Makada Wa CCM wanaosimamia kuandikisha wapiga kura Kyerwa wanavunja Sheria

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
MAKADA WA CCM WANAOSIMAMIA ZOEZI LA KUANDIKISHA WAPIGA KURA KYERWA WANAVUNJA SHERIA NA HAKI ZA WANANCHI WAKIZUIA WAPIGA KURA WASIANDIKISHWE NA KUPATA SHAHADA

CCM Kyerwa inadaiwa na wananchi kuwa imepandikiza wasimamizi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga ili kuzuia wananchi ambao sio wapiga kura wa chama wasiandikishwe na kupata shahada za kupigia kura.

Zoezi la uandikishaji linaendelea katika kata za Kibingo, Murongo, Bugomora, Kibare na Businde.

Jambo hili limekuwa kero kubwa huko Kyerwa jambo linaloweza kusababisha upotevu wa amani.

Mathalani Bw. Emmanuel Simon (0758334651) alizaliwa katika kijiji cha Murongo mwaka 1968 wazazi wake wote wakiwa ni raia wa Tanzania.

Baba na mama yake Bw.Simon Kabwa walizaliwa wakati huo Tanganyika na kubatizwa katika kanisa la Lutherani Murongo 1953 na vyeti vya ubatizo vipo.

Mzee Simon Kabwa baba yake Emmanuel anashahada za kupigia kura toka 1965 na chaguzi nyingine za kugombea Mwl. Nyerere alipiga kura.

Emmanuel Simon alisoma katika shule ya Msingi Murongo na kuishi katika kijiji hicho hadi leo.

Mwaka 2004 na 2009 aligombea kwa tiketi ya CCM katika kitongoji cha Mukagando na kuongoza kijiji hicho akiwa M/kiti wa Kitongoji.

Baadae mwaka 2013 alihama CCM na kujiunga Chadema. Aligombea kwa tiketi ya Chadema akawekewa pingamizi kuwa sio. Rufaa ya pingamizi haikusikilizwa na Msimamizi wa serikali za mitaa Kyerwa 2014. Rufaa zote za Chadema zilizokuwa zinaonyesha zikiondolewa CCM haitashinda, hazikuondolewa. Jambo hilo lilisababisha Chadema kupoteza wagombea wake kwa 70% katika uchahuzi huo wa Serikali za Mitaa.

Kwahiyo wapiga kura takribani 10 wana Chadema walio katika familia ya Emmanuel Simon wamenyimwa haki ya kuandikishwa na kuwa wapiga kura Oct.2015.

Katika mchakato wa kuandikisha wapiga kura, wale wote waliowekewa pingamizi za kugushi, na katika zoezi la kuandikisha wapiga kura orodha ya wananchi zaidi 700 imewebandikwa katika vituo vya kuandikisha katika kata ya Murongo tu.

Hali hii inasababishwa na uongozi wa CCM Kyerwa kuondoa wapiga kuwa inaojua kuwa sio wapiga kura wake ili wakose haki ya kupiga kura ili kuhifadhi nafasi za kisiasa za makada wake.

Haya yote yanafanyika kinyume cha sheria na kwa kuvunja sheria.

Mfano ndani ya familia moja, baadhi ya wanafamilia ambao ni wana CCM wanaandikishwa ila ambao ni Chadema katika familia hiyo hiyo wanazuiliwa kuandikishwa kuwa sio raia.

Kuna wananchi wengi wananyimwa haki hiyo ya kupiga kura kwa kuzuiwa wasijiandikishe na makada/viongozi wa serikali au CCM wakitishia wananchi, na mwananchi akijitahidi kudai haki yake anakamatwa na kupelekwa polisi kwa kesi ya kusababisha vurugu katika kituo cha kuandikisha wapiga kura.

Wananchi wengi wanaChadema wasiojua kijieleza, kusoma na kuandika wanatishiwa na kunyimwa haki ya kuandikishwa na kuelezwa kuwa wakisababisha vurugu watapelekwa polisi.

Wananchi wengi huko vijijini kwa kuogopa sana polisi wakiwekewa vitisho hurudi nyumbani na kuacha kabisa kurudi vituoni kujiandikisha.

Kinachofanyika Kyerwa ni uhalifu wa kisiasa unaotekerezwa na viongozi wa ccm wakisaidiana na makada wa ccm walio ndani ya serikali.

Uovu huo unalindwa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa na mamlaka zote za serikali.

Jambo hili lisiposhughulikiwa linaweza kusababisha upotevu wa amani na kuharibu kabisa mchakato wa uchaguzi kutokana na wapiga kura kunyimwa haki yao ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Hali ilivyo inaonyesha kuna uwezekano wa zaidi ya 40% ya wapiga kura Kyerwa hawatapata shahada za kupiga kura iwapo juhudi zisipofanyika kuhifadhi haki ya kupiga kura ya wananchi wa Kyerwa.

Uchafu huo wote unaotekerezwa na serikali ya ccm Kyerwa ni kutokana na watawala kuogopa maamuzi ya wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Wanalinda nafasi za madiwani wanaotuhumiwa kulinda masilahi ya mafisadi wa ccm Kyerwa na kusaliti wananchi.

Uongozi wa serikali na ccm umekuwa ukilinda na kuhifadhi uovu na uvunjifu wa sheria ili tu kulinda vigogo wachache sana waliojifanya miungu watu.

Watu wanaotuhumiwa kusimamia kushinikiza kupindisha au kuvunja sheria ili kulinda masilahi yao binafsi ni wafuatao:

1. Diwani wa Kata ya Rukuraijo Bw. Kashunju Runyogote(M/kiti wa Halmashauri-Kyerwa)

2. Bw. Daniel Damian (M-NEC-CCM Kyerwa)

3. Bw. Eustace Katagira (Mbunge Kyerwa-CCM)

Hao watatu wanakundi kubwa nyuma yao linajineemesha kwa uvunjaji sheria na ukandamizaji mkubwa sana wa haki za binadamu wanaodaiwa kuutenda kwa masilahi yao binafsi.

Kinachoendelea huko Kyerwa ni uonevu mkubwa sana unaendelea kupanua wigo wa umasikini kushamiri huko Kyerwa, vifo vya watoto, akina mama, wazee, vijana kukosa ajira, sekta za uchumi kudidimia kabisa, mateso katika vyombo vya dola kama polisi ambako badala ya haki kulindwa inaibwa na kunyingwa kabisa.

Haya yote yanafanyika kwa matumizi ya pesa za Watanzania kulinda masilahi ya watu wachache wezi na madikteta katika jamii ya watu masikink sana ya Kyerwa.

WITO KWA ASASI ZA KIRAIA ZA KULINDA HAKI ZA BINADAMU
cc:
TAWLA
LHRC
TAMWA n.k

👉Mosi, kwa niaba ya wananchi wengi sana wa Kyerwa wanaosikitishwa na uharamia dhidi ya haki za binadamu huko Kyerwa ninaomba mfuatilie na kusaidiana na vyama vya uoinzani kudai haki ya wananchi kushiriki kupiga kura.

👉Pili, walioshiriki kuvunja sheria na kuzorotesha mchakato wa uandikishaji wa wapiga kura kwa masilahi yao binafsi wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za Uchaguzi.

👉Naomba kuwekwe wawakirishi wa asasi zenu za kulinda haki za binadamu huko Kyerwa na mikoa ya pembezoni ambako kuna wanasiasa wanaokika sheria na kupotosha ukweli kuhusu uraia wakitumia nafasi zao ndani ya serikali na chama tawala CCM.

👉Ndugu Watanzania wenzangu mnaofanyakazi katika asasi hizo zinazojihusha na kulinda/kudai haki za raia hasa waliopembezoni (Marginalised citizens) mchango wenu muhimu naomba na kushauri ujitokeze katika kipindi cha uandikishaji wa wapiga kura katika mikoa ya mipakani.

Naamini mnajua na kukumbuka zoezi la Operesheni tokomeza majangiri lilivyogeuzwa na kufanywa kuwa operesheni tokomeza wananchi na viongozi wa chama tawala.

Naomba sana, msaada wenu katika uchaguzi uonyesheni katika hatua ya uandikishaji wa wapiga kura kuliko hatua ya Uchaguzi wenye. Yaani bajeti kubwa iwe katika hatua hii.

Kyerwa tunawahitaji sana. Nawaombeni mtume wawakirishi huko wakiwa na kamera na "recorders" wamulike madudu ya viongozi waliowekwa mfuko na wanasiasa wenye roho za kinyama, wezi, na wasio na hofu na Mwenyezi Mungu.

Naomba ombi langu lipokelewe na kufanyiwa kazi.

👇👇👇👇👇👇👇
Swali kwa Tume ya Uchaguzi.

Kama Tume ya Uchaguzi ni Huru, kwa nini inakubali kuwekwa mfukoni na makada hawa wa ccm na kuwaacha wavunje sheria na kuzuia wananchi wasishiriki kuchagua viongozi wao?

Kwa nini Tume isiwe na wawakirishi wa Makao makuu ya Tume katika maeneo ya mipakani hasa kanda ya Ziwa Magharibi wanaosikiriza kero hizi za wanasiasa wa CCM ambao ndio wawakirishi wa Tume wanaoweka "neutrality" kando na kubaki kuwa mawakara wa ccm badala ya Tume?

HATUA AMBAZO CHADEMA INAZICHUKUA

CHADEMA Kyerwa imeishanza kuorodhesha wananchi wote ambao wamenyimwa haki ya kushiriki uchaguzi kwa vigezo visivyo na ukweli ili kutafuta haki yao katika Tume ya Uchaguzi Tanzania kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

Jitihada zinazofanywa na chama ni kubwa ila chama kinaelemewa kutokana na kero kuwa nyingi kuliko uwezo wa maandalizi ya ofisi ya chama Wilaya ya Kyerwa.

Nahitimisha kwa kuwasihi wana CCM Kyerwa wajue nchi hii ni ya Watanzania.

Uhasama mnaoukubali kuujenga kwa faida ya wanasiasa wachache wezi utasababisha ukosefu wa amani na kupotea kwa udugu na mshikamano wa wana Kyerwa na Watanzania kwa ujumla.

Nawaomba, kabla ya kuweka siasa katika hatua ya kupata viongozi bora kwanini tuweke siasa katika mchakato muhimu ya kutafuta maendeleo ya nchi kwa masilahi ya watu wachache warafi wa mali na madaraka?

Nawasihi tujitahidi kujipambanua na kuelewa kuwa hatuwezi kuondoa umasikini katika jamii yetu bila kubadili uongozi mbaya na kuweka uongozi bora.

Na hatuwezi kufanikisha hilo kwa kukumbatia watu wachache waliojifanya miungu wanaoibia wananchi masikini na kuwadanganya vibaraka wake kwa vipesa vinavyopelekea kuwa kikwakwazo cha maendeleo Kyerwa.

Mwisho naomba Chadema Kyerwa wakitoa ushahidi na maelezo yanayoridhisha kwa Tume kuondoa kasoro za wanasiasa wa chama tawala kuharibu kabisa zoezi la kuandikisha wapiga kura, na IWAPO Tume isipochukua hatua sahihi na kwa wakati, Chama kwa ushirikiano asasi za kulinda haki za binadamu waifungulie Tume ya Uchaguzi mashitaka ya kushiriki kuviunja sheria za uchaguzi na haki ya Watanzania kushiriki uchaguzi kwa masilahi ya chama tawala ili mbivu na mbichi zieleweke mapema kabla ya Octoba 25, 2015.

Chanzo: Solomon Michael Kambarangwe
26/05/2015
 
Mungu akaufanya moyo wa WATawala kuwa mgumu ili adhirishe utukufu wake ccm imekataliwa kote duniani na mbinguni sasa awana chaguo lingine zaidi ya rafu hizi.
 
Last edited by a moderator:
Mungu akaufanya moyo wa WATawala kuwa mgumu ili adhirishe utukufu wake ccm imekataliwa kote duniani na mbinguni sasa awana chaguo lingine zaidi ya rafu hizi.
Tukipa tena ccm nchi inatakiwa tupimwe akili
 
Last edited by a moderator:
kwa huu ufedhuri wanaoufanya mbunge, dan na kinyogoli basi muanze kutarget vitu vyao viaribiwe ili huu ushenzi ukome. dawa ya moto ni moti. upuuz huu ulifanyika uchaguz serikali za mitaa sasa apa msikubali upuuz huu. wale watu wa bushangaro waliomkatia migomba mkiti ccm wilaya, wameenda mahakamani wakashinda. msilale huu ni wakati wa kushughulikia nduli ccmx
 
Back
Top Bottom