kulea matatizo kwa muda mrefu ambayo baadaye huwa matatizo makubwa yenye kusumbua chama na taifa.
Makongoro asiliba

Makongoro kasiliba, ni maneno mawili yaliyotumiwa na baadhi vijana kuelezea hotuba ya Mbunge huyo wa Bunge la Afrika Mashariki na mtoto wa Baba wa Taifa, maneno yenye kuelezea hisia kali inayojibainisha katika hotuba yake dhidi ya kitendo cha kulea uovu ndani ya uongozi wa taifa.

Kada huyo wa CCM alianza kwa kutoa taswira ya harakati za ukombozi zilivyoendeshwa na waasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere, kwa upande wa Tanganyika na Abeid Amani Karume kwa Zanzibar, kupitia vyama vya TANU na ASP na baadaye CCM.

Akirejea historia ya Tanzania, Makongoro alisema waasisi hao waliwaunganisha wakulima na wafanyakazi, ambao awali walikosa umoja, na kupitia umoja huo wakakomboa nchi zao. Hivyo kubainisha kuwa nchi hii ilishakombolewa, na kwamba huo ni urithi walioachiwa walio wengi, ambao ni watoto wa wakulima na wafanyakazi, wakombozi wa taifa la Tanzania.
"Nchi hii ni huru, tumerithi nchi iliyo huru na tajiri, watu wanapita kudanganya, ooh! mimi tajiri, sipendi umasikini, huyo ni mwongo, sana sana ni kibaka tu," alisema Makongoro na kushangiliwa kwa nguvu na umati mkubwa uliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.

Anaijenga hoja yake kwa kuiangalia CCM katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi, akisema ni katika kipindi hicho ambapo baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho walipoingiwa na ubinafsi, wakajali zaidi maslahi yao binafsi, wakatumia dhamana walizopewa kwa maslahi yao na kuwatelekeza walio wengi.
"Leo hii, CCM wote tunaitwa wezi, mafisadi, vibaka, wakati kundi hilo halikuzidi hata watu ishirini," anasema Makongoro.

Makongoro alienda mbali zaidi akibainisha kuwa kilichofanywa na kundi hilo ndogo ndani ya chama na hatua ya uongozi wa juu wa chama chao kutowachukulia hatua, ilikuwa ni kutowatendea haki walio wengi, Watanzania aliowaita watoto wa wakulima na wafanyakazi, kisha akaomba kura akisema; "Watendeeni haki walio wengi, hawa kina mama, baba, vijana na watoto, wachagulieni Magufuli, Mwakyembe na madiwani wa CCM."

Makongoro alikumbushia njama za kumfukuza aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sitta akisema; "Walitaka kumfukuza Spika na wabunge 12, walitaka kumfukuza Mwakyembe kwa sababu alihoji matendo yao, nikasema hatoki mtu hapa, mtatoka nyie, mnakumbuka kwenye NEC, nikasema huyu (Lowassa) ni mwizi.

Kikwete amejaliwa moyo wa rehema, lakini imepitiliza, wenzie walitambua hilo, yeye hakujua, akiamini wako pamoja, CCM ilikuwa inafanya makosa ya kiufundi, Mwenyekiti Kikwete akahoji sababu ya CCM kuonekana mafisadi, nikamwambia, toa Lowassa.

Tumepewa chama hiki (CCM) kutukomboa, lakini mafisadi wanatufarakanisha, mwaka 2015 mafisadi walipokaribia kutunyang'anya chama chetu, tulikataa, wakaondoka wao.

Ukawa wataipata ‘fresh', wangekuwa wanamjua kama tunavyomjua mimi na Mwakyembe, maana yule jamaa ni mchonganishi…! Mkutano Mkuu tukasema, Lowassa hapati na vibaka wake hawapati, hapa ni Magufuli, ni kazi tu."
Kwa mujibu wa Makongoro kulikuwa na wenyeviti 10 wa mikoa wa CCM miongoni mwa wafuasi wa Lowassa ambao walifanya kazi kubwa ya kuwatisha viongozi wa chama hicho kwamba iwapo asipopitishwa basi chama hicho kikongwe kingesambaratika, lakini baada ya kukatwa mtu wao, waliondoka wawili tu kumfuata na waliobakia wakafuata utaratibu wa chama chao.

Anasema kilichofanyika kwa kada huyo kuhamia Chadema ni baada ya kuwatuliza viongozi wa vyama vinavyounda Ukawa akiwataja, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwamba baada ya tulizo hilo viongozi hao wamefunga midomo na sasa hawazungumzii tena hoja ya ufisadi.

"Sabuni ya kumsafisha Lowasa hakuna, mmemsikia sio, kawaambia kama huna ushahidi shirt up, wote kimya, sisi hatujanyamaza, tunaongea," alitamba Makongoro, kasha akaendelea akisema; "CCM kilikuwa na maradhi, sasa yamehamia Ukawa, sasa wataipata fresh, wameitaka wenyewe."

Dk. Mwakyembe na demokrasia
Mbunge wa Jimbo la Kyela aliyemaliza muda wake, Dk. Harrison Mwakyembe alizungumzia umuhimu wa demokrasia na uvumilivu wa kisiasa akisema uwepo wa vyama vingi nchini ni muhimu katika ustawi wa demokrasia nchini na afya kwa maendeleo ya nchi.

"Leo hii Chadema wanashindwa kukemea ufisadi kwa sababu wameukaribisha wenyewe sebuleni, CCM Magufuli amepatikana kupitia mchakato wa kidemokrasia," alisema Dk Mwakyembe.
Mgombea huyo wa CCM kwa nafasi ya ubunge Jimbo la Kyela, aliwasihi wananchi wa wilaya hiyo kuachana na vurugu zisizo na msingi na kupigania maendeleo ya wilaya yao.

"Kyela tuweke mbele maendeleo, tuache upuuzi, tukiendekeza upuuzi tutaachwa nyuma," alisema mgombea huyo akigusia vurugu zilizosababishwa na wafuasi wa Chadema kuvamia mkutano huo wa uzinduzi kampeni za CCM, na kuongeza; "Wenzetu jana walizindua kampeni zao, ni jambo la afya, sisi ni watoto wa baba mmoja, mama mmoja, tunajenga nyumba moja, hatuhitaji kugombania fito."

Pamoja na kuzungumzia umuhimu wa kuvumiliana, Dk Mwakyembe aligusia pia kazi alizofanya jimboni humo ikiwamo miradi mbalimbali ya barabara, shule, bandari na afya, na kuelezea azma yake ya kukamilishwa kwa ile miradi inayoendelea na kuibua mipya.

Vurugu mkutanoni
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo, vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema walivamia mkutano wakiwa na mabango na kusimika bendera za chama chao kwenye eneo la mkutano, kinyume cha makubaliano ya vyama vya siasa wilayani humo kuhusu uendeshaji wa kampeni zao. Hatua ya vijana hao ilisababisha mzozo kati yao na wale wa CCM na kufikia hatua ya kupigana, huku CCM wakiwataka wenzao hao kuondoka ama kuheshimu mkutano wao.

Shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwandambo alimweleza mwandishi wa habari hii kwamba baada ya vijana wale kuzidiwa, waliwasiliana na wenzao wa Kyela mjini ambao alisema waliletwa kwa gari la mizigo aina ya Toyota Canter, kuja kuongeza nguvu. Hata hivyo, katika hali ambayo hawakuitarajiwa walijikuta nao wakidhibitiwa kwa kupigwa na vijana wa CCM, walioonekana dhahiri walijiandaa kudhibiti vurugu za wafuasi wa Chadema.

"Walizoea kutufanyia fujo, hatukujibu, kila tukilalamika kwa mbunge hutuambia tuwe wapole, tusiwajibu, tumechoka, walitunyanyasa uchaguzi wa kwanza, safari hii hatutawaruhusu watufanyie fujo, mbona sisi hatuendi kwenye mikutano yao kuwafanyia fujo?" alihoji kijana mmoja wa UVCCM ambaye hata hivyo jina lake hakuweza kutoa jina kutokana na vurumai hizo.

Katika mkutano wa kampeni wa mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Mgufuli, wafuasi wa Chadema pia walipita na magari yao yakiwa yamebeba wanachama na mabango ya chama hicho huku wakizomea na kuonyesha alama ya vidole viwili inayotumiwa na chama hicho.

Hata hivyo, busara iliyotumiwa na viongozi wa CCM pamoja na Jeshi la Polisi kuwasihi na kuwazuia wanachama wa CCM kutojibu, ilisaidia kuepusha shari.

Chanzo Raia Mwema
 
...kwa usafi gan asee??! Binti zake wawili wapo Maryland USA wanakula maisha...
 
Mchezo wa chandimu.....Mako kiboko ya Lowasa......Lowasa Kibaka
 
Watoto wao wanauza ngada alafu rais anaundiwa tume ya kusafiri wakati MWANA nyamala wanapasua tezi dumeeee huhu ccm wana matumizi mabovu ya hela hawafai viva Roma
 
Piga tu; wape vidonge vyao
Laki n inpia aangalie kuna ya kesho maana baada ya uchaguzi kutahitajika umoja. Ukifikiri unawasema wapinzani tu ujue pia unagusa na watu walioko ndani ya Chama chako.
 
Alivyotoka ccm kwenda.nccr alikuwa mchafu na amerudi ccm akiwa msafi hivyo wapinzani wanatoa uchafu aliohama nao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom