Makamu wa Rais wa Zambia ni Mzungu: Ukoloni unarudi?

Mawazo yako yamegandia wakati wa ukoloni,mabadiliko yote ya kijamii na kiuchumi yatokeayo Afrika kwenye mawazo yako hayakai kabisa. Kwa vile ngozi nyeupe iliongoza Afrika wa kati wa Ukoloni kwa mkono wa chuma,kwako kila mwenye ngozi nyeupe ni sehemu ya utesaji huo. pole sana mkuu. ni ugonjwa huo wahi tiba.

Nakubali kabisa kwamba ni sehemu ya utesaji na hata leo bado wanatutesa tu kwa ukoloni mamboleo na kunyonya maliasili zetu kama zamani. Kata minyororo mkuu vinginevyo utaendelea kuwa mateka.
 
ndugu yangu acha fikra mgando ukoloni sio rangi....kuna wakoloni wengi tu ndani ya ccm ambao ni Weusi na watanganyika asilia
 
The problem is that you think being African is Black, and being Zambian is black There a lot of black Zambians who are not Zambian, Let take for example Dr chiluba, he was congolise by origin he is the relative to Katumbi,Dr Kaunda is from Malawi , Mkapa has origin of Mozambique, Nyerere has origin of Burundi the least is endless, Sata has origin of Tanzania The thing I want to bring up is that we need leaders who will take Africa to the next level of development, The so called indigenous Tanzania or Zambia have done little to develop their country, The was just part of history of man kind we cant keep living in the past we need to soldier on,

What are you talking about? I think you are advocating and embracing Political Privatization whereby we privatize not only commercial settings but also political organizations/parties!

I am talking about Africa for Africans and not for whites. Let a Congolese rule Zambia but not a white man come to rule Zambia, etc.
 
Siyo ukoloni ni ushirikishaji wa raia wote. Huyo mzungu kam ni raia wa Zambia acha awe makamu wa raisi. Mbona huku kwetu kuna wahindi kibao ni wabunge ikiw ni pamoja na mbunge wangu Mheshimiwa Dewji
 
Kwa hiyo unataka tuongozwe na wazungu? Haya mkuu sasa hao Viongozi wako weusi ni wa nini si mngeongozwa na wazungu kuelekea kuchukua dola?

Indirectly tunaongozwa na wazungu so far mtu anakugharimia mpaka pesa ya kulipia mishahara ya wafanyakazi unaweza kusema hakuongozi hivi leo ni kitu gani tunaweza kuambiwa na marekani au uingereza tukakataa? kujitawala ni kuwa huru kiuchumi! Yaliyofanywa na Wamarekani wakati wa ziara ya Obama wanaingilia hata kuongoza ndege na kupekua abiria mbona hawakufanya hivo South? au China? au Russia? halafu unajitapa huongozwi na wazungu acha fikra fupi kimbunga? hizi buku saba zimekutoa akili kabisa??!!
 
Mkuu OSOKONI yaani umejituma kabisa na kuwa mtumwa kweli kweli. Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinasema heri mtumwa wa kutumwa kuliko mtumwa wa kujituma. Kwa hiyo huna ndoto ya kuwa kama Rusia ama China au South Africa? Umejitekesha nyara kwa wazungu? wewe ndio fikra zako zimekufikisha hapo kwamba hata uje utawala gani basi wazungu watendelea tu kutunyanyasa na sisi wenyewe kujisalimisha kama mateka na wao kutuchukua kama nyara za vita?

Yaani huna matumaini hata kidogo kwamba Tanzania itakuja kuwa na nguvu za kiuchumi? Mbona unapiga kelele kwamba mali asili yetu inapokwa na kutapanywa?

Huamini kabisa kwamba unaweza kuiongoza nchi ya kiafrika kama Tanzania yenye rasrimali lukuki ukaweza kuwalipa watumishi wako mishahara minono badala ya mishahara ya kijungu jiko ama kulipiwa na wazungu? Huamini kabisa kwamba tunaweza kuwa na uwezo wa kuwapekua abiria hata akija Rais wa Amerika ili hali uchumi ukiongozwa vyema na kujivunia mali asili zetu.

Nimeamini wewe ni miongoni mwa wale wasemao Mzungu anamkaribia Mungu kwani ukitoa herufi Z kwenye neno Mzungu unapata MUNGU!

Last edited by a moderator:
Inaama OBama ambaye sio Tu Mmarekani Mweusi ila Baba yake Ni mkenya Kutawala USA ni Afrika ina tawala USA?
 
Mkuu OSOKONI yaani umejituma kabisa na kuwa mtumwa kweli kweli. Niliwahi kusoma kitabu kimoja kinasema heri mtumwa wa kutumwa kuliko mtumwa wa kujituma. Kwa hiyo huna ndoto ya kuwa kama Rusia ama China au South Africa? Umejitekesha nyara kwa wazungu? wewe ndio fikra zako zimekufikisha hapo kwamba hata uje utawala gani basi wazungu watendelea tu kutunyanyasa na sisi wenyewe kujisalimisha kama mateka na wao kutuchukua kama nyara za vita?

Yaani huna matumaini hata kidogo kwamba Tanzania itakuja kuwa na nguvu za kiuchumi? Mbona unapiga kelele kwamba mali asili yetu inapokwa na kutapanywa?

Huamini kabisa kwamba unaweza kuiongoza nchi ya kiafrika kama Tanzania yenye rasrimali lukuki ukaweza kuwalipa watumishi wako mishahara minono badala ya mishahara ya kijungu jiko ama kulipiwa na wazungu? Huamini kabisa kwamba tunaweza kuwa na uwezo wa kuwapekua abiria hata akija Rais wa Amerika ili hali uchumi ukiongozwa vyema na kujivunia mali asili zetu.

Nimeamini wewe ni miongoni mwa wale wasemao Mzungu anamkaribia Mungu kwani ukitoa herufi Z kwenye neno Mzungu unapata MUNGU!

Ninaamini kabisa Tanzania chini ya rais mweusi inaweza kuwa strong economically kuliko hata Marekani lakini sio chini ya system iliyopo sasa!Tunatakiwa ku abolish kabisa system iliyopo sasa waje watu wengine wapya wenye mawazo mapya na waliojaa uzalendo, chini ya CCM hilo halitakaa litokee asilani!Mfano mdogo sana sasa tunaandika katiba ya nchi kwa maslahi ya sasa na vizazi vijavyo lakini CCM wanafanya kila hila wahodhi mamlaka yote ya kuandika katiba ili wabakie madarakani,.hawajiulizi wabakie madarakani ili wafanye nn walichoshindwa kukifanya kwa miaka 50 waliokuwepo madarakani! serikali inayoyokunja twiga na kuwapeleka ulaya, serikali inayoangamiza tembo., serikali inayocheka na wazembe, mafisadi, wezi serikali inaangalia namna elimu inavoporomoka kwa kasi, serikali inayokaa kimya huku watu wanakufa kwa magonjwa ya kutibika,serikali inayoshindwa hata kusimamia watu waweze kujitosholeza kwa chakula!!Hiyo hapana afadhali wakoloni!!
 
the problem with you is that you dont know zambian politics, dr guy scot is more of a zambian than a white man he has done so much to zambia than even a lot of black zambian, in zambia they do not elect a leader based on race or tribe, they elect a leader based on performance ,zambians are politically mature compared to us in tz

tanzania ni mbingu ya illiterates huwa hawachagui performance wanachagua sura na vigezo vingine vya kipumbavu kama dini na kabila ya mtu na ccm wanalisimamia hili kwa dhati.
 
Haya ni mawazo ya masafa mafupi sana! Kwani hiyo nafasi aliipata kwa kuwashikia wazambia mtutu wa bunduki? Na hao weusi wako unaolilia si ndio hao wanaotupa mabomu kwenye mikutano ya kampeni wakiona wameshindwa hoja?

Bora kuwa na rais mzungu anayewajali raia kuliko rais ambaye watu wake wanatupiwa bomu mchana kweupe lakini anapotezea tu!!!
 
Zambian Born Becomes First Black Minister In Wales

View attachment 100780A Zambian born man has become the first ever black minister for Wales in the Welsh Assembly.

Vaughan Gething has taken on a new position as deputy minister for tackling poverty and has been sworn into his role today.
Gething was born in Zambia in 1974, where his father whom he describes as "a white Welsh economic migrant" was working as a veterinary doctor. His mother is a black Zambian.
He has represented the constituency of Cardiff South and Penarth as a Labour MP since the National Assembly for Wales election of 2011.
 
Wapinzani hawashindwi kuongoza. Kinachotokea ni shida kubwa mbili: Moja, chama tawala wanataka viongozi wapya waonekane hawajui, hawafai. Kwa hiyo wanajenga mazingira ya shida kabla ya kuondoka ili hao wajao wapate shida. Yaani hulka ya roho za watu weusi ni kama vile Bush angeficha mafaili ya upelelezi kuhusu Osama bin Laden ili Obama ashindwe pa kuanzia. Pili, Wananchi viwango vyao vya elimu vipo chini wanadhani ukibadili uongozi leo, kesho matatizo yanakwisha. Yaani ni kama hili tatizo la Rushwa ambalo limestawishwa Tanzana kuanzia 1978/79 hadi hii leo, Chadema ikiingia madarakani leo wananchi watataka rushwa iishe kesho. Which is impossible! Au tatizo la udini ambalo limeanza kujengwa 1985 hadi hii leo, Chadema ikipata madaraka leo wananchi watataka kesho wakiamka wakute mashehe na mapadiri wanacheza bao. Again sidhani kama hilo litaenda haraka hivyo. Changes take time!

umejibu vizuri na kistaarabu...lakini huoni kwamba Satta anachukua muda mrefu sana kulipa visasi kuliko kuongoza? na vile ilivyo sasa kwa mazingira yetu hapa unaona kwamba CDM watashawishika kwenda na njia hiyo inayopteza mwelekeo na taswira ya utaifa na maendeleo?

....Tatizo kubwa la wapinzani Africa ni kuweka matumaini makubwa kwa wafuasi wake ili wapate kura wakijua kwamba mambo ni magumu kuliko wanayoyaahidi au kusema kwenye majukwaa (na siyo tatizo la wananchi kua wajinga kama unavyofikiria kwa sana)..ahadi na kujenga matumanini makubwa yasiyoweza kufikiwa ndiyo tatizo la kuzorota kwa demokrasia ya Africa kwa sababu wapinznai wakiingia wanajikuta hawawezi kufanya yale waliyoahidi na wanakua watawala wababe na wenyewe, wanabana wapinzani, wanakandamiza demokrasia na kugawanya jamii ili waendelee kushika dola kwa sababu wameshindwa kumeet expecttions za wananchi wao na wameshindwa deliver on their promises..it has nothing or little to do with former rulers

Nafikiri cha kujiuliza ni je hizi ahadi za CDM zinatekelezeka? na zipi ni priority ya muda mfupi (ili kuoanisha ushindi wa uchaguzi na matumaini ya mwanzo ya wananchi na kujipa muda zaidi ya kutekeleza ahadi nyingine)..otherwise CDM ni CCM nyingine tu in waiting
 
Back
Top Bottom