Maisha ya Tanzania vs Maisha ya Ulaya.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,859
Jamani sina elimi ya juu sana lakini nina miradi inayonifanya niishi mjini. Je nikienda ughaibuni nitaboresha maisha na kipato changu au nitayaangamiza? Wenye uzoefu naombeni msaada wenu.
 
Unaweza ukayaboresha au unaweza ukayadunisha. Haya yote yatategemea na malengo yako uliyojiwekea, nidhamu uliyonayo katika kuyatimiza, na jitihada ulizonazo.

Kwa ujumla kiwango cha maisha cha Ulaya kiko juu sana ukilinganisha na Tanzania kwa husasan na Afrika kwa ujumla. Ila mimi ningekushauri, kama inawezekana, uende Marekani. Ukishindwa kwenda Marekani basi jaribu hata Kanada. Ukiwa Kanada basi ni kama vile uko Marekani ingawa bado si sawa na kuwa Marekani.

Nenda Marekani kwa sababu gharama za maisha huko si kubwa kama zilivyo za Ulaya magharibi. Na hata bei za vitu mbalimbali Marekani ni nafuu zaidi kuliko Ulaya.
 
Back
Top Bottom