Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

Adriel Vin iko hivi kama wadau wanavyosema fungua code zote achana na wale wanao jifanya wako busy na kushindwa kusoma kamba ndefu,,,, hakuna mtu ambaye hana mambo ya kufanya ila kila mtu husoma kwa mda wake kadri anavyo upata.

Kwahiyo wapuuze tu na achana nao mwenye kusoma na asome na asiyeweza achape lapa .
 
SEHEMU YA 11

Tulipoishia

Majibu ya mama mchungaji yalitoka na alikua amechaguliwa kujiunga na chuo cha Mara kule. Hivyo alitakiwa akasome diploma yake huko.
Kwa upande wangu nilikua nishakua na ujanja ujanja wa chuo, nishajua kuvaa kama mwanachuo na nilishanunua smartphone HUAWEI Y300 kama sikosei.

Tuendelee sasa…

Mama mchungaji alifanikiwa kuja Mwanza ili aelekee mkoa wa Mara kwa ajili ya kuendelea na masomo.

Wakati huu mimi nilikua mwaka wa 2 na nilikua nishaanza mahusiano na binti mwingine pale chuoni.

Mama mchungaji alikuaja na mimi ndo nilienda kumpokea pale Nyegezi. Lakini wakati huu sikuwa nikimpenda na kumjali tena kama zamani.
Wakati niko sec year nilishaanza kukaa mwenyewe bila mate. Hivyo haikua shida kwa mama mchungaji kuja kukaa nnapokaa. Sijui ni nini kiliniingia kichwani mara baada ya kumpokea mama Mchungaji na kukaa nae kwa masaa kadhaa nilimwambia ntaenda home kwa mzee then ningerejea baadae lakini kiukweli sikua na plan ya kwenda kwa mzee.

Nilikwacha ndani nikaenda kwenye mambo yangu na siku hiyo sikurudi pale hostel kwangu. Mama mchungaji alilala peke yake pale huku akinitumia sms nyingi tu za kuniuliza narudi saa ngapi.

Kesho asubuhi nilirudi na alitakiwa kwenda chuo siku hiyo. Nilimsindikiza hadi Buzuruga na tukaagana pale akaondoka.
Baada ya kufika Mara sikuwa na mawasiliano mazuri na yeye kwani nilikua busy na mwanamke mpya niliyempata chuo .
Ikumbukwe hali ya kiuchumi ya Mama mchungaji na kwao kiujumla haikua nzuri na alihitaji msaada wangu sana.
Aina ya maisha aliyopitia kule Mara ingekua ni mimi nisingemaliza chuo, au nisingefaulu kabisa.

Mama mchungaji alishindwa kulipa kodi kwa muda mrefu sana hadi ikafikia hatua mwenye nyumba akamruhusu kukaa bure maana alikua anaona hata kula yake tu ni tabu. Familia yake ni kama ilikua imemtelekeza. Kuna siku amewahi niomba just elfu 5 akaprint assignment ila sikuweza kumsaidia kabisa. Alishaniomba msaada mara nyingi lakini sikuwa na msaada kwake.

Mapito aliyopitia kule mkoani Mara yalikua mazito mno lakini mbali na yote hakuacha kunipenda wala kunitafuta. Maskini mtoto wa watu kuna muda alilazimisha kuja Mwanza ili angalau anione lakini niliishia kumwacha tena ndani kwangu na sikurudi siku 2 hadi pale alipoondoka. Sijui ni nini kilikua kimeniingia lakini nilijikuta sitaki kuwa naye karibu.
Ili siku nilimwacha siku 2 ndani hadi akaondoka nakumbuka alinitumia ujumbe mrefu sana wenye kuonyesha ana maumivu kiasi gani na aliahidi kutokanyaga tena kwangu.

Nilirudi hostel kwangu na maisha yakaendelea huku nikiwa na mahusiano mapya na Binti flani wa chuo.
Mawasiliano na mama mchungaji yakakata na kuna siku nilipost picha instagram nikiwa na huyo binti wa chuo.
Mama mchungaji aliona na akanitext “Hii ndiyo sababu umeniacha na kuona sifai?” Mi sikumjibu kitu na maisha yaliendelea.

Kwa tabu sana Mama Mchungaji aligraduate, wakati huo mimi nilikua third year. Wakati anatoka Mara kuja Mwanza alinitafuta akanambia amefikia Lodge flani (iko karibu na stand) aliniomba niende kumwona. Na wakati huo kwakweli nilikua single kwani yule Binti tulikua tushaachana.

Nilienda kumwona Mama Mchungaji na kiukweli aliniuliza maswali mengi ambayo sikuwa na majibu zaidi ya kusema sorry.
Tuliongea sana na alinisamehe na alinitunuku tunda.
Lakini safari hii naona ilikua tofauti, alikua amekua na ka uzoefu flani ambako sijazoea kutoka kwake.
Ilibidi nimwambie “Naona umeamua kunicheat” na nilikua na hasira kwakweli. Alinambia ndiyo nilikua na mahusiano mengine baada ya wewe kutokua na muda na mimi tena. Alianza kulalamika sana na akadai hakumpenda yule mwanaume ila alikua anatafuta faraja tu baada ya kuikosa kwangu, akaongeza kuwa mwanaume yule alikua akimsaidia kidogo matumizi kwani hakuwa anapewa pesa yoyote kwao.
Nilijisikia vibaya sana na nikajiona mkosefu sana lakini sikuwa na namna yoyote.

Asubuhi mama mchungaji alisafiri kuelekea mkoani Shinyanga huko alikua na ndugu yake na alisema atakaa kwa muda kidogo akiwa anahangaika kutafuta kazi kwani asingeweza kurudi kwao, alishachoka na hekaheka za mama wa kambo pale kwao, pia alisema mdogo wake wa kike alipata mimba na kajifungua mtoto na wote wako palepale kwao. Hivyo aliona hawezi kurudi tena kwao Tukuyu.

Mimi nilimwambia sawa na nikaahidi kujirekebisha. Nilirudi chuo na maisha yaliendelea.

Wakati niko third year tuliandaa party ya welcome 1st year na hii ilinipa nafasi ya kuwa karibu na binti mmoja (Tumwite Nelly).

Mama mchungaji alifanikiwa kupata kazi baada ya miezi miwili tu, kuna nafasi zilitangazwa na almashauri ya manispaa ya Shinyanga. Alifanikiwa kufanya interview na alipita (alikua na ufaulu mzuri sana).
Mama mchungaji alipata kazi kama afisa mtendaji wa kijiji huko Kahama ndani ndani.

Maisha yangu chuo yaliendelea lakini kutokana na aina ya maisha niliyokua nikiishi, pesa ilikua haikai hivyo nilikua mtu wa mizinga sana hasa kwa Kaka zangu na watu wengine wa karibu.
Ilifika hatua nikawa nampiga mizinga Mama Mchungaji na kiukweli hakuwahi kuninyima pesa.
Mama mchungaji ndo akawa ananibust elfu 20 hizi au 30 mara nyingine hata 50k licha ya kuwa na mshahara mdogo.

Kwakweli sikuwa najisikia vizuri namna nilivyomfanyia alafu bado binti ana upendo wa namna ile kwangu.

Sasa kama nilivyosema niliingia kwenye mahusiano na binti mwingine ambaye ni Nelly. Nelly alikua binti wa mambo mengi, mwenye kupenda fame, kuendeza pamoja na show off.
Nilivyofika 3rd year niliigiza movie flani chuo na ndio nilikua main character then nikamvuta Nelly akawa mwigizaji pia. Mahusiano yetu yalikua na drama nyingi ma show off sana.

Mama Mchungaji aligundua nna mahusiano mengine na this time aliamua kuachana na mimi jumla jumla.

Niseme tu kama kuna mtu muhimu nilimpoteza ni mama mchungaji. Natamani kuelezea namna nilikuja kupigwa na kitu kizito na huyu Nelly lakini naona ntakua nazungumzia mapenzi sana kwenye huu mkasa.

So sitomgusia Nelly wala mwingine, ntaruka moja kwa moja hadi kwenye maisha baada ya chuo ambapo ndio chanzo cha kuandika story yangu hapa.

TUTAENDELEA leo leo

Nasoma maoni
Ukirudi nishtue boss
 
Adriel Vin iko hivi kama wadau wanavyosema fungua code zote achana na wale wanao jifanya wako busy na kushindwa kusoma kamba ndefu,,,, hakuna mtu ambaye hana mambo ya kufanya ila kila mtu husoma kwa mda wake kadri anavyo upata.

Kwahiyo wapuuze tu na achana nao mwenye kusoma na asome na asiyeweza achape lapa .
Nimekuelewa vyema na ntafunguk kila kitu
 
Habari wanaJF, bila shaka kila anayesoma hapa ni mzima na afya, na kama sio Mungu akupe lililo hitaji la moyo wako🙏

Mimi ni kijana wa miaka 30. Nimezaliwa mkoa wa Mwanza, nimepata elimu yangu ya msingi huko mkoani Mwanza. Nilimaliza kwa ufaulu wa kawaida lakini nilifanikiwa kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya sekondari huko huko mkoani Mwanza.

Mimi ni mtoto wa 2 kati ya 3 ambao tumelelewa kwa pamoja, japo nna dada zangu wengine wawili ambao hatukukuwa pamoja muda mwingi (Baba alikuwa na watoto wawili kabla hajaoa) so jumla yetu tuko watano (5)

Maisha ya nyumbani yalikuwa ya kawaida tu sio matajiri na sio masikini. Na nimekua kwenye malezi ya maadili ya kiafrika kabisa.

To cut it short

Kwenye kukua kwetu hatukuwa tukiomba hela kwa baba maana tulikua tunamwogopa, mzee alikua mkali balaa so kila kitu tulikua tukiongea na mama. Mama alikua mtu mwenye upendo sana kwa wanae na alipambana kwa namna yoyote kuhakikisha watoto wake tunasoma na kuwa vijana bora. Pesa ya kula shule, nauli, madaftari na kila kitu tulikua tukipewa na mama. Sio kwamba Baba hakuwa anatoa chochote kabisa lakini najaribu tu kuonyesha kwamba Mama ndo alikuwa rafiki yetu sana kuliko mzee. Japo fimbo na vibao vingi tumepigwa na mama kuliko mzee.

Nilipomaliza darasa sa saba, Kaka yangu alikuwa form 2 kwa wakati huo na alikuwa akisoma shule ya private. Kwa upande wangu matokeo ya darasa la saba sikuweza kuchaguliwa first selection. (Sikuwa na alama za kutosha) kama nilivyosema hapo juu nilifaulu kawaida ntafafanua mbele.

Mama alinipeleka shule ya private ambayo kaka yangu anasoma kwa wakati huo na nilifanya interview na kupewa majibu ndani ya siku 2 kuwa nimefaulu naweza kujiunga na shule hiyo ili kuendelea na elimu ya sekondari.

Nakumbuka baada ya mwezi hivi (sina uhakika sana) second selection ilitoka na nilikuwa nimechaguliwa shule flani iko wilaya ya Ilemela (Jina nahifadhi). Ilikuwa ni shule mpya kabisaa kwa kipindi hicho ziilikuwa na jina maarufu zikiitwa shule za kata. So nilichaguliwa shule ya kata.

Mama alisema niendelee kusoma kwenye shule hiyo ya private lakini niliona kama hayuko sahihi maana hali yake ya uchumi haikuwa nzuri hata ada najua alikopa. Ila kwa umri ule nisingeweza kumshauri kitu zaidi ya kusema sawa mama. Na maisha yaliendelea.

Mama yangu alikuwa mtu wa upendo sana na mchakarikaji. Niseme tu nilikuwa nampenda sana mama na nilikuwa ni yule mtoto wa mama (mamaz boy). Ilipita wiki kadhaa na mama alianza kuumwa serious. Alikuwa akilalamika siku za nyuma lakini wakati huu alisisitiza kuwa hajisikii vizuri hivyo alituaga na kuondoka kwenda hospital kwa matibabu.

Aliondoka majira kama ya saa sita nakumbuka na aliahidi angerejea baada ya matibabu.
Kuna hospital moja ipo Mwanza kwa kipindi hicho ilikua ikiitwa Mission, iko maeneo ya Ghana kama sikosei, sina hakika kama bado iko pale hadi leo.

Taarifa za mama kuumwa hazikuwa nzuri kwangu maana Mama hakufanikiwa kurejea nyumbani siku hiyo.
Mimi (Nijiite Amani…Sio jina halisi) nilikua yule mtoto ambaye hata mama akitoka ikifika saa 3 usiku hajarudi basi wasiwasi na uoga ulikua unakua mwingi.

Sasa hii siku mama hakurudi kabisa na nilikuwa na wasiwasi sana hadi hapo mama mdogo alipokuja home majira ya jioni ya kutupa habari kuwa mama amelazwa katika hospital hiyo ya Mission. Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri ilikuwa ni weekend.

Maisha yaliendelea na tulikuwa tukienda kumwona mama. Jumatatu tulienda shule kama kawaida, nilikuwa nikiondoka na kaka yangu kwani alikuwa ananizidi madarasa 2 hivyo alikuwa ananiongoza vyema tu. Kaka yangu aliwahi sana kujitambua hivyo hakuwa msumbufu sana kwa mama kama mimi.

Mimi nilikuwa hata nikitoka shule sina muda wa kusoma, ni michezo hadi usiku so hata maendeleo yangu shule hayakua mazuri sana ukiringanisha na kaka yangu.

Mama aliendelea kupatiwa matibabu kama siku 3 hivi lakini hakuonyesha nafuu hivyo alipewa rufaa kwenda Hospital ya Bugando.

Nilikuwa na ratiba kila nikitoka shule naunga moja kwa moja hadi Bugando kwenda kumsalimia mama. Nilikuwa natoka shule saa nane na nusu hivyo hadi kufika saa kumi muda wa kuona nilikuwa nimeshafika pale Hospital.

Kuna muda nilikuwa nazuiliwa na walinzi maana kwa kipindi hicho walikuwa na utaratibu wa kuzuia watoto kwenda kuona wagonjwa. Sasa mimi na umbo langu dogo dogo nilikuwa naonekana mdogo so kuna muda sikuwa nafanikiwa kuingia hadi niwe na mtu mzima.

Hali ya mama haikuwa nzuri kwakweli maana baada ya kama siku kumi hivi, Nakumbuka hiyo siku nilienda kumwona mama nikakuta amewekewa mashine ya Oxygen, ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza naona mtu kawekewa ile mirija puani.

Nakumbuka nilianza kulia pale na mama mdogo alinitoa nje maana nilikuwa nalia alafu mama ananiangalia wakati huo alikuwa hawezi hata kutoa sauti ukaisikia so alikua ananiangalia na nilikua naona kabisa anaumia kuona nalia.

Tulirudi nyumbani siku hiyo na usingizi ulikua wa shida sana nawaza mama amekuwaje. Hali ya home pia haikua nzuri kwani kwa kipindi chote hicho mama hakuwepo nyumbani.

Pale nyumbani tulikuwa na kiduka ambacho kilikuwa kinaendeshwa na mama na ndipo hapo tulikua tukipata hela ya nauli pamoja na ile ya kula shule. So wakati wote ambao mama hakuwepo hata mapato dukani yalipungua kwani bidhaa nyingi zilikua zimeisha usimamizi hakua mzuri.

Ni baada ya kama siku 2 tu nikiwa nimetoka hospital kumwona mama. Wakati huo sikua naruhusiwa tena kwenda kumwona kutokana na kile kitendo cha kulia.

Hii siku nilitoka shule nikaenda moja kwa moja home lakini ilipofika jioni baadhi wa watu waliotoka hospital walinipa taarifa kuwa hali ya mama bado si nzuri.

Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baada ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikua amefariki tayari

NITAENDELEA… Leo Leo


Usiku wake baba alipigiwa simu akiambiwa mama hali yake ni mbaya na alienda moja kwa moja hospital.
Baada ya masaa kama mawili nilishtuka kwa kelele za vilio kutoka kwa mama zangu wadogo.
Mama alikuwa amefariki tayari
Reflection kama hizi zitakusaidia sana kujua wewe ni nani na nini unataka. Tena unavyoandika ndio inakuwa profound kabisa.

Andika matukio yote, yaweke kwenye Mafungu ya miaka mitano mitano [statistical interpolation]. Kesha andika mengine uyatakayo yatakayotukia kuanzia sasa ukiitafuta miaka 30 ijayo [statistical extrapolation]. Jipange, uyafanyie kazi yajayo.

Utanishukuru baadae.

Nimekaa pale
 
Nakupa elimu ndogo kabisa, Ni baba yenu ndie alikuwa anatafuta hela za kuwalipia ada shuleni, nguo, chakula, n.k. mama yenu alikuwa anapewa ila mkimuona anavyowalipia / kuwapa mnadhani ni zake.

Nani kama mama ni misemo ya watoto / vijana ambao bado hawana familia zao kujua mfumo kamili wa jinsi mambo yanavyokwenda
Ni kweli
 
SEHEMU YA SABA (7)

Tulipoishia…


Asubuhi niliondoka na Clara alisubiri hadi bus liondoke ndo akaondoka ila alikua na maumivu makali mno na hata tembea yake haikua kawaida.
Wakati niko njiani tulikua tukichat na alinijulisha kuwa anaumwa sana, amepata hadi homa. Nilimpa pole nyingi na kumwambia ajikaze home wasijue.

Kwa upande wa Jane baada ya kumaliza form 4 alienda Dar kwa mpenzi wake baadae akaenda mwanza kwa dada yake (niliambiwa na mwenzake) lakini taarifa niliyokuwa nayo wakati naenda Advance ni kuwa Jane tayari ana mimba kubwa tu.

Tunaendelea….


Nilifika dar majira ya saa tano usiku, na hii ndo ilikua mara yangu ya kwanza kuja Dar. Aunt alituma mtu aje kunipokea na joto ndo lilinipokea vizuri.

Aunt wa Dar ana maisha yake mazuri tu na sitotaka kuongelea chochote kuhusu maisha ya kwa Aunt ila kwa ufupi sana ni maisha poa na kila mtu na time zake, mtakutana jioni muda wa kuangalia habari na kula labda

Kesho yake kuna Dada yangu alinipeleka Mwenge na Kariakoo kununua vitu vya Shule. Nilikaa Dar kama siku 4 then safari ya Mbey ikaanza.
Wakati natoka Dar nilikua na kila kitu cha shuleni. Aunt wa Dar alininunulia ( aunt wa Dar tumwite B. Mkubwa ili kutofautisha na wa Bukoba)
Account yangu ya CRDB iliwekwa laki 2 na B. mkubwa kama Pocket money ya shule then nikapewa nauli na pesa ya kula njiani. Nilinunuliwa counter Book 12, vitabu 6 na kila hitaji nilipewa. Mzee mwanza pia alinipa hela ila nilikula bata yote nilivyofika Dar ikiwemo kununua nguo mpya.

Safari ya Mbeya ilikua safi tu na nilifika Mbeya Tukuyu majira ya saa nne na nusu hivi usiku. Wakati niko njiani kuna mbaba nilikaa nae alikua ni doctor huko Kyela na alitokea kunikubali sana na tulibadilishana namba.

Changamoto ilikuja pale nilipofika Tukuyu na kujikuta nimebaki na Cash kama elfu 17 tu. Sasa nikauliza bank iko wapi, Dreva tax alinijibu “huku hakuna CRDB, kuwa linakuja gari (Mobile Bank) sijui kama niko sahihi linavyoitwa. Hilo gari huwa linakuja siku ya jumatatu tu na linatoa huduma na kuondoka”. Asee nilichanganyikiwa na sikuwa na mwenyeji yoyote Mbeya kwa wakati huo. Niliomba dreva Tax anipeleke lodge yoyote ya bei ndogo. Jamaa alinifanyia uhuni, Lodge ilikua sehemu ya kutembea kwa dak 2 tu ila jamaa akanizungusha njia ya mbali na akanipela hapo Lodge nikampa buku 3. Pale Lodge nililipa elfu 10 nikalala huku nikiwaza asubuhi naendaje Mbeya mjini maana nilikua mgeni kabisa na mfukoni nna kama elfu 4 tu.

Niliamka asubuhi nikajiandaa then nikaenda mapokezi nikamwomba jamaa aniangalizie mizigo yangu.
Nilipanda costa za Tukuyu - Mbeya nauli ilikua buku 3 kama sikosei. Safari ikaanza nami macho yangu yote yalikua barabarani nikijisemea ntakapoona ATM ya CRDB basi nashukua.
Nilishuka Mwanjelwa pale baada ya kuona ATM then nikatoa pesa kama laki hivi. Nilinunua godoro, blanketi na koti jeusi. Ile shule tulikua tunavaa full black… Yani shati white, suruali black na koti Black… suit kabisa yani.

Nikarudi Tukuyu na kubeba vitu vyangu tayari kwenda shule. Yule dreva tax nilichukua namba yake na tulikuja kuwa washkaji baadae. Alinipeleka hadi stand ya kwenda huko ndani ndani (Mbambo, Itete hadi shuleni penyewe)
Sasa pake stand nilikutana na wanafunzi kibao wanaoenda shuleni ila cha kushangaza usafiri ulikua Canter na sio mabasi… Yani mnaning’inia huko juu kwenye canter.. wanawake ndo wanakaa chini. Asee niliishiwa nguvu baada ya kusikia hivyo.
Canter inajaza balaa na mizigo ni mingi mnoo kwani watu huja Tukuyu kununua mahitaji mengi na wengi ni wafanyabiashara kule kijijini.

Safari ilianza kama baada ya masaa mawili hivi na wanafunzi tulikua tunapiga story nyingi mnoo na swali kubwa ilikua ni kuulizana we umetokea wapi. Peke yangu ndo nilikua natoka Bukoba.
Ile safari ilikua ya mateso sana. Barabara ni vumbi, madaraja ya mbao alafu barabara ina milima na kona balaa (watu wa Mbeya hususani Tukuyu wananielewa vizuri hapa)

Ilikua Gari ikilalia upande wetu nasali sana maana ukiachia zile bomba ndo uko chini hivyo
Nilianza kujuta kwanini sikusoma Bukoba tu. Baada ya masaa matatu na nusu hivi tulifika shuleni… Asee nilihisi kuna kitu kimenikaba kooni kama nataka kulia kama nimebanwa (hii hali mnaijua wengi) kwa ufupi ningekua mtoto ningelia
Shule ilikua mwisho kabisa. Yani kata ya mwisho kabisaa baada ya hapo kuna Mlima Living stone so hakuna namna utaenda kokote.

Tulipokelewa shuleni tukaonyeshwa mabweni then tukaenda kula mtaani siku hiyo maana tulifika watu washapewa chakula cha jioni shuleni pale.
Nilifanikiwa kupata marafiki wengi na maisha ya kuishi mbali na wazazi yakaanza rasmi


Tuishie hapa kwa leo

See you kesho
Huyo Mbaba Dr nahisi ataoomba kupiga tukio na wewe
 
Dogo nimepigiwa simu na wasomaji wanalalamika unachelewa kutunga episodes nyingine. Unatakiwa ushushe double double. Wewe unaendaje kulala na hujamaliza utunzi? Unaanza uvivu eeeh? Utajilaumu zaidi shauri yako.
Mbaba Dokta aliyekutana nae kwenye gari
Wakabadilishana namba
Story inaishia na Masuala ya Ushoga hii
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom