Makonda fuatilia dhuluma mradi wa fidia Jangwani watu wanalipwa 170,000 badala ya milioni 4 aliyosema Waziri

Stuka

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
214
686
Mradi wa kulipa fidia wananchi wa Jangwani kupisha mwekezaji una mambo ambayo sio ya kawaida, Waziri wa TAMISEMI, Mchengerwa ametangaza wananchi hao watalipwa sh. milioni 4 lakini kinachoendelea kwenye utekelezaji watu wamesainishwa fomu za kulipwa laki na 70 bila kujali ukubwa wa familia.

zoezi hili Makonda wananchi wanakuomba ujitokeze kwenda kuwasikiliza wananchi wa jangwani wanaopisha eneo hilo ambalo kuna tetesi kuwa anataka kupewa mwekezaji lakini wananchi wananyanyaswa kwa kudhulumiwa fidia na wajanja wa mjini ndani ya serikali.
7e7ad68c-393b-44e7-8968-e2a6e3da415d.jpg
 
Ttzo ili suala mmelifanya siasa badala ya kuangalia maisha ya watu
Ingetolewa elimu kwanza ni nani anasitahili million4 na na anasitahili 170,000 na nan apati ata mia ila kwa haya yanayoendelea watu watalia sana

Lakin pia tuache kutetea ujinga kwann ulipwe kuhama sehemu ambayo inahatarisha maisha yako, yan uhai ni wako na familia yako afu unataka ulipwe ili uondoke kuokoa uhai wako

Wangeachwa tu wakai ili sku ikija mvua moja kubwa wakafa km50 iv watahama wenyewe na ata iyo fidia hawataomba
 
Mradi wa kulipa fidia wananchi wa Jangwani kupisha mwekezaji una mambo ambayo sio ya kawaida, Waziri wa TAMISEMI, Mchengerwa ametangaza wananchi hao watalipwa sh. milioni 4 lakini kinachoendelea kwenye utekelezaji watu wamesainishwa fomu za kulipwa laki na 70 bila kujali ukubwa wa familia.

zoezi hili Makonda wananchi wanakuomba ujitokeze kwenda kuwasikiliza wananchi wa jangwani wanaopisha eneo hilo ambalo kuna tetesi kuwa anataka kupewa mwekezaji lakini wananchi wananyanyaswa kwa kudhulumiwa fidia na wajanja wa mjini ndani ya serikali.
View attachment 2817528
Daaa! Makonda ndo amekuwa tumaini la Watanzania badala ya serikali yenyewe. Makonda mungu akubariki Sana mwanawane watu Wana Imani na wewe kuliko hata Rais
 
Makonda afuatilie kama nani?,why ujipe usemaji wa watanzania?,haya ndio mambo ambayo awamu ya kwanza iliharibu, kabla ya kuweka taasisi imara za kusaidia utawala bora, President Nyerere akaamua kujiweka yeye kama ndiye mtatuzi pekee, matokeo yake kila Rais anakuja na mbwembwe zake, uzuzu na ujinga wa watanzania ndio mtaji wao, ilitakiwa anayeona ameonewa aende police akafungue docket au aende kwa PP, makonda sio mtatuzi wa matatizo
 
Ujinga wa Watanzania unawapq sana sifa na umaarufu wa kipuuzi wanasiasa wapuuzi!!

Elimu na uwazi ndio tatizo hapo.

Mfano kwa dakika 2 nilizomsikiliza Mchengerwa siku ile nilimuelewa sana kua 4mln ni kwa wamiliki wa viwanja husika ambapo hiyo wanapewa kama fidia ya kiwanja lakini pia wameshawafanyia valuation ya thamani za nyumba zao ambapo napo pia watalipw!!

Hapo hiyo 170,000 nafikiri nauli ya kuhamisha vitu kwa wale ambao ni wapangaji kwenye hizo nyumba ambazo wamiliki wanalipwa fidia maana wengi wa wamiliki wa hizo nyumba hawaishi hapo bali wanazitumia kama vitega uchumi.

Makonda hapo wa kazi gani?!! Kwa chain of command ipi?!!
 
Asante kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom