Makamu wa Rais Dkt. Mpango Mgeni Rasmi Mkutano wa 52 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Phillip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa 52 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya ambapo Kauli Mbiu ya Mwaka 2023 hapa nchini ni: 'Tawheed ya kweli haiwezi kusimamishwa bila ya Ukhalifa'.

Ikielezwa kuwa maana ya Kauli Mbiu hiyo ni kuwa mfumo wa Ukhalifa ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za Nabii Adam ndio njia pekee ambayo Mwenyezi Mungu Hudhihirisha Umoja wake Duniani na leo hii Tawheed ya kweli itasimamishwa kupitia Ukhalifa ulioanzishwa tena na Mwenyezi Mungu katika Uislam sawa na ahadi iliyotolewa na Mtume Muhammad s.aw.
d6b8f38f-8017-4c6a-ab9b-fabbc3ecfbc7.jpeg

Viongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Tanzania na Ghana wakati wa mkutano na Wanahabari, Septemba 28, 2023

Akizungumzia ujio wa mkutano huo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry ambaye ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Tanzania amesema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Septemba 29 hadi - Oktoba 1, 2023 katika eneo la Ahmadiyya Centre lililopo Kitonga, Kata ya Msongola, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema watu 5,000 hadi 6,000 kutoka mataifa tofauti wanatarajiwa kuhudhuria Jalsa hiyo ya 52 wakitokea Nchi za, Kenya, Uganda na Ghana wanatarajiwa kuhudhuria.

Amesema "Mkutano huu unafanyika ili kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwa washiriki, kupata Taqwa, kumjali Mwenyezi Mungu, kuepukana na mabaya, kupata moyo wa huruma na kuongeza upendo baina yao na wawe mfano wa kujenga udugu baina yao, unyenyekevu na ukarimu na tabia ya ukweli vipatikane ndani yao."

Ameongeza kuwa viongozi wa Kitaifa wa kiserikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini mbalimbali na jamii kwa ujumla nao wanatarajiwa kualikwa ili washiriki katika kutoa nasaha zao.
8d69337b-47b9-41bb-bf01-ddd9971f1abe.jpeg

b282afa3-8e78-4fce-aa19-321a8596f34b.jpeg


Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Ghana
Upande wa Muhammad bin Salih ambaye ni Amir na M'bashiri Mkuu Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Nchini Ghana ambaye yupo Nchini, amesema “Mkutano huu umekuwa ukifanyika katika mataifa mengi na kushirikisha watu wenye hadhi tofauti ikiwemo Rais, Mawaziri, Wabunge na wengine wengi.

“Mwaka 2021 hatukufanya mkutano huo Ghana kutokana na uwepo wa mazingira ya maambukizi ya COVID-19, safari hii tunatarajia kufanya mwanzoni mwa Mwaka 2024 inaweza kuwa Februari au Machi.

“Uzuri wa Mkutano huu unawashirikisha watu wa dini zote kwa kuwa lengo ni kuwafanya watu kuwa karibu na Mungu.

“Niwajulishe ndugu zangu Watanzania kuwa Ahmadiyya imefanya mambo mengi Nchini Ghana na itafanya hivyo pia hapa Tanzania, ikiwemo kuboresha elimu, kwani tunatambua Elimu ni Msingi wa maendeleo ya Nchi yoyote.”

Utaratibu wa kufanyika kwa Jalsa Salana (Mkutano wa kila mwaka) ulianzishwa na Mwanzilishi mtukufu wa Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s. kwa malengo ya kuwapatia waumini fursa ya kukuza udugu, maelewano mema na ufahamu wa pamoja miongoni mwao.

Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ni nini?
Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ni Jumuiya ya kimataifa inayopatikana kwenye zaidi ya Nchi 212 Duniani ikiwa chini ya kiongozi mmoja (Khalifa mtukufu). Lengo lake kuu ni kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam Duniani kote na kuwa mstari wa mbele katika kupinga maana zisizo sahihi zinazonasibishwa na mafundisho ya Uislam kama vile dhana potofu za ugaidi na misimamo mikali isiyovumilia wengine. Pia Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya inajitahidi kupambania amani duniani kote.

Jalsa Salana hufanyika katika kila nchi ambapo Jumuiya ya Waislam Waahmadiyya ipo, na hivi karibuni Jalsa hizo zimefanyika katika Nchi za Uingereza na Ujerumani ambapo washikiri wapatao 41,000 walihudhuria katika Jalsa ya Uingereza na 47,000 katika Jalsa ya Ujerumani.
 
Mbona kuna wabishi humu husema uislam hauna madhehebu, ni mmoja, sasa hawa waahmadiyya, wahabi, waislamiyya, wasunni, washia, wasufi ndio nini katika uislam? Tena hizi jumuiya zina waanzilishi wake watukufu, au ndiyo maswahaba wa mtume mohamed s.a.w ?
 
Back
Top Bottom