Makonda aiagiza Serikali impe Mbowe kibali cha kuruka na Helicopter na kama hana mafuta ameongea na Rais ili wamsaidie

Wakimpa ndege baada ya siku kadhaa.wanachomoa kidogo boya la pampu ndege inapata ajali mboe anaungua angani.

wambakishie mrembo wake erythrocyt kilio
 
Wote tunajadili haya haya, na ndio hoja yangu kuwa haya yanawatoa watu kwenye hoja za msingi, na matukio hayataisha ila wapinzani kuwa spika ya matukio ya ccm ni mbaya zaidi.
Kwa taarifa yako tukio ni tukio tu, bila kujali linajadiliwa na nani. Ni mara ngapi yanatokeza matukio kwa wapinzani na wote tunajadili hayo hayo, au ccm huwa mnajadili tofauti na hayo? Cha muhimu ni kuangalia unajadiliwa katika mlengo upi. Kama zaidi ya 70% ni negativity kuhusu nafasi yako, hapo unafaidika na Nini?
 
Katibu mwenezi wa CCM ndugu Paul Makonda amesema amemuona Mbowe akiwa Songwe Lakini hana helicopter kama tulivyomzoea

Hivyo Makonda ameviagiza Mamlaka za Serikali zinazohusika na Utoaji wa vibali vya anga wampe Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe Kibali na kama hana mafuta aseme kwani ameongea na Rais Samia waweze kumsaidia

Chanzo: EATV
Hivi kwanini rais anapenda kujuzungushia watu wenye tuhuma na sifa mbaya katika jamii? Kuna waziri mmoja mpendwa wake anajulikana kwa wizi na ufisadi wa kutisha bado anamuacha kwenye wizara nyeti, na sasa kamfufua huyu mwenye tuhuma nzito za mauaji ya watu wasio na hatia, utekaji na utesaji
 
CCM wanajua njia nzuri wa kuwatoa wapinzani kwenye hoja ni kuwapa vichwa vya habari, na uteuzi wa Makonda unakwenda kufanikisha hilo vizuri.
Na mfano mzuri ni jinsi ambavyo sasa hivi tunacheza ngoma yao.

Wanachama wengi wa chadema ndio wanaripoti tukio la leo la Makonda, na alikuwa sahihi kusema vyama vya upinzani ni maReporter.

Upinzani wakitaka waondoke kwenye huu mtego, waache kuwa spika ya kujadili matukio ya CCM.

Upinzani gani unamuongelea Makonda. Hapa wanaotoa taarifa za Makonda ni chawa wa CCM.
 
Katibu mwenezi wa CCM ndugu Paul Makonda amesema amemuona Mbowe akiwa Songwe Lakini hana helicopter kama tulivyomzoea

Hivyo Makonda ameviagiza Mamlaka za Serikali zinazohusika na Utoaji wa vibali vya anga wampe Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe Kibali na kama hana mafuta aseme kwani ameongea na Rais Samia waweze kumsaidia

Chanzo: EATV
Mimi naanza kuona tabu kidogo. Huyu msemaji wa CCM anapotoa amri kwa Serikali anaongea kwa madaraka yapi? Kwenye hotuba yake inaonyesha kama majukumu yake hajayajua. Kimsingi yeye siyo muwajibishaji. Kazi yake kubwa ni kutetea ilani na kututangazia maamuzi ya vikao mbalimbali. Na kusambaza aliyotumwa na wakubwa zake. Sana sana, kwa upande wa mawaziri, anachoweza ni kuwachongea kwa wakubwa au ndani ya chama. Lakini si kuwawajibisha kwa hali yoyote ile. Kwa hotuba yake ya leo, yaonekana hata kazi yake hajaijua.
 
Ni dalili za chama kuishiwa
.yaani form four ya 28 utegemee ikinyenyue chama kinacho tawala dola kweli ...hebu tuwe serious kidogo jamani.
 
Daud Albert Bashite hana uwezo wa kufanya kazi ya uenezi wa Chama Chochote cha siasa.Mwaka kesho 2024 ni uhakika kabisa ataondolewa."Mark my words".
 
Back
Top Bottom