Majizo alikuwa fundi cherehani wa nguo za wagosi wa kaya

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
DJ Majay a.k.a Majizo siku hizi ni baron wa tasnia. Utambulisho wake haukomei tena Kwa Fujo DJs Member, E-Masterz CEO, Maisha Club Operator, Media Leader, bali sasa ni Media Magnate.

Majay ndiye owner wa EFM Radio na ETV. He’s mogul nowadays, au sio? Basi, hiyo ndio tafsiri ya “the hustle is real”. Fikiria kutoka fundi cherehani hadi kumiliki vyombo vya habari.

Tena, sio vyombo vya habari just to make up numbers. Vinafanya vizuri sana kwenye tasnia. Give it up for the hustler!

Hiyo wala sio topic. Chukua sentensi “Majay fundi cherehani”, halafu tuiendee mada husika. Mwaka 2002, Diamond Jubilee Hall, Upanga.

Wagosi wa Kaya wamekamilisha albamu ya Ukweli Mtupu, iliyorekodiwa MJ Production, chini ya label “MJ Records”.

Enzi hizo Diamond Jubilee ndio spot la kishujaa. Na kwa vile Wagosi ni mashujaa wa ‘haswahaswa’, ikapitishwa albamu ikazinduliwe kiotani hapo.

Mwanamuziki unapozindua albamu, unakuwa sawa na bwana harusi harusini. Mwonekano unaongeza thamani. Wagosi hilo walilizingatia.

“Sijui nitavaa nini” ni swali la kila mwanamke, ndani ya kila nyumba, pia wanamuziki. Wagosi wa Kaya wakajikuta katikati ya viulizo.

“Kuna fundi cherehani mzuri Kinondoni, anaweza kusababisha,” ndivyo jina la fundi Majay lilipokuja. Baada ya vipimo na michoro, jeans za kijivu, zilishonwa usiku na mchana.

Siku ya uzinduzi, Wagosi waliingia saresare maua. Walipendeza. Yalikuwa masiku ya mwanzo ya ingizo la fasheni kwenye Bongo Flava. Wagosi waliua. Majay did it!

We are casting our minds back, kimuhemuhe kikiielekea siku maalum ya Wagosi kutunukiwa plaque za maisha ya mafanikio kwenye muziki, vilevile kutambua mchango wao katika ukuaji wa Bongo Flava.

Baada ya kazi kubwa waliyoifanya ya kuu-dedicate muziki wao katika shida, changamoto, kero na vijimambo vya maisha ya Watanzania, kivipi Wagosi wasitunukiwe hadhi stahiki ya Bongo Flava Honors?

Shughuli ni Oktoba 27 (kesho), Alliance Francaise, Upanga. Sugu The Jongwe ataongoza karamu. Shoo-shoo kwa live band with Swahili Blues. Legend Boniluv atafundisha kwa nini muziki ni burudani.

Wagosi ni sauti ya Watanzania. Tukawape heshima yao.

1698339235467.jpg
 
WAgosi walitisha sana..walituburudisha sana kwa nyimbo zao zenye kuelimisha..waligusa kila sehemu,wauguzi,walimu,kwwnye mpira nk..wanastahili.
 
Bakhresa aliku fundi viatu pale buguruni kwa mnyamani ndo akashauliwa anunue eka mbili nawazee wakizaramo tazara
 
Bakhresa aliku fundi viatu pale buguruni kwa mnyamani ndo akashauliwa anunue eka mbili nawazee wakizaramo tazara
Haikuwa buguruni..
Alikuwa anatengeneza kobazi zile za ngozi Kariakoo.. Livingston street ambapo Hadi Leo ndo head office ya kampuni zake ...alinunua baadae nyumba zote ...mtaa huo kuanzia Ile aliyopanga Hadi za majirani... including bakery uliyokuwa Kona ya Livingston na Uhuru ilikuwa inaitwa ABC bakery ya wahindi ndo akaanzisha bakery yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom