Maisha yataendelea kuwa magumu hadi lini?

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Nimetua jiji la Dar leo nikashukia hoteli moja niliyozoea kufikia. Nimeshanagzwa na vyumba kuapandishwa kwa kiasi kikubwa. Chumba cha shs 50,000/= sasa kimekuwa shs 75,000/= vile vya 30,000/= sasa ni 40,000/= . Nimeshangaa kwani siyo zaidi ya miezi miwili nilikuwa hapa na bei imepanda hivyo. Nilipouliza kwanini wamepandisha(kwa utani tu kwani najua hawawajibiki kunijibu) walichonijibu ni kuwa sasa wanatoa huduma ya umeme kwa kutumia generator 24 hours. Nikawauliza nami kwa utani kwa hiyo tukimbana Ngeleja akatoa umeme na kuach mgao mtashusha? Wakasema ndiyo – japo najua hakuna kinachoshuka TZ, hata kama kimepanda kwa Bahati mbaya Hivi maisha yetu yataendelea kuwa magumu hadi lini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom