MAISHA YA ‘PAPO HAPO’ NI UONGO

Encryption

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
996
1,339
………….
Bila shaka umeshakutana sana na matangazo kama haya: • Jishindie shilling milioni 50 papo hapo
• Gari ya shilingi milioni 50 inakungoja wewe.
• Waweza kuwa milionea leo.
• Nk, nk
………….
Siku hizi kumeanza kujengeka tabia ya kuhimiza watu kucheza bahati nasibu kwa nia ya kushinda mamilioni ya fedha.
………..
Ndugu yangu, huko nje kuna watu wenye akili sana lakini pia ni wajanja mno.
Wakishafanikiwa kubadili mtazamo wako wa maisha, utakuwa sawa na punda wao. Hii ni hakika kabisa.
Kila kidogo utakachopata, utawapelekea wao.
…………
Hakuna maisha ya PAPO HAPO.
Huo ni udanganyifu mkubwa kabisa.
Si kwamba watu hawashindi, lakini wanaocheza ni wangapi na wanaopata ni wangapi?
Huwezi kuendesha maisha kwa kutegemea bahati nasibu.
………..
Maisha SIO bahati nasibu.
Usiishi kwa kutegemea bahati.
Maisha yana kanuni kabisa na ukizizingatia, utafika kule unakotamani kufika.
………..
Ukweli wa maisha ni kuwa, kile kidogo ulicho nacho kinaweza kukufikisha mbali.
Watu unaoona wamefanikiwa:
1. Walianza kwa kuwa na lengo (mfano, nataka niwe na biashara kubwa)
2. walianza chini;
3. walikumbana na vikwazo lakini waling’ang’ana.
4. Walianza kukua hatuta kwa hatua
…………..
Usione mtu ni maarufu leo ukatamani tu kuwa kama yeye ukidhani alikuwa hivyo toka kwanzo.
Hapana! Alianza chini kama ulivyo wewe.
Huo ndio UHALISIA wa maisha.
Ukitaka kupita short-cut, utashindwa tu.
..............
Jeremy Kitson alisema:
Hatima ya mtu si suala la bahati nasibu; bali ni suala la uchaguzi. Si suala la kulisubiria; bali ni suala la kuliendea na kuliendea na kulifikia.
……….
Huwezi kuyadanganya maisha.
Ukifanya kilicho sahihi, yatakulipa mafanikio.
Ukifanya kisicho sahihi, yatakulipa maumivu.
LAZIMA!
 
Daudi de classic ni kweli kabisa, sometime huwa nawaza sana kwa mfano hawa wachezesha michezo ya kubashili kama vile 3mzuka why mtu asipocheza muda mrefu huwa wanambembeleza kucheza tena kwa kumlagai kuwa anaweza kuwa Milionea ama kweli
Wajinga ndiyo waliwao
ushauri yeyote anaedoma hii komenti aache kubashiri.
 
Mtakaopita hapa mjifunze,hakuna kitu kama utoe Tsh500 halafu ukae miguu juu unapiga miluzi then uje ushinde million 50.never ever hata Mungu hapendi ujinga huu yaani watu wanatafuta million 1 mwezi mzima wanavuja jasho ili waipate ila wewe uipate hali yakuwa umekaa tu unasubiri upigiwe simu?....stukeni mnaibiwa!!!
 
Back
Top Bottom