Maisha Bora kwa Kila Mtanzania: Tanzania yashindwa kupunguza vifo vya watoto Masikini

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Leo hii nimesoma habari inayosema kuwa Tanzania imeshindwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara.

Nimejiuliza, tumeweka juhudi kubwa kama Taifa kujenga mfumo wa maisha ya anasa na hata katika kampeni hizi za uchaguzi, tunaahidiwa vitamanisha macho, viwanja vya ndege, meli, simu, majumba na ahadi zingine lukuki, lakin sijasikia ahadi hasa kutoka Chama tawala au kuona utekelezaji kwa ufanisi kupunguza umasikin wa lile kundi la watu ambao ni mafukara.

Sijasikia leo CCM katika kujisifu na utawala wao bora uliowaletea neema Watanzania kuwa wameweka juhudi za kulinda uhai wa Mtanzania ambaye hana uwezo wa kujitegemea na ni fukara. Leo Mtanzania huyu, atapewa kadi ya chama, kofia na fulana akipigie chama kura kwa kuwa kimeliongoza Tanzania kwa miaka 50 na Rais wetu kamleta Rais wa Marekani lakin chama hikihiki, hakiwezi mhakikishia Mtanzania huyu uhakika wa uhai wake dhidi ya magonjwa na lishe kwake na kwa watoto wake!

Natumaini habari hii vyama vya upinzani vitaziona na kuzifanyia kazi.

Tanzania yashindwa kupunguza vifo vya watoto maskini

na Andrew Chale

TANZANIA imeelezwa ni miongoni mwa nchi ambazo imeshindwa kutekeleza kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa familia maskini na fukara kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Katika ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Save the Children linaloshughulikia misaada ya kibinadamu kwa watoto duniani, kwa vyombo vya habari jana, ilieleza Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizopoteza watoto 2,800,000 katika kipindi cha miaka kumi kutokana na kutokuwa na usawa.
Mkurugenzi wa shirika hilo hapa nchini, Rachel Pounds, alisema kuwa kama kutakuwa na usawa kwa jamii, ikiwemo kusaidia familia maskini kupata huduma muhimu za afya na kupunguza gharama za matibabu na dawa kunaweza kupunguza tatizo hilo kwa familia masikini na fukara.
“Ni kwa kulenga suala la usawa tu serikali ikiwemo ile ya Tanzania zitaweza kupunguza vifo vya watoto miongoni mwa makundi yote katika jamii. Kila mtoto ana haki ya kuishi na kila serikali ina wajibu wa kuwalinda,” alisema Rachel.
Katika ripoti yake hiyo maalumu, inayojulikana kama ‘Fursa Sawa Katika Maisha’ imebainisha kuwa juhudi sawa za kupunguza vifo vya watoto miongoni mwa matajiri na maskini zinamaanisha mafanikio ya haraka ya kufikia lengo namba nne la maendeleo ya milenia.
 
we are going to have our own dubai pale kigoma na viwanja vya ndege lukuki pamoja na kwamba tuna ndege moja

hayo ya akina mama ntakuja na ahadi mpya baada ya uchaguzi
 
Kuna neno moja muhimu ambalo Rev umelisahau katika bandiko lako hili, "vinavyoepukika". Tumeshindwa kupunguza vifo vinavyoepukika vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara. Wanaweza kukuambia kuwa kila kifo ni mapenzi ya mungu hata pale ambapo watoto wanakufa au kupata vilema vya kudumu kutokana na kukosa chanjo muhimu.
 
One of the very potential and valuable resources one could ever dare to lose is children.

God bless Tanzania, God bless Africa. Amen!

Leo hii nimesoma habari inayosema kuwa Tanzania imeshindwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara.

Nimejiuliza, tumeweka juhudi kubwa kama Taifa kujenga mfumo wa maisha ya anasa na hata katika kampeni hizi za uchaguzi, tunaahidiwa vitamanisha macho, viwanja vya ndege, meli, simu, majumba na ahadi zingine lukuki, lakin sijasikia ahadi hasa kutoka Chama tawala au kuona utekelezaji kwa ufanisi kupunguza umasikin wa lile kundi la watu ambao ni mafukara.

Sijasikia leo CCM katika kujisifu na utawala wao bora uliowaletea neema Watanzania kuwa wameweka juhudi za kulinda uhai wa Mtanzania ambaye hana uwezo wa kujitegemea na ni fukara. Leo Mtanzania huyu, atapewa kadi ya chama, kofia na fulana akipigie chama kura kwa kuwa kimeliongoza Tanzania kwa miaka 50 na Rais wetu kamleta Rais wa Marekani lakin chama hikihiki, hakiwezi mhakikishia Mtanzania huyu uhakika wa uhai wake dhidi ya magonjwa na lishe kwake na kwa watoto wake!

Natumaini habari hii vyama vya upinzani vitaziona na kuzifanyia kazi.
 
Natumaini habari hii vyama vya upinzani vitaziona na kuzifanyia kazi.
Mimi ningesema natumai wananchi wataiona na kufanya chaguo lililo sahihi kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Kwasababu hilo sio geni kwa vyama vya upinzani linapigiwa kelele kila uchao.
 
Tatizo wananchi ambao ndio tungetegemea walione hili na kufanya uchaguzi sahihi ndio wanaorubuniwa na kofia na t-shirt. Zaidi ni wapinzani kuendelea kulipigia kelele suala hili mpaka hapo watu watakapoelewa kuwa maisha bora si kumiliki simu, magari n.k!
 
Labda Bajaj zilizoahidiwa zitapunguza tatizo hili jamani - zitatumika pia kuwawahisha watoto hospitali.
 
Leo hii nimesoma habari inayosema kuwa Tanzania imeshindwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara.

Nimejiuliza, tumeweka juhudi kubwa kama Taifa kujenga mfumo wa maisha ya anasa na hata katika kampeni hizi za uchaguzi, tunaahidiwa vitamanisha macho, viwanja vya ndege, meli, simu, majumba na ahadi zingine lukuki, lakin sijasikia ahadi hasa kutoka Chama tawala au kuona utekelezaji kwa ufanisi kupunguza umasikin wa lile kundi la watu ambao ni mafukara.

Sijasikia leo CCM katika kujisifu na utawala wao bora uliowaletea neema Watanzania kuwa wameweka juhudi za kulinda uhai wa Mtanzania ambaye hana uwezo wa kujitegemea na ni fukara. Leo Mtanzania huyu, atapewa kadi ya chama, kofia na fulana akipigie chama kura kwa kuwa kimeliongoza Tanzania kwa miaka 50 na Rais wetu kamleta Rais wa Marekani lakin chama hikihiki, hakiwezi mhakikishia Mtanzania huyu uhakika wa uhai wake dhidi ya magonjwa na lishe kwake na kwa watoto wake!

Natumaini habari hii vyama vya upinzani vitaziona na kuzifanyia kazi.

Hivi una uhakika na hicho chanzo cha habari?????Go to WHO and see how we are rated!!!Doh!!JF kuna waokota mambo hapa.Tunabomoa.
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000​
mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.

http://www.cms.ccmtz.org/doc/ilani.pdf
 
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000
mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.

http://www.cms.ccmtz.org/doc/ilani.pdf

Ni heri wala usingeleta hilo la Ilani ya CCM maana kila kilichoandikwa humo kina urembo wa uongo. Kama jinsi usivyoamini vyanzo vingine, ndivyo nasi tusivyoamini vyanzo vyako vya habari, Ilani ya CCM!
 
we are going to have our own dubai pale kigoma na viwanja vya ndege lukuki pamoja na kwamba tuna ndege moja

hayo ya akina mama ntakuja na ahadi mpya baada ya uchaguzi
Mimi nafikilia alipaswa apigwe manati wakati akiyasema hayo....unatuambia uwanja wa ndege wakati usafiri wa walala hoi ni treni, badala uboreshe ndiyo kwanza shirika la reli limekuwa la majaribio...asilimia ngapi ya watu kigoma wana uwezo wa kupanda hiyo ndege kama si kuwa tukana watu wa kigoma, je huo uwanja ndege yake kifisadi itaweza kutua au inaweza kutua USA na UK....CCM acheni kutufanya watanzania wote wajinga
 
Hivi una uhakika na hicho chanzo cha habari?????Go to WHO and see how we are rated!!!Doh!!JF kuna waokota mambo hapa.Tunabomoa.
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000​
mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.

http://www.cms.ccmtz.org/doc/ilani.pdf
hapa JF huwezi kuwandaya watu, kama mjini hali mbaya kiasi hiki vipi vijijini..
 
Attachments

  • Upungufu+wa+vitanda+vya+kulala+hospitali+ya+Mwananyamala+7+Oktoba+2008%5B1%5D.JPG
    Upungufu+wa+vitanda+vya+kulala+hospitali+ya+Mwananyamala+7+Oktoba+2008%5B1%5D.JPG
    33.5 KB · Views: 52
Hivi una uhakika na hicho chanzo cha habari?????Go to WHO and see how we are rated!!!Doh!!JF kuna waokota mambo hapa.Tunabomoa.
(i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000​
mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.

http://www.cms.ccmtz.org/doc/ilani.pdf

Mkuu ni kweli idadi ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano imepungua kama takwimu hizo zinavyoonyesha ila hili bandiko la hapa linazungumzia vifo hivi likihusisha wazazi wenye vipato vya chini (lowest income quintile). Bandiko hili halipingi au kukinza takwimu za kushuka kwa idadi ya vifo bali linaashiria ya kwamba idadi kubwa ya kushuka kwa vifo hivi imetokea kwa wazazi ambao hali zao za kifedha si duni
 
we are going to have our own dubai pale kigoma na viwanja vya ndege lukuki pamoja na kwamba tuna ndege moja

hayo ya akina mama ntakuja na ahadi mpya baada ya uchaguzi

Kila mtoto wa primary kutumia Computer yake mwenyewe iliyounganiswa na mtandao BY JK :becky: - sijui mgombea huyu anajua kwamba hawa hawa watoto anaotaka watumie computer ndiyo wanaendelea kufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika?
 
Hivi ufukara umeletwa na nini? kama si uvivu wa watanzania vijijini na kuzaa sana, kula sana na kuomba omba sana, kulewa sana, kuoa wake wengi na kuoza mabinti kwa umri mdogo kwa vibabu. hakika yule afanyaye kazi kwa bidii Mungu hatamwacha aangamie. jaribu kufany kazi uone kama utabaki maskini. ggoluck to chagas.
 
Mkisubiri kuletewa hayo maisha bora mtayaona, yatakuja tu, mbona hat biblia imesema msisumbukie ya kesho?
 
Remmy,
Mkuu wangu kukinga maradhi na kuepuka vifo hayana kufanya kazi kwa bidii. Nakuiomba usitake kutumia imani yako ya dini kuhalalisha mabovu ya utendaji wa serikali. Hujafa hujaumbika mkuu wangu....wabantu tunasema...tema mate..
 
Back
Top Bottom