Makamba atumia Biblia kuwalaani Chadema: HUYU MZEE KACHANGANYIKIWA

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Makamba atumia Biblia kuwalaani Chadema

Thursday, 06 January 2011
Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba amekilaumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile alichoeleza kuwa kimekaidi amri ya mamlaka halali na kufanya maandamano yaliyoleta vurugu na maafa.

Akizungumza na gazeti hii jana, Makamba alisema kitendo kilichofanywa na Chadema ni cha kinyama na kinapaswa kulaaniwa na watu wote wanaoitakia mema nchi hii "Ukisoma Biblia katika kitabu cha Warumi Sura 13, imeandikwa " Itiini Mamlaka inayowazidi nguvu; hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu," alisena Makamba na kuaongeza: "Sasa mamlaka imesema msiandamane, ninyi mnaandamana.


Nasema hawakufanya vizuri. Sasa tumlaumu nani kama sio Chadema." Makamba alisema haoni sababu Chadema kuandamana kwa sababu ya suala la Umeya, kwani kama hilo ndio sababu, alipaswa kwenda mahamani kudai haki wanayoeleza kuwa imeporwa na CCM badala ya kufanya maandamano yenye madhara kama hayo.


"Kama hoja ni umeya, huwezi kudai unayoamini imeporwa kwa maandamano, haki inapatikana mahakamani.

Sasa Mimi (Makamba) nawapa pole walioathirika na maandamano hayo
lakini pia nalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Gari la katibu wangu wa Mkoa limevunja vioo na ofisi yetu imeharibiwa vibaya," alisema Makamba mwisho

Source:
Mwananchi

Huyu mzee kalaaniwa watu wamepoteza maisha yeye anasikitikia mali zilizoharibika.Upuuzi tu.
 
Huyu Makamba aache upuuzi wake na sasa tunataka atuambie vifungu vya Kuruani maana anakimbilia Biblia ya wakristu kwanini?

Hapa haiwezeani kwa sisi kumwamini Makamba na siyo haki yake kutumia vibaya vitabu vitakatifu.

Nashangaa viongozi wa dini wanaangalia tu waumini wao wanateketezwa na serikali dhalimu ya JK
 
atuambie pia Biblia inatuambia nini kwa Mwalimu wa shule ya Msingi ambaye anakutwa na tuhuma za kubaka au kulawiti mwanafunzi.....
 
Huyu Makamba aache upuuzi wake na sasa tunataka atuambie vifungu vya Kuruani maana anakimbilia Biblia ya wakristu kwanini?

Hapa haiwezeani kwa sisi kumwamini Makamba na siyo haki yake kutumia vibaya vitabu vitakatifu.

Nashangaa viongozi wa dini wanaangalia tu waumini wao wanateketezwa na serikali dhalimu ya JK


anatumia biblia kwa sababu ni rahisi kwa chadema kuelewa, si umeona hata wote walioshitakiwa ni waumini zaidi wa kitabu hicho
 
anatumia biblia kwa sababu ni rahisi kwa chadema kuelewa, si umeona hata wote walioshitakiwa ni waumini zaidi wa kitabu hicho
Kama nimesoma vizuri kuna waislamu na mpagani pia. Je wale wapemba waliokimbia 2001 kwenda Uingereza na nchi zingine za Ulaya kulikuwa na Wakristu kutoka Pemba?

 
Asante mkuu nimekuelewa, huyu mzee kazeeka vibaya


Sayansi inatuambia uzee huambatana na upotevu wa kumbukumbu pamoja labda na concentration kidogo.Ubongo huongezeka kidogo, lakini IQ inabaki palepale. Sasa ukichanganya na life experience kubwa ndio maana wazee wengi hubaki kama chachu ya kupata mawaidha na ushauri na si vinginevyo.
 
Huyu Makamba aache upuuzi wake na sasa tunataka atuambie vifungu vya Kuruani maana anakimbilia Biblia ya wakristu kwanini?

Hapa haiwezeani kwa sisi kumwamini Makamba na siyo haki yake kutumia vibaya vitabu vitakatifu.

Nashangaa viongozi wa dini wanaangalia tu waumini wao wanateketezwa na serikali dhalimu ya JK
Jamani kwani mlitegemea la maana kutoka kwa mzee wa pumba?
 
Yangekuwa maandamano ya kumuunga mkono JK au ya CCM wala usingeona Polisi wakiingilia .. Nchi imeoza sana kwa akili kama za akina Makamba. Polisi wanaonyesha uwezo katika kuua wasio na hatia na wasio na siraha, ila linapokuja suala la Ujambazi wanasema hawana vifaa. Shame on the rotten Government! Hii pia ni shida ya kuwa Polisi wenye Elimu ndogo.
 
Mh. Makamba ( Katibu Mkuu wa CCM) naomba unijibu hata kupitia kwa January Makamba ambaye huwa humu JF kwa jina jingine.

Ulisema CHADEMA hawakutii amri halali.
1. Je ukiwa na barua ya kukuruhusu kuandamana, kisha pakatokea taarifa kwa mdomo kuwa umezuiwa kuandamana bila maandishi. Utatii amri ipi?

2. Kama polisi walikuwa na taarifa za kiitelijensia kuwa kuna shida itatokea na ndio maana wakawa wengi mno hata kutoka mikoa mingine kuzuia maandamano. Kwa nini wingi huo usitumike kuzuia yaliyokusudiwa katika taarifa hizo za kiitelijensia?

3. Unadhani kama kweli kuna taarifa za kweli zilizoonyesha kusudio lolote baya, je kwa nguvu iliyotumika na maisha yaliyoondolewa na waliojeruhiwa ( waliokuwamo na wasiokuwamo) imesaidia kugeuza ubaya wa yeyote aliyekusudia mabaya au mmewaongezea mashabaki hao waliokusudia mabaya?( kama kweli wapo waliokusudia mabaya)

4. Ni kwa nini vurugu haikutokea kabla ya polisi kuanza kuzuia maandamano?

5. Hata kama umezuiliwa kuandamana lakini ukapewa kibali cha mkutano wa hadhara. Je watu waende kwenye huo mkutano kwa Helkopta ili wasikamatwe kwa kuandamana? Je unaweza kuwawekea watu muda maalum wa kwenda kwenye mkutano mtu moja mmoja ili wasiende kwa pamoja au kwa makundi?

6. Kama kinacholindwa ni UMEYA na siyo wananchi wanaohudumiwa na meya huyo, ukishawaua utawasimamiaje?

7. Je CCM inaiheshimu mamlaka iliyo kuu (katiba) ambayo ndiyo mamlaka kuu kuliko zote? JE VIONGOZI WANAJUA KUWA MAMLAKA KUU NI KATIBA NA SIO WAO?
Ulisema kuwa unalilia mali za CCM zilizoharibiwa. Kwa ushauri wangu sio vizuri wakati kuna watu wamepoteza maisha uanze kuzungumzia mali badala ya maisha yaliyopotea. Je CHADEMA wazungumzie Gari lililovunjwa vioo na polisi katika wakati huu?
TAFADHALI NIJIBU.
 
Back
Top Bottom