Majaji waonya: Mahakama Isigeuzwe Gari Bovu

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
PAMOJA na dhamana kuwa haki ya msingi ya mshitakiwa, katika kesi ya Mbunge wa Arusha
Mjini, Godbless Lema (Chadema), Mahakama ina haki ya kuizuia dhamana hiyo.

Wakizungumza na gazeti hili hivi karibuni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu walionya kuwa
Mahakama si gari bovu, kwamba kila mshitakiwa au jamaa zake, wanaweza kuisukuma itende
watakavyo, kwa kuwa inafanya kazi kwa kuzingatia sheria na misingi ya haki.

Walifafanua kuwa nafasi ya Mahakama kutoa dhamana kabla ya siku ya kesi iliyopangwa kwa
mshitakiwa aliyeikataa awali, haipo kisheria si tu kwa aliyeikataa kwa makusudi bali hata kwa aliyekosa wadhamini kwa bahati mbaya.

Walikuwa wakizungumzia sakata la dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
(Chadema) ambaye wiki iliyopita aling'ang'ania kwenda rumande katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo licha ya dhamana yake kuwa wazi kwa kile alichodai kuwa anaandamwa
na Polisi kwa kufunguliwa mashitaka mengi.

Pia Lema katika uamuzi huo wa kutokubali dhamana alisema ni bora aendelee kukaa rumande
kama ishara ya kutetea wanyonge kabla ya kubadilisha uamuzi wake akitaka dhamana baada ya kilichoitwa kushauriwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe lakini akanyimwa
na Mahakama.

Majaji hao wa Kanda ya Dar es Salaam ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema
hakimu aliyemkatalia Lema dhamana, alitoa msimamo sahihi kisheria, utakaowafanya watu
wengine kuheshimu taratibu za Mahakama.

Wakati mmoja wao akisisitiza kuwa dhamana ni haki ya mshitakiwa pale atakapokuwa
ameikubali, mwingine alisema si kazi ya Mahakama kulazimisha mshitakiwa kukaa nje ya Mahakama endapo yeye mwenyewe (mshitakiwa) haoni umuhimu wa kufanya hivyo.

Lakini alifafanua kuwa mahakimu wanapokubali kutoa dhamana kwa washitakiwa wanaokuwa wamekosa wadhamini wakati kesi zao zinapofikishwa mahakamani, ni ubinadamu tu na wala si matakwa ya kisheria.

"Inawezekana watu wanadhani kinachofanywa na mahakimu wengi kwa sababu ya ukarimu kutokana na washitakiwa kukosa wadhamini wakati ule kesi zao zinaposomwa mahakamani ni maelekezo ya sheria. Ule ni utu tu wa hakimu na hakuna sheria inayolazimisha hilo litendeke.

"Sasa sembuse mshitakiwaanayegomea haki yake ya dhamana? Huyu hana njia ya mkato ya kuwa nje, ni lazima asubiri kesi inapoletwa tena mahakamani, ndipo aombe dhamana yake kwa kufuata taratibu za kimahakama," alifafanua Jaji huyo.

Jaji mwingine aliongeza kwamba Lema alipaswa kufikiria kuwa ana majukumu mengine bungeni na hivyo kukataa dhamana kwa sababu yoyote, kusingeweza kuisukuma Mahakama kumbembeleza afanye vinginevyo, eti kwa sababu ni kiongozi.

"Kesi hupangwa kila baada ya siku 14, sasa Lema alipaswa afikirie na kukumbuka hilo kabla ya kugomea dhamana, kwa sababu Hakimu yeyote hawezi kukubali kupindisha sheria na kuandika hati ya dhamana kwa mtu aliyetingisha kiberiti, wakati muda wa kesi yake uliopangwa haujafika. Kwanza kugomea dhamana ni makusudi na sheria haiendelezi makusudi hayo," alisema.

Source: GAZETI HABARILEO
 
Hao Majaji wanaotoa misimamo yao kwa kujificha na wakikataa kuandikwa magazetini ni vilaza wateule wa JK! Mtu mwenye kujiamini hawezi kujificha nyuma ya gazeti!
 
[h=1]Mafisadi CCM lazima wavue gamba[/h]Kutoka Gazeti la Habarileo

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, amesema yeye ni sawa na mtu aliyeteuliwa kufanya kazi ya kunyonga mkosaji aliyehukumiwa adhabu hiyo na Mahakama, hivyo hawezi kuogopa kutekeleza hukumu hiyo.

Akifafanua kauli hiyo jana mjini Morogro, Mukama alisema uamuzi wa ngazi za juu wa CCM ukishatolewa kuhusu kuvua gamba watuhumiwa wa ufisadi, hakuna kiongozi atakayepuuza kuutekeleza.

“Ufisadi unasemwa dhahiri na wananchi kwa kuwataja watuhumiwa hadharani wakiwahusisha ana EPA (Akaunti ya Malipo ya Nje ya Benki Kuu), Dowans, ununuzi wa rada na Richmond … na vikao vya chama vimetoa uamuzi.

“Kilichobaki ni utekelezaji tu…na hukumu ikishatolewa na Mahakama hakuna njia nyingine isipokuwa kutekeleza agizo hilo,” alisema Katibu Mkuu huyo alipokuwa akizungumzia madai, kwamba anaogopa kutoa barua za kujivua gamba kwa watuhumiwa wa ufisadi.

Akihutubia mahafali ya wanafunzi wanachama wa CCM wanaomaliza Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro, Mukama alisema hataogopa kusimamia kikamilifu uamuzi wa chama hicho wa kuwatosa watuhumiwa hao.

Alisema vitendo vyao vimesababisha CCM na Serikali ichafuke mbele ya Watanzania.

Mbali na kuwavua gamba, Mukama alisema CCM pia itashughulikia suala la wafanyabiashara wasio waadilifu wanaojipenyeza ndani ya chama hicho, na itapambana na saratani ya kujilimbikizia madaraka na kukiondoa chama hicho katika utegemezi wa matajiri na wahisani wanaokiweka pabaya.

Alisema, hakuna mwananchi asiyejua kuwa ndani ya CCM wapo viongozi wenye nyadhifa kubwa wanaotuhumiwa kwa ufisadi kuanzia wa EPA, Richmond, Dowans, Rada na kashfa nyingine.

Katibu Mkuu huyo alisisitiza kwamba ili kukisafisha chama hicho mbele ya jamii na kukifanya kikubalike katika uchaguzi wowote, ni lazima watuhumiwa hao watoswe ili kurudisha imani kwa Watanzania.

Mukama alionesha katuni aliyodai imemchora hivi karibuni, akiwa na barua mkononi ikionesha kuwa ameshindwa kutoa uamuzi na kusisitiza kuwa uamuzi huo ni wa chama, hivyo utatekelezwa kama ilivyopangwa.

Awali katika risala ya wanafunzi hao, walitaka viongozi wote wa CCM kujikita kuwaletea maendeleo wananchi, ili baadaye wapimwe kwa kazi zao.


Wanachama hao waliwataka viongozi wahubiri amani badala ya kuendeleza malumbano na vyama vya upinzani na kuwataka watumishi wa Serikali kuachana na siasa wakati wakiwa watumishi wa umma.utoka Gazeti la Habarileo


 
Back
Top Bottom