Makonda: Ukawa Wanapokea Sh. 450,000/= Kwa Siku!

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,412
3,272
Wakuu ile hali ya woga imezidi kuiandama CCM kwa kuiogopa CHADEMA na sasa hata baada ya CHADEMA kujificha ndani ya UKAWA bado CCM wanawayawaya.

Hali hiyo ilimkumba Nape kwa kusema CHADEMA inafadhiliwa na nchi za Magharibi ili kuiangamiza CCM.

Hali hiyo imejirudia baada ya Kijana Makonda kudai UKAWA imefadhiliwa na Mataifa ya nje ambapo hupokea kiasi cha Sh. 450,000/- kwa siku ili kuharibu mchakato wa Katiba mpya.

Akiongezea akadai hata hivyo fedha hizo hazitawasaidia kwani UKAWA itakufa mapema na CHADEMA Itakufa Rasmi mwaka 2015.

Swali kwa Makonda iweje serikali ishindwe kuzuia fedha hzo haramu zisiingie nchini?

Je muda wa CHADEMA kufa umezogezwa mbele kwa nini ilihali Nape na Wasira walitabiri CHADEMA kufa 2013/2014?

CCM jikiteni kuwaeleza wananchi kuhusu ahadi alizotoa Kikwete zimefikia wapi na hili deni la Taifa trilion 30 zinalipwaje achaneni na mambo ya Utabiri.
 
ni kweli ukawa wamehongwa na mataifa ya kigeni wavuruge amani ya nchi
 
Vipi wakati akiongea simu na ipad za watu zilikuwa salama?

Kijana mwizi wa simu na lap top anajua nini juu ya UKAWA?
 
Anao ushahidi wa beyond reasonable doubt, wa hayo anayoyasema?

Je Makonda anajua kuwa, no research no right of speech?
 
Thubutu!!! Haogopi jinsi Serikali ilivyomruka Masele!? Kama ana ushahidi wa kuthibitisha kauli yake si azitaje nchi husika na kiasi cha pesa kilichotolewa na kila nchi?

Mbona hayatajwi hayo Mataifa?
 
Aliyetoa wazo la kuwa na Ukawa ndiye mtu muhimu wa kukumbukwa kwa karne hii. 1404795918996.jpg
 
Mwizi wa simu kwenye bunge la katiba.
Huenda hakuiba, alijiazimisha kupitia ile kitu yao ya ubinafsishaji na huenda lengo ilikuwa aendelee kuwa hewani JF. Kwani ni nani asiyejua kuwa zile za ufadhili wa buku saba ziko pale lumumb...
 
Cha kushangaza ni kwamba ndani ya Ukawa ccm wanaiona Chadema tu Mbatia,Lipumba hawawaoni kweli uhai wa Chadema ni Mauti ya ccm.
Adui mwombee njaa sio kifo.
 
Tatizo la maccm kila mtu ni msemaji wa chama (eg Masele) lakini akitaja nchi tuu basi wanamruka. Ndio maana hapa wamekomaa kusema UKAWA wanapewa pesa na mataifa ya nje lakini hawataji. Waseme basi kama wana ubavu tuone.
Chama ni tawala lakini hakijiamini kimebaki na majungu tuu


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Vurumushaneniiiii ila nchi yetu mtuachie ikiwa salama!
Heri mkate mkavu na amani kuliko nyama na vinono ktk vita!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom