Adriel Vin
Senior Member
- Jun 25, 2020
- 148
- 748
- Thread starter
- #181
Nitaendelea na simulizi na ntaelezea every detail ili twende sawa
Ooooh.... I will.Ziwa Nyanda
Kaangalie kwenye Atlas
Uzi unasemaje huo as au nipe jina la mleta uzi nimtafute Dogo anasikitisha sana 👇👇👇
SeHEMU YA TISA (9)
Tulipoishia…
Tabia ya kwenda porini ikakua na tukaanza kucheza kamali kule. Tulikua tukicheza kamali ya karata na dau nakumbuka lilikua 100 au siku nyingine 200. Ilikua pesa nyingi kwa maisha ya shule kwani ukipigwa kama elfu 3 hivi basi wiki nzima utakunywa uji mkavu…
Nikawa na ukaribu wa mdada flani (tumwite Tina) alikua mwanafunzi wa O-level… Asee kumbe yule dada kuna mwalimu anamtaka…. Hapa nikawa nimeyatimba
Tuendelee sasa…
Tina alinijuza kuwa kuna mwalimu huwa anamtaka sana na sasa ananiulizia.
Ngoja nipunguze maelezo naona watu wamesema hayana umuhimu
Huyu Tina alinipa msala, alikuja kupata mimba shuleni alafu kila mtu akawa anasema lazima mimba ni yangu. Tulikua form 6 tayari hapo na maisha ya kucheza kamali na kutoroka shule nilishayazoea
Nilishauza zile counterbook zote 12, nilibaki na moja tu la masomo yote. Niliuza vitu vyangu vingi mnoo
Katika yooote sikuacha kwenda kanisani jumapili. Na kuna mzee mmoja alikua na mwanae yuko form 4 pale shuleni. Yule mzee alinipenda sana, akawa kila jumapili lazima aniletee matunda pale kanisani, sikunyingine samaki au dagaa. Mzee alikua akinisisitiza nisome lakini mwanae pia asome kwani wana maisha duni na ni mtu pekee kwao walikua wakimtegemea (huyu dogo nilikuja kutana nae baada ya miaka 6 hivi mbele, pia story yake nimeiachia hapa)
*Kuna kipande muhimu sana cha dada kiongozi wa Dini haswaaa, nilijikuta kwenye mahusiano nae na hata nilivyoenda chuo bado nilikua nae. Huyu Dada nilimfanyia vitu vya ajabu sana kwakweli na niseme nilipoteza mtu muhimu basi tu. Ila sasa nikileta story yake watu watasema najizungusha story iwe ndefu.
Tuendelee kwa ufupi yule Tina alikuja gundulika ana mimba na mwenye mimba sio mimi, kuna jamaa flani alipewa msala huo. Maisha yakaendelea
Mtahani wa mock wa form 6 nilifeli tena… Nilipata 3 ya mwisho…
Kwa kipindi kilichobaki niliona nikomae na shule tu. NECTA ilifika nikafaulu na baadae nilichaguliwa kwenda SAUT Mwanza
TUENDELEE, NTASOMA MAONI YA WENGI KAMA TWENDE NA SUMMARY AU NIELEZE KWA KINA MATUKIO MUHIMU HADI NIMALIZE MKASA WANGU
ASANTENI
Kabla ya saa 12 jioni ntakua nimeshusha epsode nyingine ndefuEpisode nyingne xaa ngap mkuu?
Shusha vituSEHEMU YA KUMI (10)
Tulipoishia…
Nilikamilisha taratibu za malipo yote chuoni, hostel na kila kitu kilikua poa na nilikua tayari sasa kuanza maisha mapya ya chuo.
Mzee alinipa pesa kidogo pia.
Tuendelee sasa
Maisha ya chuo yaliendelea na ndani ya wiki mbili majibu ya waliopata mkopo yalitoka.
MUNGU mkubwa nilikua kwenye list ya waliopata mkopo na nilikua nna asilimia 90+ nilifurahi sana hii siku.
Sasa nakumbuka mzee alinitext akasema kama niko free niende home kuna harusi ambayo amechanga na ana kadi 2, so moja ntaenda mimi na bro (Bro alikua likizo wakati huo na alikuja mwanza kusalimia, likizo za watu wanaosoma medical zilikua kidogo tofauti na sisi wengine)
Nilienda home kwa bashasha na mbwembwe sana maana niliona kitendo cha kupata mkopo basi maisha yangu chuo yatakua poa.
Tulijiandaa tukaenda harusini ilikua mwanza town pale, ukumbi ulikua ghorofani ila sikumbuki vizuri unaitwaje.
Tumeingia ukumbini mi hata maharusi siwajui ila nilishangaa kukutana na watu wengi tuliosoma wote primary na baadhi secondary kule mwanza (Rejea epsode 1& 2)
Nilifurahi sana kuonana na sura zile na story zilikua nyingi ikiwemo now unafanya nn, mi jibu langu lilikua straight, niko SAUT nasoma.
Tulipata meza katikati ya ukumbi na tulikaa hapo mimi na bro pamoja ma watu wengine nisiowafahamu (mzee hakua na muda na sisi, alikua na marafiki zake)
Ile furaha ya kupata mkopo ikanituma ninywe pombe. Sasa hadi wakati huu sikua nime-master unywaji wa pombe maana nilikua nakunywa mara chache sana.
Hii siku nilikunywa pombe sana na nilichanganya hadi inafika muda wa chakula mimi nilikua hoi na bro alitambia hilo. Basi akanifatia chakula, kitendo cha chakula kufika mezani tu mimi nilitapika sana baada ya kusikia harufu ya msosi na nikazima tena kama kule bukoba.
Kaka yangu alihangaika sana na mimi akanipa maji mengi, sasa issue ilikua kunitoa pale ukumbini hadi chini. Sikua na nguvu kabisa na yeye asingeweza peke yake. Mzee alishaona lile tukio na aliamua kulinda heshima yake, hakusogea hata nilipokua, alimtext bro kuwa anipeleke home. Bro alimpigia jirani yetu mmoja akaja na boda chap wakanipeleka home. Huko home hali haikua nzuri kwani niliendelea kutapika sana na baadae nikapitiwa na usingizi.
Asubuhi bro alienda kununua zile IV Fluids (Drip) akaniwekea canula mkononi then drip akatundika dirishani nikaanza kula dozi (bro alikua mwaka wa 3 wakati huo so alikua amemaster vitu kadhaa vya medical)
Mzee hakusema kitu kuhusu mimi kulewa na asubuhi alijiandaa akaenda kwenye shughuli zake.
Baada kama ya masaa manne nilikua naweza kupiga story na watu kabisa pale home ila nilikua weak bado.
Sasa siku hiyo ilikua ndo FIESTA Mwanza na ilikua inafanyikia CCM Kirumba pale.
Bro na marafiki zake kadhaa niliwasikia wakipanga kwenda FIESTA, Nikakumbuka kuna rafiki zangu wawili kule chuo walisema twende FIESTA. Sasa ikabidi nimwambie bro kuwa tutaenda wote jioni ila tukifika huko mi ntaachana nae na ntaungana na marafiki zangu. Bro alinikazia nikaona nikae kimya. Akaniwekea drip ya mwisho kisha sikujua wameondoka vipi, alinikwepa 😅.
Saa moja jioni nilikua fit na nikaanza kucheck na marafiki zangu wa chuo, walisema kuwa wataenda FIESTA na mimi nakawaambia tutakutana uwanjani. Saa tatu kamili nilikua nimejiandaa tayari na chap nikaondoka zangu ila sikua fit sana.
Nilifika CCM Kirumba nikalipa kingilio huyoo nikaingia ndani, katika zunguka zunguka nilikuatana na bro na marafiki zake walivyoniona wakacheka sana kisha bro akasema wao wana ratiba zao na mimi niendelee na zangu.
Nilikutana na marafiki zangu mle ndani saa nne na tukaanza kuvibe ila mi nilikua nakunywa maji tu.
Baada kama masaa mawili niliona kabisaa sina nguvu hata kusimama kuangalia wasanii ikawa issue. Nikaaga pale huyooo nikapanda boda hadi home nikalala.
Kesho jioni nilirudi chuo kuendelea na maisha ya kusoma.
Sasa wakati huu wote sikua na ukaribu sana na Mama mchungaji maana nilikua na mambo mengi lakini pia yule Clara alikua ashaanza kuwasiliana sana na mimi.
Clara ni binti aliyenipenda sana sanaaa na kwakweli mi kwa wakati huo sikua nampa muda sana.
Mama mchungaji aliendelea kupitia changamoto za pale anapokaa lakini Mungu ni mwema alifanikiwa kumaliza masomo yake ya certificate. Kwenye kuomba chuo ili asime diploma alichagua kimoja cha Mkoani Mara na chuo cha hapo Iringa kama sikosei (nnachokumbuka alichagua vyuo viwili) lengo la kuchagua mkoa wa Mara ilikua alitaka kuwa karibu na mimi. Mara na mwanza sio mbali sana hivyo aliamini tungekua tukionana sana.
Mimi nilimuunga mkono lakini niwe muwazi sikua namjali tena kama mwanzoni.
Hapo nilishaanza kuonana na Clara mara kadhaa na kushiriki nae tendo.
Mwaka wa kwanza wote sikutaka kujihusisha na mahusiano chuoni. Nilikua nakumbuka namna B.mkubwa alinishihi sana kuhusu wanawake chuo. (Nakumbuka alisema ukiona umeshindwa kujizui tumia kondomu)
Hivyo mwaka wa kwanza nilikua nikipoteza muda sana na Clara
Huyu Clara nilikua napajua kwao na kwetu wanamjua vizuri tu. Kuna wakati nilikua nikienda kumtembelea mzee home namshtua Clara anakuja na nilishafanya nae tendo pale pale home🤦🏿♂️
Majibu ya mama mchungaji yalitoka na alikua amechaguliwa kujiunga na chuo cha Mara kule. Hivyo alitakiwa akasome diploma yake huko.
Kwa upande wangu nilikua nishakua na ujanja ujanja wa chuo, nishajua kuvaa kama mwanachuo na nilishanunua smartphone HUAWEI Y300 kama sikosei.
Siku zilienda na tulikua tunakaribia kumaliza mwaka wa kwanza.
Kuna kitu nimesahau. Wakati niko first year nilianza mahusiano na binti ambaye alikua anasoma Moshi (MUCCOBs). Tulikuana kupitia instagram.
Kwa wakati huo nilikua situmii facebook sana na nilishahamia insta, Instagram pia nilikua na fan base kubwa sana. Nakumbuka nikiwa first year nilikua na 10k+ followers.
TUTAENDELEA
Huyu Binti wa MUCCOBs ana story yake mbeleni huko
Stori yako hata haisisimui.SEHEMU YA NNE (4)
Tulipoishia…
Yale matokeo yakafifisha ndoto zangu za kwenda Science jumla…
Tuendelee Sasa…
Familia ya pale home kwa aunt ilikua poa tu maana hakukua na challenge sana na nisingependa kugusia part hii maana sio muhimu sana.
Baada ya matokeo yale ratiba ilibadilika, ilikua hata nikitoka tuition lazima home nisome usiku, uncle (mume wa aunt) alikua lazima aje usiku kuchungulia room kwetu kama tumeamka kusoma (Kuna mtoto wa mwisho wa aunt mwingine alikua pale ma alikua primary bado ndo tulikua tunapeana kampani kusoma)
Kwa upande mwingine maisha ya kiroho pia yalikua yanakaziwa pale, kila jumapili lazima kwenda kanisani, ilikua ni lazima so nilinyooka na kuwa kijana mzuri tu, sikua na makundi kama Mwanza kule.
Turudi kwa Jane kwanza… Wakati wote ambao niko kwenye mahusiano na Jane sikua nimewahi kufanya chochote. Kuna siku tulipanga kwamba weekend twende mlimani huko ( kulikua na mlima flani una majani na miti miti na hakukuwa na nyumba karibu na maeneo yale) ukipanda huko juu unaiona Bukoba vizuri kabisaaa, mlima uko maeneo ya Buyekera karibu na shule ya msingi Buyekera. Kwa watu walioishi Bukoba mjini wanapafahamu ingawa kwa sasa mlima huo una nyumba kibao tu.
Tuliplan twende kule tukashiriki tendo wakati huo mimi ndo mara ya kwanza na mwenzangu yeye alikua ashapiga show kadhaa huko nyuma.
Maisha yaliendelea na weekend ilifika tukaenda zetu juu huko mi nilibeba maji ya kunywa tu. Tulikutana mahali na tukaanza safari.
Baafa ya muda kama 20 min tulikua kule juu tukajichimbia mahali ma story ziliendelea huku nisijue naanzia wapi.
Kufupisha, tulishiriki tendo na ndo ilikua mara yangu ya kwanza. Siwezi sema nilienjoy sana maana sikua najua mambo mengi na niliishia bao la kwanza wala sikutaka kuendelea.
Sasa baada ya yote Jane alizidi kunipenda na mimi nilikua nampenda sana kwakweli. Kule shuleni walikua wanasema tu mi napata story ila hatukuwahi kuweka wazi mapenzi yetu mbele za watu. Baadhi ya washikaji walikua na chuki na mimi kisa Jane. Jane alikua na mwili mkubwa kidogo kunizidi na alionekana kunizidi kama mwaka hivi (nilijua baadae kuwa ananizidi)
Sasa wakati penzi likikolea Jane alikua na Kaka yake ambaye nilikua tu namwona na kwa kipindi kile jamaa alikua anakula moshi (anavuta Bangi) yule Kaka yake sikuwahi kuwa karibu nae ila nilikua najua anamtaka mtoto wa aunt yule aliyefanya nijuane na Jane.
Siku natoka tuition mida ya saa 12 jioni nilikutana na kaka yake akiwa na kundi lake na wanilisimamisha nilikua naendesha baiskeli kwenda home. Jamaa alinipiga beat na kusema natoka na dada yake, atanitafuta, pale asingeweza kufanya kitu kwani tulikua road.
Asee niliogopa sana nikaenda home straight kwa Dada (yule mtoto wa aunt tumwite Tiva)
Tiva alimind sana akanambia twende, kufika kule alimfokea sana jamaa na jamaa akasema hajasema kitu kibaya kwangu na hawezi kunigusa maana sijamkosea kitu.
Kun siku tuko shuleni, muda wa break Jane alikua ananifata kwenye dawati langu na kuongozana hadi jikoni kupata chai (BUKOBA SEC ilikua na utaratibu wa kugawa maandazi na chai kwa kila mwanafunzi na ilikua buree, utaratibu uliwekwa kwa members yaani wanafunzi mnakua na makundi ya watu 12 na kiongozi ndo anafata maandazi na chai then anawagawia)
Sasa huu utaratibu sikua nimeuzoea sababu kule Mwanza hamna mambo hayo, pili sikua nimezoea sana kuongea na watu, tatu kulikua na vurugu flani hivi. Jane ndo mtu pakee alikua ananichukulia maandazi na kuniletea kwenye Table yetu pale canteen then tunakula. Siku nyingine nilikua siendi kabisa Canteen. Sasa kuna siku nilimwambia siendi yeye akatangulia then baadae akili ikanambia niende nikanunue Karanga za bubu (zilikua maarufu sana na muuzaji alikua bubu). Wakati nanunua karanga nikamwona Jane yuko Posta (Bukoba sec iko karibu na ofisi za posta) anaongea na jamaa hivi ambaye sio mwanafunzi. Wivu ukanijaa na nikachukia sana na aliniona.
Nikarudi class na sikusema kitu, jioni muda wa kutoka akaja kunichua kwa desk yangu tuindoke nikamwambia asinifate tena na asinizoee, nilikua na ujinga mwingi asee.
Jane aliondoka hakutaka kudraw atention yoyote pale maana wengi walikua hawajui kama tunadate.
Jioni alikuja home kuniulizia na akaambiwa niko Tuition. Home hawakua na wasiwasi wanajua tunasoma wote. Usiku akaja tena na nikamkazia nikasema sitaki mahusiano tena. Aliniomba msamaha na kunidanganya yakaisha.
Nakumbuka Jane alikua akiniletea pesa na vijizawadi sana.
Sasa kumbe sakata la yule kaka yake Jane kusema atanitafuta lilikua limetengenezwa na jamaa flani alikua anamtaka sana Jane ila Jane anakaza, jamaa aligundua Jane ana mahusiano na mimi.
Nakumbuka hiyo siku nikua natoka tuition, mida ya saa moja jioni giza tayari limeingia, nikiwa njiani kabisa kufika home, ile sehemu yenye shamba la miwa ambako nilikiss mara ya kwanza na jane. Nilikutana na jamaa wawili wakanisimamisha, wakati nashuka kwenye baiskeli niwasikilize asee nilipigwa ngumi moja ya uso hadi chini… Sikujua napambana nao vipi nikajikuta nimebaki chini pale kama nimezima ili wasiendelee maana wangenipasua.. Jamaa wakakimbia (mmoja alikua yule anayemtaka Jane na nilikua namjua sababu Jane aliwahi nionyesha)
Walivyokimbia nikaamka nduki nikaenda nyumbani na nilikua na uoga sana ikabidi nimwambie Aunt kuwa watu flani wamenivamia na kunipiga kisa Jane (nilikua na utoto mwingi). Aunt alichukia na akasema twende kwao Jane ila tupite kwa balozi kwanza kutoa taarifa then tukaenda kwao na Jane
Itaendelea…
🌝🌝Cjaona ya pili nakuendelea hataMkuu tuko sehemu ya nane fuatilia zote ziko hapa hapa