Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
January Usikate Tamaa. Wewe ni mpiganaji . Wewe ndo dawa ya mafisadi Wizara hiyo imeoza kwa ufisadi! Pigana hadi kieleweke |
Patricia Kimelemeta KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini, imeitaka Wizara ya Nishati na Madini, kuwasilisha mikataba ya kampuni za Mantra na Urinex, zinazojihusisha na uchimbaji wa madini ya Uraniam, ili kuliwezesha Bunge kujiridhisha juu uhalali wao katika kufanya shughuli hizo. Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba, ambaye alisema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa madini yenyewe katika dunia ya sasa.Alisema kukaguliwa kwa mikabata hiyo, kutasaidia kubaini uhalali na uwezo wa kampuni hizo katika kufanya shughuli hizo. "Kuna kampuni mbili za uchimbaji wa madini ya Uranium hapa nchini, lakini hadi sasa mikabata yake hatujaiona, kwa hiyo tumeitaka wizara kuwasilisha mikataba hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge ili tuweze kuikagua,"alisema Makamba. Alisema Kampuni ya Urinex inachimba madini hayo katika maeneo ya Manyoni, mkoani Singida na Bahi huko Dodoma wakati Kampuni ya Mantra, inachimba Uranium katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania. Alisema Serikali kupitia kamati hiyo inapaswa kuhakikisha kuwa madini yanawanufaisha wananchi kuiwezesha nchi kujiingizia mapato. Alisema madini hayo yanahitajika sana duniani katika shughuli mbalimbali na kwamba kwa msingi huo kama lazima ijue mikabata yote inayohusu uchimbaji wa Uranium.Alisema kutowasilishwa kwa mikataba ya kampuni hizo, kumeifanya kama yake, kushindwa kujadili suala lolote kuhusu kampuni hizo. |