Makala ya James Mapalala kwenye gazeti la Mwananchi Imenisisimua!

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Dondoo:

1. Ndiye muanzilishi wa Kafu.

2. Nyerere alipoanzisha 'hoja dhaifu' ya Chama kushika hatamu, James Mapalala hakuridhika, alihisi uhuru wa maoni na kukusanyika unakandamizwa. akaanza kuandamwa na 'mikosi' ya mkono wa serekali kumfuata fuata. anasema kuna wakati alitiwaga kizuizini bila kufunguliwa mashitaka akawa anahamiswa selo moja kwenda nyengine. Nyerere na CCM yake walikuwa wanamnyanyasa.

3. anasema alipataga kazi ya walimu naijeria akawa anajiandaa. basi siku moja akiwa kanisani st.peters oysterbay mara akakutana na nyerere akamuuliza 'nasikia unataka kuondoka?', mapalala akasema, 'ndiyo mzee'. nyerere akamuambia 'usiondoke nitakupa kazi nyengine'. akapewa kazi ya kununuwa ngombe. mapalala anasema alifanya kazi ile kwa kishingo upande kwa miaka miwili, baadaye akaikacha...safari ya naijeria ikawa imeota mbawa na akaanza kula msoto.

4. baadaye mfumo wa vyama vingi ukaruhusiwa. akaanzisha chama cha kafu tanzania bara. lakini kumbe na zenji kulikwa na kafu zenji. basi ikabidi waswahili wa pwani wampige kiswahili kuviunganisha vyama viwili hivi ili kiwe chama kimoja chene sura ya kitaifa. ikazaliwa kafu hii unayoijuwa wewe, kafu ngangari jino kwa jino. yeye bwana mapalala akawa mwenyekiti.

5. kwa kuwa chama cha siasa ni NGO, ilibidi waanze kutembeza bakuli kwa wahisani. na kwa ushawishi uleule wa waswahili walewale, ikakubaliwa kwamba bakuli litembezwe kwenye nchi za waarabu. hapo ndo kikawa kimbembe. wale waarabu wakadai safu za uongozi, na walipogunduwa kuwa mwenyekiti wa NGO inayotaka mpunga, Kafu, kwamba mwenyekiti wake ni 'kafiri', waarabu wakasema hakuna hela. 'hatuwezi kuwapa hela wakati chama chenyee kinaongozwa na kafiri'. mapalala mwenyee ndo anasema haya siyo mimi Ng'wanangwa. anao ushahidi. eti yeye ni 'kafiri'.

6. mapalala akapigwa fitna kuanzia ndani ya kafu mpaka nje. waswahili wa pwani wakawa wanamusingizia anakisaliti chama. yeye ni gamba. basi ikafika siku wakaamua kumchinjia baharini. duh! wakampeleka Tanga kwa waswahili wengine. tena ile ishu mzee mapalala anasema ilikuwa inashadadiwa na msajili wa vyama vya siasa wa wakati huo bwana Liundi. mwisho wa mapalala kuiongoza kafu ukawa umefika tamati. akapigwa chini. akalambwa mkono. kafu hao.

hapa nimechuwa dondoo tu jamani. mimi siwezi ku-type kazeti zima. kama kuna mtu ana soft copy ya ile makala aiweke, ila habari ndo hiyo, huyu lipumba amekalia sana udini. kumbe na huyu mtatiro ipo siku tu watamchomowa.

chezea kafu!

Updates (Shukurani kwa Nonda)
=================
James Mapalala:Mwanzilishi wa mageuzi aliyeishia kwenye mikosi

View attachment james_mapalala.jpg
James Mapalala akiwa katika moja ya mabanda anayoishi baada ya nyumba yake kubomolewa kwa amri ya mahakama

HARAKATI za mageuzi nchini zina historia ndefu, zikianza kabla ya uhuru ambapo wa wananchi kupitia vyama na vuguvugu za aina mbalimbali waliungana ili kuwaondoa wakoloni.

Hadi mwaka 1961 chama cha Tanu kilichokuwa kikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere kilishinda uchaguzi na kuunda Serikali.

Vyama vingine vilivyokuwepo ni pamoja na AMNUT, ANC na UTP.Baada ya Mwalimu kuunda Serikali, alifanya mabadiliko kadhaa ambapo mwaka 1965 alifuta mfumo wa vyama vingi na kukifanya chama cha Tanu kushika hatamu za uongozi.

Mbali na kufutwa kwa mfumo huo, pia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa asasi za kiraia ulidhoofishwa huku jumuiya mbalimbali za kiraia zikichukuliwa na kuwa jumuiya za Tanu.

Hata hivyo, hatua hiyo haikuwafurahisha baadhi ya watu akiwemo James Mapalala ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mwalimu.

Mapambano yalipoanza
Akizungumza maisha yake hivi karibuni, Mapalala anasema aliamua kupambana na mfumo huo kutokana na ukandamizwaji wa haki za binadamu uliokuwa ukifanywa na Serikali tangu ngazi za juu hadi chini.

"Nilianza mapambano yangu rasmi mwaka 1968 wakati huo nikiandika makala katika Gazeti la Kiongozi wakati huo nikiwa naishi Tabora. Nilieleza kutoridhishwa na mateso wanayopata wananchi wakati huo ingawa kwa kweli Mwalimu Nyerere alikuwa na nia njema tu," anasema Mapalala na kuongeza:

"Viongozi wa vijiji wakati ule walikuwa wakitesa wananchi na mimi niliandika kila kilichotokea."

Kutokana na hali hiyo Mapalala alijikuta matatizoni na kufungwa jela katika gereza la Uyui na huo ulikuwa ni mkasa wa kwanza.
"Mkuu wa mkoa wakati huo akiitwa Makinda ambaye ni baba wa spika wa sasa, Anna Makinda, aliniweka jela.

Nilikaa kwa muda fulani hadi maaskofu na mashehe wa mkoa huo waliponihurumia na kumwandikia barua Mwalimu Nyerere kumwomba nitolewe," anasema.

Anasema ombi hilo lilikubaliwa na Mwalimu Nyerere na hivyo kutolewa.

Hapo alifungua ukurasa mwingine ambapo kutokana na taaluma yake ya ualimu, aliomba na kupata kazi katika Shirika na la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) mwaka 1971.

"Nilitakiwa kwenda kufundisha Nigeria, hivyo nikaenda kuripoti kisha nikarudi ili niichukue familia yangu. Niliporudi, Jumapili moja nikiwa kanisani pale St. Peter, Oysterbay nikakutana na Nyerere… akaniita na kuniuliza, ‘nasikia unataka kuondoka?' nikamjibu ni kweli. Akaniambia nisiondoke kuna kazi atanipa, hivyo niripoti ofisi za Tanu pale Lumumba siku iliyofuata," anasema.

Anasema siku hiyo alipofika ofisini hapo, aliwakuta maofisa wa chama ambao walimpangia kazi ya kununua na kuuza ng'ombe kutoka mikoani.

"Niliifanya kazi ile kwa shingo upande kwa miaka miwili kisha nikaiacha. Hapo tena ile kazi yangu ya Unesco ikaota mbawa," anasema.

Anasema tangu wakati huo alianza kufanya kazi zake binafsi ikiwa ni pamoja na kuwa mkandarasi wa majengo ambapo anasema aliwahi kupata zabuni ya kujenga maghorofa ya bandari.

Hata hivyo anasema ilipofika mwaka 1983, mapambano yake yakaanza tena ambapo wakati huo kulikuwa na mkutano wa wanasheria jijini Dar es Salaam ambao pia walimkaribisha.

"Wakati huo kulikuwa na wanasheria kutoka katika Chama cha Tanganyika Law Society walinialika kwenye mkutano uliokuwa ukizungumzia matatizo ya demokrasia nchini. Walizungumzia matatizo ya mfumo wa chama kimoja, lakini hawakutoa suluhisho. Mimi nilipendekeza uanzishwe mfumo wa vyama vingi nchini," anasema Mapalala.

Hata hivyo, pendekezo hilo halikutiliwa maanani hadi mwaka 1984 wakati Chama Cha Mapinduzi kikiwa na mkutano mkuu ambapo Mapalala alifanya tena ‘uchokozi' wake.

"Mwaka 1984 nilimwandikia barua Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano mkuu wa CCM nikimtaka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. Hapo ndipo matatizo yakaanza kwani niliwekwa kizuizini. Nilikuwa nikihamishwa kutoka kituo kimoja cha polisi hadi kingine kwa karibu mwaka mmoja. Lakini zikufunguliwa kesi yoyote," anasema.

Anaongeza kuwa mwaka 1986, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Muhidin Kimario alimkamata na kumfunga minyororo na kumpeleka kizuizini mkoani Lindi ambako alikaa hadi mwaka 1990 na wakati huo nilikuwa nikihamishiwa kisiwani Mafia.

Licha ya matatizo yote hayo Mapalala anasema hakukata tamaa na mawazo yake ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi.

"Baada ya kutoka kizuizini, nilirudi tena na mawazo ya kuanzisha chama cha siasa. Nilikuwa na wenzangu ambapo tulianzisha chama wakati hakukuwa na sheria ya vyama vingi," anasema na kuongeza:"Hatukuogopa, tulikwenda kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, wakati huo Augustine Mrema na kumweleza haja yetu hiyo. Mrema alikuwa mkali sana akatufokea na kutufukuza."

Baada ya kuona hivyo anasema waliamua kuandamana wakidai haki ya kuanzisha chama cha siasa,"Tulikuwa watu 35 hivi, wakati maandamano yetu yanaanza. Tulipokuwa tukikaribia Kariakoo, watu waliongezeka na kufika hadi 1,000. Polisi wakaingilia kati na kuwakamata watu 25, mimi nikakimbilia Ubalozi wa Sweden kujificha."

Anaendelea kusema kuwa, wale wanachama waliokamatwa na kupelekwa mahabusu waligoma kula kwa siku kadhaa na kuanza kuitisha Serikali.

"Ilibidi Serikali ije kuniomba niwasihi wale chakula. Ikabidi kitolewe chakula kizuri tena kutoka Kilimanjaro Hotel na kupelekwa gerezani na kuwabembeleza kula," anasema.
Wakati mivutano hiyo ikiendelea, tayari kulishaanza kujitokeza mabadiliko ya kisasa na kiuchumi ulimwenguni ambapo mfumo wa ukomunisti ulianza kuanguka.

Kuanzisha, kufukuzwa CUF
Baada ya misukosuko ndipo walianzisha chama chao rasmi kikitwa Chama cha Wananchi (CUF) mwaka 1991.

Baada ya Serikali kupitisha sheria ya vyama vingi mwaka 1992, Mapalala anasema wanaharakati wengine wa mageuzi walikutana ukumbi wa Diamond Jubilee mwaka huo na kuanzisha chama cha NCCR-Mageuzi.

Hata hivyo, anasema mwaka huo kulikuwa na chama kingine huko Zanzibar cha ZUF (Zanzibar United Front) ambacho kilitaka kuunganisha nguvu na chama cha bara ili kiwe cha kitaifa.
"Walipokuja bara kuangalia chama chenye nguvu, wakaridhika na chama chetu na kuomba tuungane. Halmashauri kuu za vyama vyetu zikakaa kujadili suala hilo na hatimaye kukubaliana. Mwaka 1993 niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF iliyoungana," anasema.

Baada ya hapo anasema alifanya ziara katika mikoa karibu yote ya bara na Zanzibar kwa ajili ya kukitangaza chama hicho.

Hata hivyo, bahati haikuwa yake, anasema ilipofika mwaka 1994 mambo yakabadilika kwani wenzake hasa viongozi wa Zanzibar wakamgeuka na kuanza kumtuhumu kuwa anakisaliti chama.
Lakini mwenyewe anasema ilikuwa ni sababu za kidini pamoja na mkono wa Serikali uliokuwa ukiendelea kumwandama.

"Nilifukuzwa CUF kwa sababu za kidini tu. Ilikuwa mwaka 1994 baada ya kukijenga chama hicho nikashangaa mambo yamebadilika na viongozi wenzangu wamenigeuka. Wakawa wananishutumu kuwa natumiwa na CCM, mara nimechana bendera za chama, na tuhuma nyingi tu.

Lakini nilipata hadi nyaraka zilizothibitisha sababu za udini," anasema na kuongeza:
"Wakati huo CUF ilikuwa ikifadhiliwa na nchi za kiarabu, kwa hiyo wakasema ‘mtatakaje msaada wakati chama kinaongozwa na kafiri?' Ndipo vituko vikaanza. Lakini hata Serikali pia ilichangia, nakumbuka siku ya mkutano wa kunifukuza kule Tanga, Msajili wa vyama vya siasa wakati huo, George Liundi alikuwepo hadi saa tisa za usiku akishadadia kufukuzwa kwangu."

Baada ya kufukuzwa Mapalala akaanza upya tena mikakati ya kuanzisha chama kingine. Hata hivyo ilimchukua muda mrefu hadi mwaka 2003 ambapo alianzisha Chama cha Haki na Ustawi alichonacho hadi sasa.

Tangu alipokianzisha alifanikiwa kupata diwani mmoja tu mkoani Mara mwaka 2005 ambaye hata hivyo hakuendelea baada ya kumaliza miaka yake mitano.

Mapalala anazungumzia pia tukio la kunyang'anywa nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Morocco jijini Dar es Salaam kwa amri ya mahakama mwaka 2010, na kulihusisha na misukosuko aliyoipata katika harakati za kuleta mageuzi nchini.

"Hapa unapoona ninaishi kwenye mabanda ya ng'ombe, baada ya nyumba yangu kubomolewa kwa amri ya mahakama, yaani ni misukosuko tu. Chama changu kinanitegemea kifedha lakini kwa hali hii inaniwia vigumu kukisaidia," anasema.

Anazungumziaje upinzani wa sasa?
Akizungumzia vyama vya upinzani vya sasa, Mapalala anasema kuwa vimejikita zaidi kwenye kutafuta madaraka badala ya kueleza sera zao kwa wananchi.

"Tofauti kati ya upinzani tuliokuwa tukiupigania miaka ile na wa sasa, ni watu kuwa na mawazo ya kwenda Ikulu tu bila kusema watawafanyia nini wananchi baada ya kufika huko. Hata kwenye chama tawala, CCM, hali ni hiyo hiyo, watu wanalilia tu Ikulu. Sisi tunasisitiza sera tu… sera nzuri ndiyo zitakazouza chama, chema chajiuza kibaya chajitembeza," anasema.

Last edited by a moderator:
Duh ndiyo maana mwenyekiti na katibu mkuu lazima watoke kuleeeee ha ha ha ha.
 
Mtatiro amewekwa pale kama puppet tu ili kuhadaa watu. Alafu sikumbuki kama hawa walishawahi kukanusha madai ya Mumewe (ccm) kuwa CUF ni chama cha waislamu.
 
Jaman spendagi kuchanganya chama na dini, tunapoteza malengo yetu ya kugombana kumwondoa nduli ccm
 
Hakika niliipenda cuf ya mapalala sio hii ya leo. Sikubahatika kumuona enzi hizo nilikua nikimsikia tu.
 
wewe mtu sijui ni mswahili wa wapi? maana kiswahuli chako kina majeraha mengi!
 
Mtatiro will never grow to become the Chairman of CUF unless......................
 
hiyo mbona tunajua..cuf ni chama cha waarabu ndio maana kinataka zanzibar ijitoe kwenye muungano ili waarabu wachukue kile kisiwa kiwe cha kwao....wazenji halisia hawajui hiyo wanapiga makelele kila siku wanataka uhuru wao hawajui kua muungano ukivunjika haimaanishi kua watakua na uhuru bali ule ukoloni wa usultani utarudi kitakua kisiwa cha waarabu ndio maana cuf hakuna mkristo kwenye uongozi wao na nimeshasema tena na narudia tena 2015 tuwafute kabisa cuf kwenye ramani ya tanganyika..wasipate mbunge hata mmoja popote pale...
 
wewe mtu sijui ni mswahili wa wapi? maana kiswahuli chako kina majeraha mengi!

Na wewe je? sentensi moja ya pili jeraha. Ukiandika sentensi 10 itakuwaje? Muhimu tusipende kuhama kwenye mada kuu. Thread hii imetukumbusha historia ya CUF na maumivu yaliyompata muasisi wake.
 
...

5. kwa kuwa chama cha siasa ni NGO, ilibidi waanze kutembeza bakuli kwa wahisani. na kwa ushawishi uleule wa waswahili walewale, ikakubaliwa kwamba bakuli litembezwe kwenye nchi za waarabu. hapo ndo kikawa kimbembe. wale waarabu wakadai safu za uongozi, na walipogunduwa kuwa mwenyekiti wa NGO inayotaka mpunga, Kafu, kwamba mwenyekiti wake ni 'kafiri', waarabu wakasema hakuna hela. 'hatuwezi kuwapa hela wakati chama chenyee kinaongozwa na kafiri'. mapalala mwenyee ndo anasema haya siyo mimi Ng'wanangwa. anao ushahidi. eti yeye ni 'kafiri'.

...

Asante sana Mzee Mapalala kwa kutufumbua macho na pole sana kwa madhila yaliyokupata katika maisha yako ya kisiasa. Eti hiki ndicho chama kinachotaka tukikabidhi nchi! Ha ha ha ha ha!
 
Na wewe je? sentensi moja ya pili jeraha. Ukiandika sentensi 10 itakuwaje? Muhimu tusipende kuhama kwenye mada kuu. Thread hii imetukumbusha historia ya CUF na maumivu yaliyompata muasisi wake.
Ni kweli,lakini mmh ile imezidi si typo error bali ndiyo style yake!thanks anyway!
 
Dondoo:

1. Ndiye muanzilishi wa Kafu.

2. Nyerere alipoanzisha 'hoja dhaifu' ya Chama kushika hatamu, James Mapalala hakuridhika, alihisi uhuru wa maoni na kukusanyika unakandamizwa. akaanza kuandamwa na 'mikosi' ya mkono wa serekali kumfuata fuata. anasema kuna wakati alitiwaga kizuizini bila kufunguliwa mashitaka akawa anahamiswa selo moja kwenda nyengine. Nyerere na CCM yake walikuwa wanamnyanyasa.

3. anasema alipataga kazi ya walimu naijeria akawa anajiandaa. basi siku moja akiwa kanisani st.peters oysterbay mara akakutana na nyerere akamuuliza 'nasikia unataka kuondoka?', mapalala akasema, 'ndiyo mzee'. nyerere akamuambia 'usiondoke nitakupa kazi nyengine'. akapewa kazi ya kununuwa ngombe. mapalala anasema alifanya kazi ile kwa kishingo upande kwa miaka miwili, baadaye akaikacha...safari ya naijeria ikawa imeota mbawa na akaanza kula msoto.

4. baadaye mfumo wa vyama vingi ukaruhusiwa. akaanzisha chama cha kafu tanzania bara. lakini kumbe na zenji kulikwa na kafu zenji. basi ikabidi waswahili wa pwani wampige kiswahili kuviunganisha vyama viwili hivi ili kiwe chama kimoja chene sura ya kitaifa. ikazaliwa kafu hii unayoijuwa wewe, kafu ngangari jino kwa jino. yeye bwana mapalala akawa mwenyekiti.

5. kwa kuwa chama cha siasa ni NGO, ilibidi waanze kutembeza bakuli kwa wahisani. na kwa ushawishi uleule wa waswahili walewale, ikakubaliwa kwamba bakuli litembezwe kwenye nchi za waarabu. hapo ndo kikawa kimbembe. wale waarabu wakadai safu za uongozi, na walipogunduwa kuwa mwenyekiti wa NGO inayotaka mpunga, Kafu, kwamba mwenyekiti wake ni 'kafiri', waarabu wakasema hakuna hela. 'hatuwezi kuwapa hela wakati chama chenyee kinaongozwa na kafiri'. mapalala mwenyee ndo anasema haya siyo mimi Ng'wanangwa. anao ushahidi. eti yeye ni 'kafiri'.

6. mapalala akapigwa fitna kuanzia ndani ya kafu mpaka nje. waswahili wa pwani wakawa wanamusingizia anakisaliti chama. yeye ni gamba. basi ikafika siku wakaamua kumchinjia baharini. duh! wakampeleka Tanga kwa waswahili wengine. tena ile ishu mzee mapalala anasema ilikuwa inashadadiwa na msajili wa vyama vya siasa wa wakati huo bwana Liundi. mwisho wa mapalala kuiongoza kafu ukawa umefika tamati. akapigwa chini. akalambwa mkono. kafu hao.

hapa nimechuwa dondoo tu jamani. mimi siwezi ku-type kazeti zima. kama kuna mtu ana soft copy ya ile makala aiweke, ila habari ndo hiyo, huyu lipumba amekalia sana udini. kumbe na huyu mtatiro ipo siku tu watamchomowa.

chezea kafu!

Sorry unaumri gani?
 
Hakika niliipenda cuf ya mapalala sio hii ya leo. Sikubahatika kumuona enzi hizo nilikua nikimsikia tu.
Mapalala ilikuwa mashine hata uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa Ubunge 1994 kule Igunga inasemekana alimshinda Rostam lakini kama kawaida yao CCM walichakachua.
 
hapa nimechuwa dondoo tu jamani. mimi siwezi ku-type kazeti zima. kama kuna mtu ana soft copy ya ile makala aiweke, ila habari ndo hiyo, huyu lipumba amekalia sana udini. kumbe na huyu mtatiro ipo siku tu watamchomowa.

chezea kafu!

Hilo gazeti halina webpage?

Au ni toleo la mwaka gani?

Ng'wanangwa...weka wazi ikiwezekana,wewe ni mwanachama wa chama chochote cha siasa au ni mpenzi wa chama cha siasa? Hiyo nyekundu ndio imenifanya niulize hili suali.
 
Back
Top Bottom