Elections 2010 Maisha Baada ya Octoba 31..

Nicky82

JF-Expert Member
Mar 14, 2009
941
64
Tarehe 31 Octoba ni siku ambayo wakristo wengi wataamka mapema kuwahi kanisani ili wakitoka tu wakapange foleni tayari kwa kuchagua hatma ya nchi hii kwa miaka mitano ijayo. Kwa wale wasio wakristo au wale ambao hawatakuwa wamekwenda kanisani wengi wataamka tayari kuelekea vituoni na kuanzisha foleni tayari kwa kuungana na wengine kila kona ya nchi hii kuchagua hatima ya nchi hii kwa miaka migine mitano.

Maswali ninayojiuliza ni kuwa nini kitafata baada ya siku, wiki, miezi baadaye na ikiwa CCM watashinda..Je wale waliojiunga kwa Fujo JF tutaendelea kuwa nao humu jamvini au kazi yao itakuwa imekwisha? watapewa mafao yao au watapozewa???..wale wasanii ambao kwa sasa wanashabikia ccm tutawasikia wakiendelea kulilia wizi wa kazi zao ambao serikali wanayoishabikia imeshindwa kuwatetea??? watu wa DSM wataendelea kukaa kwenye foleni masaa matano kila siku na safari nzima wakilalamikia uozo wa serikali ambao watakuwa na miezi michache tangu wairudishe, au ujenzi wa fly-overs na reli utakuwa umeanza??? Je wale wapenzi wa CHADEMA humu JF wataendelea kuwa na nguvu ya ile ile ya kutetea sera zao???Kesi za EPA zitaendele pale kisutu au zitafutwa???..Je serikali itakuwa na Boom la kutosha kuwagawaia wanafunzi wa higher learing au zote zitakuwa zimeishia kwenye Uchaguzi???..Zanzibar hali itakuwaje, umoja walio nao utaendea hata kama mmoja atadai kuibiwa kura???..Bunge litakuwa na msisimko tena??? Kelele za ufisadi zitaendelea bungeni au zitabaki historia???? Maswali ni mengi ya kujiuliza, ni vema watanzania Tutapofanya amuzi tuzingatie mambo mengi zaidi ya ushabiki tu.
 
Kama kila mwananchi angetambua umuhimu wa kura yake' ya kwamba ndio silaha pekee ya kukataa ubabaishaji it doesnt matter ni babaishaji wa chama tawala au vyama vya upinzani, ya kwamba ndio nafasi yake ya pekee itakayompelekea kupata elimu bora, matibu maji na huduma za usafafirishaji asingethubutu kuiuza kwa kwa kipande cha godoro au nusu kilo ya chumvi ama sukari na fulana ya rangi ya njano na kijani!
 
Back
Top Bottom