Majina ya watoto wa nchi za Magharibi

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,396
Naamini hili jukwaa lina watu wengi wanaofahamu tamaduni za watu wa Ulaya na Marekani.

Inaonekana ni kawaida kwa baadhi ya watu wa Ulaya kuwapa watoto wao majina mawili kwa mkupuo, ambayo hayana uhusiano na jina lake (mzazi).

Mfano, baba anaweza akawa anaitwa James Allen Robert, lakini mtoto wake akamwita David Joshua Robert. Hapo utaona jina pekee lenye uhusiano na la baba yake ni la tatu, ambalo ni jina la babu yake baba yake.

Mwingine anaweza akatia fora kwa kutokutumia kabisa jina lenye uhusiano na familia yake. Labda yeye anaitwa Robert Clement William, lakini mwanaye akamwita Charles Smith Capps.

Lakini pia kuna wale ambao huwa na majina yanayofanana na ya wazazi wao, kinachotofautisha ni Jr na Sr pekee. Hilo lipo hata kwa Wamarekani weusi.

Kuna mtu anaitwa Martin Luther King Jr, baba yake aliitwa Martin Luther King Sr. Jr ni mtoto na Sr ni baba.

Hata aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush, majina yao yalifanana. Na kwa kuwa wote walishawahi kuwa Marais wa Marekani, watu huwatofautisha kwa utambulisho wa Bush mkubwa na Bush mdogo. Nafikiri wengi wanamfahamu George W. Bush. Na baba yake aliitwa pia George Bush.

Watu wa Magharibi wanazingatia nini katika kuwapa watoto wao majina?
 
Hakuna kitu kina nikera bongo kama jina lako... jina la baba... jina la ukoo et ndo jina lako. Tungekuwa huru kuwaita tutakavyo.
Ila mwamba mmoja alimuita mwanae Burito jina la ukoo sijui alitumia principle gani wakati yeye ni nyerere
 
Hakuna kitu kina nikera bongo kama jina lako... jina la baba... jina la ukoo et ndo jina lako. Tungekuwa huru kuwaita tutakavyo.
Ila mwamba mmoja alimuita mwanae Burito jina la ukoo sijui alitumia principle gani wakati yeye ni nyerere
Kuna kosa nisipoufuata huo utaratibu uliozoeleka Tanzania kuwapa wanangu majina?
 
Back
Top Bottom