Majina halisi ya WanaJF waliofariki

Kuna mmoja alikuwa mfanyakazi wa Itv &RadioOne Arusha, na siku za mapumziko ya Xmass na Mwaka mpya akaamua kuondoka na saloon kwenda Dar akafia maeneo ya Same kwa ajali.
Niliweka thread yake hapa majamvini japokuwa tulishindwa kujua ID yake hapa ndani, na yeye ndiye alimshauri Crashwise kujiunga na JF.
RIP ewe member mwaminifu na Mungu akuangazie nuru.
 
Nadhani ni vema kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa wetu waliofariki kama alivyopendekeza PJ kwenye posti moja hivi. Mimi naanza:

1. Juma Kidogo
2. Baruti Mwesiga aka Kandambili
3. Profesa Jwani Mwaikusa
4. Regia Mtema
5.
May God Feed them honey....
 
Kuna mmoja namfahamu tulkuwa tunapga sana stori za jf ingawa hatukufahamiana ID zetu alkuwa anafanya kazi ofisi ya mkuu wa mkoa mtwara anaitwa kedmon mgatta pia alishawahi kuwa kiongozi wa daruso yeye pa1 na kina julius mtatiro
 
bandika la ukweli kama mie nikifa pale radio 1 watatangaza na kila member atajua
masikini mimi ambaye hakuna ajuae jina langu halisi nikifa sijui wana jf wenzangu watajuaje nimekufa?
hata hivyo nitajivunia hata huko niyakapokuwa kuwa nilikuwa member wa forum muhimu kwa jamii ya JF.
and i will tell ma self RIP me.
 
Nadhani ni vema kuwaenzi na kuwakumbuka mashujaa wetu waliofariki kama alivyopendekeza PJ kwenye posti moja hivi. Mimi naanza:

1. Juma Kidogo
2. Baruti Mwesiga aka Kandambili
3. Profesa Jwani Mwaikusa
4. Regia Mtema
5.

Na hii ndio hasara ya kutumia majina feki kwenye jukwaa sensitive kama jf.
 
walale salama wapendwa, mungu atawafufua siku ya mwisho...hivi malaria sugu yuko hai? tusije tukamsahau katika hizi rehema.
 
masikini mimi ambaye hakuna ajuae jina langu halisi nikifa sijui wana jf wenzangu watajuaje nimekufa?
hata hivyo nitajivunia hata huko niyakapokuwa kuwa nilikuwa member wa forum muhimu kwa jamii ya JF.
and i will tell ma self RIP me.
nadhani Mods waweke ka-system ambako sisi tunawapa baadhi ya real identity ila wao wanaziweka na kuzificha, pia awepo mtu wa karibu anayefahamu rela name ili siku ukitundikiwa tani kadhaa za mchanga basi huyo aliye karibu nawe ambaye pia ni member wa JF atoe taarifa kwa mods ili watoe taarifa kwa umma wa JF kuwa jamaa kalamba mchanga!
Ni muono wangu tu ila bado mnaweza kuona namna ya kuuboresha kama una mapungufu!
 
Kuna jamaa pia tulikuwa naye Swiss Aid akiitwa Justin Mdemu mtu wa Iringa alikufa ghafla akiwa kikazi Kigoma
 
Dah! Swali gumu hili. Kabla sijatangulia nitapata nafasi ya kuwasiliana nao. Lakini pia nina kijana wangu anafahamu mimi ni addict humu. Atawafahamisha.
sasa hapo nimekuelewa! vinginevyo nilikuwa na mashaka nikadhani mwenzangu ukienda huko utabeba mpaka laptop na modem...hahahahaha!
 
Back
Top Bottom