Bundewe
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 400
- 141
Najua siasa za Igunga zimekwisha na wachakachuaji wameendeleza historia yao kwa kujiundia vituo bandia na kujipatia kura za chee. Lakini nimejiuliza ni kwa nini makatibu wakuu hawa wa vyama vinavyotawala kwa ubia katika nchi yetu hawajaonekana igunga ikiwa wao ndo watendaji wakuu. Mhe. Wilison Mkama hajaonekana kama ilivyo kwa counterpart wake wa CUF Seif Sharrif Hamad. Hivi nae Mkama alizuiliwa na RA? Na kilichomzuia Seif ni nini kwa upande wake? Mwenye taarifa naomba atujuze tafadhali.