Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu tuhuma za kughushi vyeti vya taaluma, kuiba jina

Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,

Hii imeeleweka kabisa anayeendelea kubisha atakua ana Mapepo!
 
Nilitegemea katika majibu ya mtu msomi kuona haya.

1 . Shule ya msingi ulisoma ipi?
2. Ulianza na kumaliza nwaka gani?
3. Pengine utaje hata wanafunzi wawili watatu uliosoma nao
4. Wapo walimu waliomfundisha Magufuri primary je wewe unaweza tutajia hata wawili?

Inakusaidia nini acha kupoteza muda wako au hujui kusoma!!
 
Ha ha ha , hapa nimetulia tuli na karanga zangu robo naangalia mchezo unavyoendelea na wala sitiii neno ila nakumbuka msemo wa kimang'ati usemao " time will tell" na yale maneno yasemayo kila jiwe litafunuliwa ha ha ha huu uhakiki huu mh
 
Mimi ninavyo kumbuka ni kwamba zile form za maendeleo ya mwanafunzi na kumaliza Shule ya msingi zilikuwa zinajazwa kuanzia darasa la tano Kama sikosei, sasa wengi wakirudia Shule ilibidi wawe wanatafuta Jina la Mtu aliye acha Shule na haja maliza la saba ili taarifa zake uchukue wewe unaye rudia Shule au Ndio Hiyo ya kurekebisha given name na first name , iliuonekane kwamba Jina Hilo halikumaliza Shule ya msingi.
Sasa ndugu yetu Ile ya kwenda kuchukua ngombe halafu kurudi Shule inawezekana alimaliza la saba ha kuchaguliwa hivyo ilibidi arudi darasa la tano na kuchukua taarifa za huyo lameck mwigula Nchemba au alitengeneza taarifa za mwanafunzi mpya kwa Jina Hilo .
Lakini kuna kitu kingine cha msingi cha tuhuma au hisia kwamba ukiisha Anza kuwa Huna uadilifu the kuna uwezekano mkubwa kwamba Huko mbele utakuwa sio muadilifu kwenye mitihani au kazi au siasa .
Sasa tatizo kubwa linakuwa atatokaje hapa ? Na akafanye nini ?? Kwa mtaji upi , je kuna adhabu yoyote zaidi anayo stahili kwa kosa aliyofanya Kama slit enda tendo baya ?? Jamani pia Mlugo alikuwa na Tuhuma??? Na wengineo.
Ki ukweli ukiingia kwenye siasa ni vizuri ukajihakikishia uadilifu mkubwa wa maisha yako , mpaka uraia wako
 
Kwema mkuu Shumbi?

Kwanza nikupongoze kwa ujasiri wa kujitokeza hadharza vyeti haziwezi kufanana.ujibu tuhuma hizi. Hakika huo ni ukomavu na uungwana uliotukuka.

Nimefurahi pia kujua maana ya neno Mwigulu na Madelu leo. Asante sana. Ila mzee, hapa tutakutwanga tu maswali kwa heshima na taadhima. Usitukimbie tafadhali..

Sasa mie swali langu ni moja tu hapo kwenye kuamua kuchukua majina ya huyo nesi/daktari.

Ninachouliza, yeye hakuwahi kusoma? Na kama alisoma alitumia majina gani? Huoni kwamba utakuwa umechanganya kuchukua jina lililowahi tumika kutahiniwa? Nadhani hapo ndio msingi wa maswali haya kuibuka...

Iliwezekanaje kutumia majina ya daktari kwenye taaluma ilihali na yeye aliyatumia pia?
Beth mbona swali lako lko wax tu hapo swala la kufafanana majina no la kawaida ..is to she kabdli jini lakini namba ya vyeti
 
Mleta uzi naomba one to one Q&A

Nataka nikutajie uliofanya nao mtihani wa darasa la saba kwa miaka miwili tofauti.

Sema tawile (inamuhusu mleta mada wengine muwe wasikilizaji)
Nafikiri hoja hapa ilikuwa vyeti fake yaani ambavyo mtu navitumia wakati hana elimu hiyo. Sasa kuhusu majina na kurudia miaka hiyo mimi naona siyo issue. Kama mtu alikuwa anarudia miaka ili afaulu maana yake alikuwa anatafuta elimu kwa juhudi zake. Kwakuwa alikuwa anaingia darasani na kufanya mitihani yeye mwenyewe yaani physically maana yake ni kuwa anaelimu husika ianayoelezwa kwenye vyeti mpaka itakapothibitishwa kuwa hivyo vyeti si vyake au ni vya kugushi
 
  • Thanks
Reactions: NHS
Kwa hiyo unasemaje kuhusu uhakiki wa vyeti..?? Uendelee au uachwe..?? Au wahakikiwe wasio mawaziri na wakuu wa mikoa..??
KAMA KUCHOKONOA BASI WENYEWE NDO WAMEANZISHA, NA WANANCHI WANATAKA HAKI ITENDEKE KWA KILA KTANZANIA ANAYETAKIWA KUHAKIKIWA VYETI VYAKE AFANYIWE HIVYO BILA KUJALI NAFASI YAKE..
Uhakiki uendelee maana umeshaanza. Waliorudia darasa watasema walitumia jina la nani au ruhusa ilitoka kwa nani kama alitumia jina lake halisi. kiujumla wako wengi!
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. .....

Mwigulu,
Asante kwa kuweka kumbukumbu sawa.
Hii pia aiwekee kumbukumbu sawa. Comrade anatajwa twajwa humu kwenye uzi wenye kichwa cha habari "ridhiwani kikwete amuunga mkono makona kutokomeza madawa ya kulevya" kama mods hawataiweka "magufuli" na kutupa funguo baharini.

Tuhuma ni nzito.
 
Safi sana Mwigulu. Watu wanashindwa kutofautisha kuendelea kusoma kwa kutumia ufaulu wa mtu na kuendelea kusoma kwa jina lingine. Hapa cha kujiuluza ni je, ulifanya mtihani na kufaulu kuendelea na masomo? Haijalishi ulikua na jina la nani.
 
That is relative. Ukweli ni kuwa. Hata kama ni ABCD katika mambo ABCDA jamaa sasa ana PhD. Je una swali jingine?
 
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Bora hata usingejibu!
 
Back
Top Bottom