Mahusiano, mapenzi, urafiki je mambo haya ni lazima yafuatane au ni vitu vitatu tofauti ,Je kipo kinachoweza kukosekana au kisiwepo au kikawepo kimoja tu na vingine visihusishwe ,Kivipi ?
Naona mnabangaiza tu Ila ukweli bado hamjauona katika hayo mambo matatu ,kwa upande wangu naona urafiki ni kitu kingine na uhusiano ni kitu kingine na mapenzi ndio kabisa ila kuna product ambayo ndio itajumuisha yote hayo.
Hebu yapime haya yafyatayo :-
Hamuwezi kuwa marafiki halafu mkawa wapenzi wala hamuwezi kuwa na uhusiano halafu mkawa marafiki.
Ndugu hawezi kuwa rafiki wala mpenzi ,mke hawezi kuwa rafiki wala mpenzi wako ,jamani huwezi kusema huyu ni mpenzi wangu ,ukisema hivyo tu akili ya mke inaweza ikaruka na usiku pasikalike. Endeleeni nawapa muda mtafakari ,Mwiba
Unaanza Uhusiano halafu urafiki halafu ukimaliza kunakuja kupendana na hapo kukizidi kunaweza kukatoa mke.natumai mumeiona tofauti .Naona mgomba mnauita mdizihahaha, mkuu mwiba hapo ndo umekoroga kabisa, yaani umefananisha utamu wa sukari na asali, ssa mke asipokuwa mpenzi wako anakuwa nani tena, au ndo huwa mnajifaragua kuwaita binti masudi sijui mama hepi, kwa siye tulioona mwanga kidogo ni wapenzi tu, hebu chunguza chunguza mahsuiano ambayo mke ni rafiki na mpenzi, utaona yana afya bila mgogoro; eeh..