Makombo siyawachii-sapoti

Jan 4, 2012
61
23
MAKOMBO


Ama kwa mlaji kweli,ambaye hapuuzii,
Asiye na mushkeli,kula afanya bidii,
Mle hujiweka mbali, kukera sidhamirii,
Nakula siyawachii,niyakutapo makombo.
Dk. Kassim Pazi Haumotile,
MWANANCHI, Septemba 27,2013


MAKOMBO(SAPOTI)


Makombo yana utamu,nikutapo sizembei,
Halani hutia timu,nafasi siichezei,
Siwezi kulaza damu, na yalipo sipotei!
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.


Niyakutapo makombo,mbali nayo sisogei,
Nakula nijaze tumbo,ni bure hayana bei,
Hujifunga kwa masombo,uvivu siyatendei!
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.


Ninapoamua kula,hapo mimi silegei,
Hujihifadhi mahala,nilengapo sikosei,
Maini au salala,kwangu yote ni "Okei!"
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.

Yanabana matumizi,pesa haziteketei,
Makombo siyabakizi,nipewapo simezei,
Walao "kilezilezi",kuliwa siwatetei!
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.

Makini wajiliao, naapa siwaendei,
Na wale kwa raha zao,macho siwakodolei,
Ila kwa wachezeao,huruma siwaonei!
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.


Kaditamati makombo,kuacha sitegemei,
Si kwamba nina msimbo, "kichwani hazienei",
Ndani yake kuna jambo,leo siwaelezei!
Nakula siyaachii, niyakutapo makombo.

Lambert F.Chialo( Mhadhiri wa malenga)
Magogoni, Dar es Salaam,
0713961860



 
Ndo nini hiki???

Hahah
Unakumbuka uchambuzi wa vitabu vya Kiswahili hususani fasihi andishi?
Wakumbuka mashairi ya kitabu cha Diwani ya Mloka kama 'Hutaniacha Morogoro', 'Ndege Tunduni', 'Kwa nini' na mengineyo?
 
Hahah
Unakumbuka uchambuzi wa vitabu vya Kiswahili hususani fasihi andishi?
Wakumbuka mashairi ya kitabu cha Diwani ya Mloka kama 'Hutaniacha Morogoro', 'Ndege Tunduni', 'Kwa nini' na mengineyo?

hahaa hatakuwa hakumbuki huyu............

Diwani ya mloka lol sikunyingi saana
 
hahaa hatakuwa hakumbuki huyu............

Diwani ya mloka lol sikunyingi saana

Heheh...ndio maana nimemkumbusha maana miye bado ninazo kumbukumbu hizo ingawaje nimesoma kitambo sana.

Wakati wa kujibu mtihani wa kiswahili 'NECTA', katika yale maswali ya fasihi, ilikuwa ni lazima ujumuishe na beti kadhaa.
 
Back
Top Bottom