Majukumu Maalumu ya kesho Juni 9, 2023, Siku moja kabla ya Bunge Kuridhia au Kutoridhia Watanzania kuuzwa Uarabuni

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
1. WATANZANIA
Watanzania wote katika kila Jimbo wahakikishe wanampigia simu Mbunge wao wakimkanya kuhusu kuridhia mkataba ovu wa kuwauza Watanganyika Uarabuni.

2. ASASI na TAASISI MBALIMBALI
Kila asasi au Taasisi ya kiraia, ihakikishe inatoa tamko kali la kupinga uidhinishwaji wa mkataba hatari kama huu kuwahi kutokea.

3. WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU
Wahakikishe wanapiga kelele kwa nguvu zote kupinga jambo hili la hatari.

4. VIONGOZI WA DINI ZOTE (TEC, CCT, BAKWATA)
Wahakikishe wanatoa tamko kali la kupinga jambo hili la hatari.

Kama watakaa kimya bila kutoa tamko la kupinga jambo hili la hatari watakuwa wamepoteza kabisa sifa ya kuwa viongozi. Maana huwezi kuwa Kiongozi wa dini halafu maovu yanatawala wewe umekaa kimya tu bila kukemea huku unasubiri sadaka za waumini wako.

Binafsi kama viongozi wa Dini hawatatoa tamko lolote, nimeapa kutotoa ZAKA wala SADAKA Kanisani siku zote za maisha yangu.

Majukumu maalumu ya kesho kutwa 10.06.2023.
1. WABUNGE
Kila Mbunge ahakikishe anapinga kwa nguvu zake zote mkataba huu hatari tena bila kumung'unya maneno.

2. SPIKA
Ahakikishe anatoa nafasi kwa Wabunge kujadili kwa kina mkataba huu na kutolea maamuzi sahihi.

3. WATANZANIA
Kila Mtanzania ahakikishe anamfuatilia Mbunge wake na kunukuu maneno yote atakayosema katika kujadili mkataba huu hatari.

Kwa ujumla kila Mtanzania awaye yote na mwenye cheo chochote kile au nafasi yoyote ile aliyonayo katika Nchi hii, ahakikishe anatumia vema nafasi hiyo kupinga jambo hili la hatari.
 
We tafuta ugali kwa ajili yako na familia yako, nchi utakufa na kuiacha.
 
Back
Top Bottom