Mahusiano na Mitandao ya Jamii

Shkamoo babu lao.

Jamani hiyo ndiyo kawaida ya binadamu..."Kipya kinyemi..."

Mambo ya mitandao ni mapya kwa jamii zote na kwa hiyo watu bado wanajifunza...

Waache wachafuke kwani, "wasipochafuka watajifunzaje"? Ila baada ya hapo lazima watajua mahali salama pa kuchezea!

Babu DC!!
 
Wanapenda wapenz wao wa zaman wajue keshapata mtu mwingine ili wawaumize mioyo.
 
Bora sie ambao huwa hatuweki picha yoyote ile yangu au ya nani
 
Mi nadhani issue si kuwa muwazi au msiri... ila unakuwa muwazi na nani...kuna watu wana wapenzi lakini wamejituliza na wapenzi wao...sasa hata wakiamua ku share their happiness na marafiki kuna ubaya gani? unajua ukipenda kweli kweli you would like the whole world to know...that's natural

Kuna wale wenzangu na mie kwa mwaka wapenzi kumi...

Sasa hata uweke status gani haibadili uhalisia wa tabia ya ntu na ntu...
Kuna watu wasiri lakini wanajulikana...wao kutwa wanaweka 'complicated' na 'single' kumbe maana yake hata wenyewe hawajielewi wako na nani...na jamii ndio kabisa haiwaelewi...hivyo hizi status hazibadili tabia...ni jinsi ulivyo...
 
Ulisomea mahusiano ya mitandao ya kijamii? On point kabisa.

Miss Kim

Sielewei hii kitu na hawa watu huwa wanafanya wakifikilia nini?? Mwanznoni mwa mwaka huu nilifanikiwa kupata mpenzi mmoja ambaye nilitokea kumpenda kwa dhati. Huyu binti alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa katimka kusikojulikana na baada ya jitihada za kumtafuta kukwama ndo tukakutana. Kwa siku za mwanzo akawa anahangaika kuweka picha zake na maandishi kibao ooohh nimekumiss, mara anaweka zawadi alizopewa na maneno kibao. Mwisho wa siku akaanza kuweka picha za kuvunjika mahusiano. Kwa kuwa nampenda nikala timing kule kinuke na mimi niingie rasmi. Baada ya ombi langu kukubaliwa nikaanza kupewa promo WhatsApp na mambo mengi yaliyonifanya niamini kuwa sasa ametua na hapa hatoki. Nikawa kwenye harakati za kuandaa masuala ya posa na vitu vingine na huku nikiwa nimeshatumia karibia 2mil kwa ajili yake. Siku moja akaniomba kiasi kikubwa cha hela nikashindwa kumpa kwa kuwa hakutaka kunieleza ni za nini. Nikamwambia usiponiambia ni za nini sitaweza kutoa, heeehh si ikawa nongwa. Nikipiga simu anapokea lakini majibu yanakuwa ya ovyo ovyo, mara stori stori ziwe fupi na tukipanga kukutana anakuwa na ratiba nyingi kiasi cha kuniweka pending saana. Mi kuona hivyo nikapunguza matumizi kwa kuwa kengele zilianza kulia kwenye kichwa change.
Heee, si ghafla nimepigiwa simu naambiwa mahusiano yetu yamefika mwisho na wala hataki hata urafiki na mimi. Kwa hiyo nikapigwa kibuti cha nguvu na baadae line ikabadilishwa mtu kapitiliza hukooo anakokujua yeye.
Nilikaa na kujiuliza maswali kibao nikikumbuka picha tulizopiga pamoja na raha tulizokula pamoja iweje ghafla amegeuka na kutimua mbio.
Baadae nikapata jibu la haraka na la kutia faraja na nikakumbuka maneno aliyonitamkia mwenyewe kuwa nimempa raha ambazo hajawahi kuzipata, nikasema sawa nenda mwana kwenda. Nina reserve ya dola na madafu na nimemaliza mjengo wangu wa kisasa ambapo nilikuwa nimemtengea mazingira yake kwa ajili ya kuoga na kujitengeneza sasa kaenda anakokujua yeye.
Nitazifurahia mali nilizopewa na Mungu na kasha nitapata mwanamke atakayekuja kuwa faraja yangu, hao sweetie kwenye whatsapp endeleeni nao nyinyi wa kizungu mimi ataaa!!!!
 
Last edited by a moderator:
hawawezi kujifunza wala kujirekebisha katika hilo maana ni nature, ni sawa na kumwambia mwanamke asipige vigelegele kwenye harusi

wanawake wa kizazi cha dot.com hawajui kupiga vigelegele mkuu, tutavimiss sana kwenye harusi zijazo.
 
Back
Top Bottom