Majibu ya Sitta kwa Dr Slaa: Asema Dr Slaa Mnafiki, Dikteta

Huyu mzee ni mnafiki wa hatari hatari nimewfahamu kwa muda mrefu tokea akiwa tic ni mnafiki ile mbaya,me nafkiri kuzidi kumjadili tunampat chati tuacheni ajadiliwe na mama sita.
 
Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za msingi sikubaliani nazo.

Hili kujua unafiki wa huyu mzee, soma haya hapa chini ni maoni yake alipohojiwa na Mwananchi kuhusiana na elimu, afya kutolewa bure.



Sitta: Elimu Na Afya Bure Inawezekana

Edwin Mjwahuzi, Kagera

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema Serikali kutoa huduma ya Elimu na Afya bure inawezekana ikiwa tu mianya ya rushwa na ufisadi itadhibitiwa ipasavyo na wananchi wataweza kunufaika na rasilimali zilizopo nchini.
Sitta alisema ni lazima turudi kwenye misingi ya uadilifu, kujali wanyonge, kukataa rushwa na kukataa ufisadi wa aina yoyote ndipo tutaweza kukusanya na kuinua uchumi wa kutosha na kulipana mishahara mizuri, kumlipa pensheni mzee na kutoa huduma hizo bure.
Aliyasema hayo alipokaribishwa katika mkutano wa akinamama wajane kutoka wilayani Karagwe na Kyelwa mkoani Kagera na kuwashirikisha wazee wa Wilaya hizo uliofanyika katika ukumbi uliopo katika ofisi za CCM wilayani Karagwe.
Sitta alisema itakuwa ndoto za kupata huduma hizo bure kama nchi haitafanikiwa kuziba mianya yote ya rushwa na wananchi wataendelea kupiga kelele wakitaka kupatiwa huduma hizo bila ya mafanikio.
“Ningependa kuwaambia wananchi, najua karibu wote tunataka utoaji wa huduma ya afya, elimu ya kuanzi msingi mpaka elimu ya juu kuwa bure, ndugu zangu katika hali ambayo hata huduma ya afya ya kawaida haipatikani ni mtihani mkubwa kwa kutoa elimu ya bure,” alisema.
Aliongeza, “Hatuwezi kuwa na nchi ina kila kitu, tunayo makaa ya mawe, maziwa, mito, bahari, madini, gesi, mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro na tuna hekta za kilimo zaidi ya milioni 88, tunataka Watanzania muamke na muache kushabikia rushwa ndogo ndogo tuingie katika utamaduni unaotuwezesha kujenga heshima ya nchi yetu kwa kujali uongozi ulionyooka na wenye uhadilifu.”
Sitta alisema wananchi wasiwe na ndoto ya maisha bora kwa kila mtanzania ikiwa rushwa na ufisadi utaendelea kutawala na kufumbiwa macho.
“Ndugu zangu hatuwezi kupata maisha bora kama kiwango cha rushwa, ufisadi na dhuluma kikiwa hivi hivi tunavyokiona hivi sasa, kwa sababu Serikali ilileta utoaji pembejeo kwa kutumia vocha sasa tutaendelea vipi kama vocha zenyewe zinachakachuliwa?” alihoji.
“Iwapo tutadhibiti mianya ya ufisadi na rushwa, nchi yetu itainuka na kuweza kuwasaidia wazee wetu, wajane, watoto yatima kwa kuwapatia huduma nyingi nzuri, ilimpadi tu ufisadi unatakiwa kupigwa vita kuanzia chini huku,” alisema Sitta.
Sitta pia aliwaomba wajane hao na wazee kupita kila mahali na kuwashaui wananchi wao wakiwemo na wana CCM kuwa makini wa watu wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa na kiserikali wasije wakafanya makosa kuwaweka watu wenye nia mbaya na nchi hii kwa kujali matumbo yao na familia zao.
“Sasa hivi hata kule bungeni mnaona baadhi ya mawaziri, anatokea mtu amekuwa waziri ndani ya miaka 2 au chini ya hapo unasikia kanunua nyumba Mikocheni ya mabilioni, haiwezekani na wala haingii akilini hakuwa waziri wa wananchi huyu ameingia kuchuma tu,” alisema.
Waziri Sitta amemaliza juzi ziara ya kiserikali ya siku tano mkoani humo alipokuwa akiangalia miradi mbalimbali inayohusiana na muingiliano wa uchumi na kijamii kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Gazeti Mwananchi jumapili
 
Sasa SIta mara Mbowe anauzoefu wa disko mara hata Kawawa alikuwa mwigizaji, Kweli? Jipange six uzuri CCM wenzio wanamwamini Slaa sana kuliko wewe. Kazi unayo.
 
Juzi kasema elimu bure inawezekana, leo anakana, juzi tena kasema Dr. Slaa safi leo Dikteta sasa huyu mzee jamani!!!?
 
Kumbe Slaa alimuomba Sitta akagombee Urais chadema? akamtosa!
 
Huyu mzee ccm ya lowasa hana chake,sasa kote alikotaka kwenda alinyea kambi kwa hiyo kabaki kama zezeta ana lopokalopaka tu,mara amsifie slaa mara amchafue,bora anyamaze tu,hana mvuto wowote kama anavyojisifu yeye......aligombana na gazeti la mwanahalisi leo chadema hivyo ndio kujipambanua kuwa mpinga ufisadi?pumbavu kabiosa huyu bwana.......mwige lowasa hana maneno machafu kwa mtu au chama chochote kile....yeye anahaha kimpango.....sita chadema wanachukua dola soon,uroho wako wa madaraka umedika kikomo huku hatuna kupozana au kuogopana kama ccm.....kwishney 6
 
Napata mashaka makubwa kwa huyu mzee Six, juzi kamsifia Dr Slaa, leo anamuita mnafiki, sasa hapo nani mnafiki wa kweli? Sita au Slaa?

wanafiki ni wale waliokwenda kumbembeleza agombee urais mwaka juzi na leo rais wao huyo mtarajia wanatuambaie hafai hata kuongoza kata....! hizi ndio mzee sitta anaziitaga siasa za maji taka na leo katuongezeamsemo mwingine 'safu nyembemba mno ya uongozi"
 
Asichokifahamu Sitta ni kwamba kinachohitajika sasa ni serikali na Cabinet ndogo sana kuliko hii ya sasa ambayo hata ushirikiano wa Afrika Mashariki ni wizara badala ya kuwa Idara tu kwenye wizara ya mambo ya nje. Sitta pia hafahamu kuwa wanaCHADEMA sio hao tu anaowafahamu yeye na anaowaona majukwaani na Bungeni.
Sitta angefuatwa yeye na Dr Slaa kugombea URAIS angekwisharopoka siku nyingi ili kujizolea umaarufu wa haraka na bei nafuu. Hivi kweli hivyo alivyo SITTA anaweza kuwa RAIS wa NCHI hii? Tuache utani jamani. Tumesota sana kipindi hiki.
 
SITTA WASHA MOTO,USIONGEE KWA KUOGOPAOGOPA,WAMESHAKUINGIA KWENYE CHUPI HAO,TATIZO LAKO UNAPONDA MARA UNASIFIA NDIO MAANA UNAONEKANA MNAFIKI.SASA MAMBO YAMEHARIBI UWEZI KWENDA CDM,UNAFIKIRI Dr.SLAA KWANINNI WATU ANAMZUKA NAE,HUWA ANAWASHA MATO NDIO MAANA VIJANA WENGI WANAPENDA,SIASA ZA VURUGU NDO SASA,FAIR FAIR HAMNA NI MAMBO YAKIZAMANI,WANATAKIWA WATU WAPEWE MZUKA IWE KWELI AU UWONGO,NDIPO TULIPO FIKIA HAPO.
 
Sitta ni mnafiki sana yani leo unajifanya unamsifu mbowe!
 
Sitta ni mnafiki sana yani leo unajifanya unamsifu mbowe!
Hajamsifu bali amesema huwezi kueleza wasifu wa mbowe bila kutaja mchango wake kwa taifa kwenye mambo ya uchezaji wa disco!huo ndio ukweli anao mchango mkubwa sana kwenye mambo ya kuwawezesha watz kuwa wacheza disco
 
Yeye anamvuto gani hadi vyama vyote viwe vinamtafuta:
  • .....CCJ walisema SITTA ni mmoja wa waasisi wake na tena ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa mpango huu;
  • ......Aliyekuwa mbunge wa Kishapu, FRED MPENDAZOE, anasema SITTA, MWAKYEMBE na NAPE NNAUYE ni wasaliti!... Walimtanguliza kuijenga CCJ kabla ya kuhamia;
  • ......CHADEMA walionyesha utayari wa kumpokea baada ya yeye kuonesha nia ya kuondoka CCM.
 
Sitta anaanzisha vita na wananchi si Dr Slaa wala CDM. Sidhani kama amejipanga vizuri kupigana vita hiyo,na nahisi Moto utamwakia sasa,na amejiharibia
 
Ukweli ni kitu kingine yaani sitta amekuwa humbled mpaka anajiita mpiga kura wa tanzania? chadema moto.na hakuna kumwacha kajibu kinyenyekevu asishambuliwe zaidi,mnafiki kabisa huyu mara elimu bure haiwezekani mara inawezekana ufisadi ukiisha,mtamwelewaje mtu huyu,tumbiri kasoro mkia
 
Tofauti na watu wengi wanvyochukulia mambo kwa mtazamo wa kichama chama
Lakini sisi tunaochukulia mambo kwa jicho la uhalisia Mh Sita amejibu vyema kama mtu aliyekomaa kisiasa

Tatizo lililopo hapa JF ni kwamba wengi wetu ni wanazi wa CDM hatuoni hatusikii na kuthibitisha hilo hata Sita angejibu kwa kuuomba radhi uongozi wa CDM bado comments zetu zingekuwa ni hizi hizi tu, mnafiki,mroho wa madaraka nk nk kwasababu tu Sita ni CCM

Hapa swala la msingi la kujiuliza ni je kama kweli Sita alikuwa anazima mijadala,fisadi,mroho wa madaraka na tuhuma zote alizotupiwa na Dr na wana JF, je hawakulijua hilo akina Dr hadi wakubaliane naye awe mgombea wao wa urais?
Au baada ya kuwatosa kama Dr salaa alivyothibitisha kwenye madai yake ndio wamemuona fisadi.

Kama CDM walifikia kuwa tayari kumpisha kiti cha urais kilaini hatuoni hii ni sababu Sita anaona CDM hakuna safu kubwa hadi wanaanza kuvizia kurubuni viongozi makini toka vyama vingine

Hivi sasa mijadala mingi humu JF inakosa nguvu na kuwa ya upande mmoja tu, watu wanataka kusikia mabaya ya CCM na mazuri ya CDM tu, kwenda kinyume na hapo wewe ni msaliti na hufai kwenye hii jamii

Tujadili kwa jicho la upande wapili pia kama nilivyoainisha hapo juu
Maana sasa isije ikawa hata hoja za msingi zinazohitaji mjadala zikazimwa kwakuwa tu CCM ni mafisadi
 
Huyu mzee kanya halafu anataka kuzuga si yeye,umeingia choo cha kike hakika....hakuna nguvu ya umma iliyowahi kushindwa duniani,mnafiki sana huyu!!!!magamba mfukuzeni huyu kigeugeu.
 
Back
Top Bottom