Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

Sasa kama unajua kuwa ni Mungu tu ndo anamfaham mbona wengine mnaendelea kumjadili mwanadamu mwenzenu wakati mnajua kuwa hamuwezi kumfahamu? Nimesema kama kuna ambaye anao uthibitisho kuwa aliyosema Mwigulu ni uongo basi auweke hapa au auwahishe mahakamani. Zaidi ya hapo tunaulizana na kujibizana hewa.
Hii ukiisoma bila chuki wala kujuana ni kweli imekaa vibaya. Maelezo, miaka nk vimepandana. Sisi tuliozoea kuchambua mambo hili liko wazi kabisaa.
Haswa hapo shule ya msingi hapajatulia kabisaaa.
Baadhi ya maelezo yake yanawatia hatiani watu wengine.
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Hapo pamekaa sawa MZALENDO,vyovyote iwavyo tunaofahamu historia yako shule ulizopita tunajua kuwa wewe ni kichwa....pale Mazengo na hata UDSM umeacha vumbi zito...,nadhani ndo mana watu wanapoteana,take it easy mkuu endelea kujenga nchi SHIKAMOO ZIKO NJIANI..
 
1. Watanzania wengi wanaandika kwa ku meander na kuto hit the point. Mtu kafika mpaka uwaziri halafu anashindwa kuandika straight to the point hata kama anaandika ukweli unashindwa kujua mara moja. Too emotional mpaka facts inakuwa vigumu kuijua.

For this reason, I give Mwigulu Nchemba the benefit of doubt. Otherwise kaandika kama mtu anayeficha kitu.

2. Utetezi mzuri ungeambatanisha vielelezo. Kila mtu anaweza kuweka story ya kuunga unga. Ningeheshimu utetezi wa Mr. Mwigulu Nchemba kama angeambatanisha vyeti, majina ya shule alizosoma, miaka, watu aliosoma nao etc. Mimi leo mtu akitilia shaka elimu yangu rasmi nitataja watu niliisoma nao wanaonijua ambao wanaweza kunitetea kuhusu miaka niliyosoma nao. Nitaweka vyeti wazi. Nitatoa majina ya walimu walionifundisha, madarasa waliyonifundisha, masomo waliyonifundisha. Nitatoa habari za mambo niliyofanya shuleni na miaka iliyohusika.

Sijaona vielelezo hivi. Sisemi kwamba muheshimiwa Nchemba ni muongo, nasema kama mtu aliyefanya kazi kubwa serikalini alitakiwa kujua maana ya vielelezo ni nini na kutoa utetezi wenye vielelezo badala ya maneno tu ambayo kila mtu anaweza kuandika vyake.

Dah!

Ni sawa, ila huoni kwamba hiyo ni shughuli kubwa mno?

Na kisa ni kuwajibu tu watu wasiojulikana wanaohoji elimu yako huko mitandaoni?
 
Nmefurahishwa na majibu. Swali. Naomba utufafanulie kwa nini ulichukua jina la daktari wakati wewe una jina lako mimi sijaelewa vizuri hapo mweheshimiwa.
 
Haya ndio majibu kutoka kwa waziri wa Tanzania ?
Hahaaaaa! Hii nchi inatia huruma sana... Kuna mmoja nimeona hapo juu alisoma naye A level na chuo japo walikuwa miaka tofauti, jamaa anamsifia kuwa alikuwa na IQ kuuubwa! Sasa ajabu amemalizia kwa kumuelekeza alivyotakiwa kujieleza ili aeleweke! Ukisoma post ile unabaki unajiuliza nani kati yao ana IQ kubwa?!
 
Na majitu yenyewe yasojulikana hata uandikeje bado tu hayataamini.

Kujibu tuhuma za kwenye mitandao kutoka kwa watu usiowajua hata majina wala sura, ni kazi bure tu.
Huyu ana wapiga kura wake. Hawezi kupuuza tuhuma za asiowajua maana wanaweza kuwa wapiga kura wake.

In any case, ukiamua kujibu, jibu kwa vielelezo.
 
MTU usome mpaka wapi bila hata ka certificate ka sheria ni shida tupu. Sikutegemea uandike gazeti bila supporting evidence. Ungefanya summary Mwaka ulipoanza na kumaliza kila stage na walimu hata wawili na wanafunzi ulosoma nao mbona ungeeleweka sana?
 
Jina la kwanza sawa unaweza badili kirahisi, hata la pili!!
Daa never seen labda kwa kuapa
 
Mheshimiwa ikiwa ulivyosema ndivyo; wanaolewa watakuelewa tu!
No hayajaisha. Mimi ningekua najibu hizi hoja ningetoa vyeti vilivyohakikiwa,mathalani cha kuzaliwa au cha Form IV ili kutoa shaka kabisa. Mheshimiwa hapo juu kahadithia na kuonyesha correctly kwamba mjina hubadilika. Aendelee ushujaa aliouonyesha kwa kuweka nakala za vyeti hivi. Viongozi kutegemewa kuenda extra mile, sasa enzzi hizi za uhakiki kila kona na kila uchao ndugu yetu asiache hata kimwanya cha shaka.
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Mpaka hapo hakuna ubishi kuwa jina la Lameck Mwigulu siyo jina lako ni jina la nesi,kama nesi alienda shule tayari kuna vyeti viwili vyenye jina moja la Lameck Mwigulu,Lameck nesi na Lameck mh waziri,kama mkanganyiko huu wa majina ulianzia tangu utoto kuna uwezekano mkubwa kwa wale wanaosema kuwa jina la Lameck Mwigulu ni la urithi wa kukuwezesha kuendelea na shule watakuwa wako sahihi.
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Mkuu Mhe. Mwigulu, kwa vile hili bandiko nimelikutia page 33, na sijaweza kusoma mandandiko ya nyuma, wala bandiko la tuhuma, hivyo siwezi kujua kama ulijibu haya, kwanza kwa heshma na taadhima, nikupongeza kujitokeza kujibu tuhuma, ila very unfortunately, majibu yako, hayajitoshelezi kabisa!, hakuna kitu chochote ulichojibu hapa, there are more questions than answers and there is something fishy!.

Majina yana formula ya majina, na hayawezi kuijiibukia tuu hivi hivi, na formula hiyo ni universal, dunia nzima.

Jina lina given name, yaani jina ulilopewa wewe, hili given name linaweza kuwa moja au hata kumi, haijalishi, kwenye given name, ni lile jina unaloitwa, liwe la utoto, ubatizo, etc, Kiingeza linaitwa fast name!.

Jina la pili, ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako, na hapa hakuna excuse, kama mwanzo kwenye given name, umetumia jina la nyumbani, la kilugha, then jina la pili lazima liwe jina la ubatizo, ukitangulia na jina la ubatizo, then jina la pili au liwe ni jina la kwanza, la mzazi wako, au ukitumia fast name ya majina mawili yote ya kwako, then jina la tatu ni lazima liwe ni jina la kwanza la mzazi wako!, na jina la nne ni lazima liwe ni jina la ukoo wenu yaani sir name.

Kwenye majina yako, sijaweza kuona jina la mzazi na jina la ukoo, huwezi kutumia majina yote ya given name bila jina la mzazi na jina la ukoo!.

Naomba wenye acess na immigration, fatulieni DN ya Mhe. Mchemba muone imeandikwaje, kwa sababu bila jina la mzazi na jina la ukoo mtu huwezi kupata passport kwa majina ya kuokotezwa!.

This is the begining of pandora box, we have to reach to the bottom of this, ila asante sana kujitokeza na kujibu, kwa sababu uwongo, ukisemwa sana na kurudiwa rudiwa bila kukanushwa hugeuka ni ukweli.

Finally, wewe mwana Ilboru mwenzangu, ujege mara moja moja humu jf sio mpaka tuu kuja kujibu tuhuma, na ile shule iliokufikisha hapo uikumbukege!.

Asante.

Pasco
Rejea, kati ya wagombea wote wa urais wa CCM, Mhe. Mwingulu, ndie aliye ni impress sana kuliko wote kwa kuwa the most genuine kumbe. .m
Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The ...
 
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck

Daah,inamaana huyu daktari alikua anaitwa lameck ila kwa kilugha mwigulu?yaani mwigulu na lameck ni jina moja ama....kama itakua hivyo ulizawadiwa majina yote mawili na daktari wa kijiji....nifafanulie hapo tuuu comrade
 
Mkuu,
1. Hapo uliposema uliacha Shule ukarudi kuchunga Ng'ombe na uliporeje Shuleni ndiyo ukabadilisha na jina? Why?

2. Uliporejea masomani je! Ulirudia Darasa ama uliendelea na Darasa hilo hilo wakati umebadilisha majina?

Ntobi

Inavyoonekana,alifeli mara ya kwanza na alivyorudi akaona abadilishe majina yote labda anaweza faulu na kuendelea na masomo yake na ndo kilichotokea,mawazo yangu ya haraka haraka
 
Nakubaliana nawe kuhakiki ufanisi kazini badala ya cheti, ndoa hazidumu kwa ajili ya vyeti vya ndoa bali matendo kwenye ndoa au kwenye maisha ya ndoa, ila sasa tunaandikisha watumishi wapate vitambulisho

Kwa hiyo unataka kutuambia serikalini mko makundi mawili:kundi la wanaohakiki vyeti na wale(kundi lako) mnaotaka uhakiki wa ufanisi.Kama ndivyo hilo Baraza la Mawaziri ni la aina gani? Na je unaweza kutuambia bila kupepesa macho kuwa kujitokeza kwako hapa kuja kujibu tuhuma hizi hakutasikindikizwa na tukio jingine huko mbeleni,mintarafu kazi yako?
 
Mkuu, vipi shule ulizosoma ni zipi?

Vipi ni utaratibu upi ulitumika kubadilisha jina uliporudi kuendelea na shule? Maana drs la kwanza hadi la tano jina jingine,, la tano na kuendelea jina jingine... Iliwezekanaje hii?
 
Back
Top Bottom