Majivu ni alama ya nje, tujichunguze ndani

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Ninachowaomba wana JF Wakristu ni kujitahidi katika mfungo huu unaoanza leo kuishi maisha yanayo mpendeza Mungu. Ingawa twapashwa kuishi maisha ya utauwa kila siku, udhaifu wetu hutuvuta kutenda yaliyo mabaya. Tumwombe Roho Mtakatifu, atujalie nguvu ya kupigana na maovu ili jamii inayotuzunguka ione uwepo wa Mungu kupitia kwetu.

La muhimu sio KUFUNGA KULA TU, bali ni kumrudia Mungu katika roho na kweli kwa kusali na kuomba, huku tukiutiisha mwili kwa roho. Tulio na ziada basi tuwasaidie maskini, na hiyo ndiyo funga sahihi.

Na hapa JF katika post zetu tusitukanane, na hasa tusikejeli au kudharau imani za wenzetu.

Nawatakia mfungo mwema.
 
Hivi yale majivu ni ishara ya nini? sie kanisani kwetu hakuna majivu
 
Hivi yale majivu ni ishara ya nini? sie kanisani kwetu hakuna majivu

Ni alama ya nje ya toba. Sio ya lazima na hautendi dhambi yoyote kutoyapaka. Unakumbushwa kuwa BINADAMU NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI. Ni mapokeo ya Wayahudi ya kuonyesha toba kwa nje, mfano walivaa magunia, walijipaka majivu, n.k.

Ikumbukwe kwamba kujipaka majivu pekee sio toba, ila ni alama ya nje tu. Inatakiwa kujikataa kwa ndani na kukumbuka mara kwa mara kuwa wewe mwanadamu ni VUMBI tu mbele ya MUNGU. Soma Zaburi 90.
 
..kweli ni uzuniiii ..kwakifo chake bwan yesuuu...
tutubu na kuziacha njia zetu mbaya..ehh mungubaba tusaidie..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom