Makamu Mwenyekiti UVCCM, Rehema Sombi apokea vifaa, kusaidia wanafunzi katika vyuo sita

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Rehema Sombi amepokea vifaa mbalimbali vya kiofisi vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita kuwezesha elimu nchini.

Akipokea vifaa hivyo Septemba 14, 2023 Rehema ameishukuru UCSAF kwa kuonyesha nia ya kutoa mchango katika kugusa wanafunzi na elimu nchini huku akieleza kazi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya sita kuboresha na kuendeleza sekta hiyo.

“Serikali imeweka msukumo mkubwa katika sekta hii ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya ujenzi wa madarasa, kuongeza stahiki za walimu ikwemo kuwapandisha madaraja tena kwa mseleleko, kugharamia elimu kwa wanafunzi kutoka msingi hadi kidato cha sita (Elimu bila Malipo) na zaidi kupandisha kiwango cha mikopo ya wanafunzi wa elimu” amesema Rehema.

Ameongeza kuwa umoja wa vijana wa CCM umepokea vifaa hivyo na umepanga utaratibu mzuri kuviwasilisha katika vyuo vikuu vikasaidie kuwapunguzia gharama wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa lengo la kuboresha ufanisi wa wanavyuo iuendane na kasi ya sayansi na teknolojia nchini.

"Vifaa hivi vitatolewa kwa campus za Rukwa, Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Arusha na Singida kama awamu ya kwanza. Zoezi hili ni endelevu kwa Campus zingine," amesema.
IMG-20230914-WA0285.jpg
IMG-20230914-WA0284.jpg
IMG-20230914-WA0286.jpg
IMG-20230914-WA0283.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom