Elections 2010 Makamba panga safu yako ya kampeni upya !

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
Mheshimiwa Makamba, uliwahi kufukuzwa kazi ukiwa kama mkuu wa wilaya, uliondolewa si kwa utendaji wako mbaya wa kazi bali wakuu wengi wa idara wilayani kwako walikuangusha. Ukiachilia mbali siasa umekuwa mchapa kazi mzuri sana. Katika kipindi cha uchaguzi kampeni za CCM zisilenge kwenye kutoa ahadi ambazo mantiki yoyote. Hii timu ya kampeni ya Raisi ina mapungufu makubwa sijui ni nani anayemshauri Raisi, inawezekana kabisa mtu huyo hana malengo mazuri na CCM na Raisi mwenyewe vitu kama ahadi za bajaj zinatokea wapi? Alichotakiwa Raisi ni kuboresha huduma za afya vijijini, kuwapatia maji safi na kuongeza huduma za kijamii kama lengo lilikuwa ni kuwasaidia wajawazito basi Raisi alipaswa kuahidi kuongeza vituo vya afya na watendaji wake, bajaji hazitatua matatizo ya wajawazito, kinga ni rahisi kuliko tiba. Hii ahadi ya meli na uwanja wa ndege Kigoma nayo mh. Makamba ni kweli tunalitaka jimbo la Zito lakini ahadi kama hizi zitatuweka pabaya 2015; si vibaya kuahidi kuboresha usafiri Kigoma lakini ahadi zimekuwa nyingi na hazitekelezeki, cha msingi washauri wa Raisi katika kampeni wanaonyesha upeo mdogo sana wa kuchanganua mambo kumbuka ahadi hazitatui matatizo kinachotakiwa ni utekelezaji sera za chama. Panga safu upya ! mambo kimbelembele
 
we kama una muda wakutosha , ungekua unafanya mambo mengine, Makamba ndio mshauri wa JK mwenye akili zaidi, akifuatiwa na Tambwe Hiza, huu ushauri wako ni mwepesi sana, hata usoma, na hata akihadithiwa hatatilia maanani, nasikia ahadi ya Bajaj ni ushauri wa Tabwe Hiza.Ushauri wa kutengeneza kadi zile za kule Mkoani Mbeya alitoa Kingunge na idea ikatiliwa nguvu na Makamba na mkuu akakubali. hahaaaah. unapoteza muda wako kumshauri Makamba.
 
Kikwete+na+Sheikh+Mustafa.jpg
 
mwambie akupange wewe chama unaweza ukawa MS au TUMAIN
 
waache na hiyo safu yao dhaifu ya kupiga majungu ili waanguke na wafe kifo cha mende............shaabash
 
Unaishauri CCM leo?
Baba wa Taifa alichemsha. jamaa ni vichwa sugu hata ingekuwa ni wewe ungekuwa kama wao tu.
 
Nasikia huko Bukoba alitoa ahadi hata za kujenga barabara za vichochoroni kwa lami. Sijawahi kusikia raisi anatoa ahadi kama hizi za kujenga barabara za kichochoroni. Hizi zinashughulikiwa na manispaa. Yeye anatakiwa atuambie zile trunk road atazijengaje. Ni aibu tupu kwa rais wenu. Anatapatapa leo baada ya kugundua mshindani wake anauzika na ni chaguo la wengi. Bwahahahahahahaha. Yuko wapi mshikaji FMES siku hizi?
 
Back
Top Bottom